Thursday, 19 April 2018

Trump Atishia Kujiondoa Katika Mazungumzo na Kim Jong un

Trump Atishia Kujiondoa Katika Mazungumzo na Kim Jong un
Rais wa Marekani Donald Trump anasema kuwa iwapo mazungumzo yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un hayazai matunda 'atainuka na kuondoka katika mazungumzo hayo'.

Katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, yeye na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe walisema kuwa shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini ni sharti iendelee kwa kukataa kusitisha utengezaji wa silaha za nyuklia.

Bwana Abe yuko katika mgahawa wa rais Trump wa Mar-a-Lago resort mjini Florida kwa ,mazungumzo.

Mapema , bwana Trump alithibitisha kwamba mkurugenzi wa CIA Mike Pompeo alifanya ziara ya kisiri hadi Korea Kaskazini ili kukutana na Kim Jong Un.

Alisema kuwa bwana Pompeo aliweka uhusiano mzuri na bwana Kim ambaye bwana Trump alimuita 'mtu mdogo' na kwamba mkutano wao ulifanyika vizuri.

Ziara hiyo iliadhimisha mawasiliano ya juu kati ya Marekani na Korea Kaskazini tangu 2000.

Mkutano huo kati ya Trump na bwana Kim unatarajiwa kufanyika kufikia mwezi Juni. Maelezo ikiwemo eneo litakaloandaa mkutano huo bado yanaendelea kufanyiwa kazi.

Rais Trump alisema katika mkutano wa pamoja kwamba iwapo anadhani kwamba mkutano huo hautafanikiwa basi hatoshiriki na kwamba iwapo mkutano huo umefanyika na haoni matunda yake basi atasimama na kuondoka.

''Kampeni yetu ya shinikizo itaendelea hadi pale Korea Kaskazini itakapositisha utengezaji wa silaha za Kinyuklia'', aliongezea.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search