Thursday, 5 April 2018

WATOTO WAWILI WAFA MAJI WAKICHEZA KWENYE BWAWA


Watoto wawili wenye umri wa mwaka mmoja wamefariki dunia baada ya kuzama katika bwawa lililopo katika katika kitongoji cha Mwandu,kijiji cha Buchama kata ya Tinde,tarafa ya Itwangi wilaya na mkoa wa shinyanga. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule amesema tukio hilo limetokea Jumapili Aprili mosi,2018  asubuhi ambapo watoto hao waligundulika wakiwa wamekufa maji baada ya kuzama ndani ya bwawa la maji wakiwa wanacheza ndani ya bwawa hilo. 

Amesema watoto hao wawili ambao ni wa familia tofauti ni Sliva Mhoja mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi nane mkazi na Odisia Lugangula mwenye umri wa mwaka na miezi tisa wakazi wa Buchama. 

Kamanda Haule amekitaja chanzo cha tukio hilo kuwa ni watoto kucheza kwenye bwawa na kisha kuzama. 

Amesema miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na mganga wa serikali na kisha kukabidhiwa kwa ndugu kwa mazishi. 

Kamanda Haule anawaasa wazazi, walezi na ndugu kuwa karibu sana na watoto wadogo hasa kufuatia mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga na hivyo kusababisha kuwepo kwa mabwawa mengi ambayo ni hatari kwa watoto wadogo wanaocheza maeneo hayo au kuogelea.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search