Monday, 30 April 2018

WATU SABA MBARONI KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA

Watu saba wakiwamo waganga wawili wa jadi, wanashikiliwa na polisi wilayani Igunga mkoani Tabora kwa tuhuma za kupiga ramli na kusababisha familia tatu kukosa makazi baada ya nyumba zao kuteketezwa kwa tuhuma za kishirikina.


Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa amewataja waganga hao kuwa ni Chemani Ndishiwa (79) na Nzali Mayunga (40).

Wengine waliokamatwa ni Masanja Seni (65), Kasura Msomi (31), Michael James (19), Dotto Lukelesha (41) na Samwel Jonas (18) wote wakazi wa kijiji cha Mwakwangu.

Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea juzi Aprili 28, 2018 saa tano usiku katika kijiji hicho baadhi ya wananchi walikwenda kwa waganga hao wawili kupiga ramli na kuambiwa kijijini wapo baadhi ya familia ni wachawi.

Amesema baada ya kuelezwa hivyo, baadhi wa wananchi waliamua kukodi vijana kwa kuwalipa fedha na hakuweza kutaja kiwango waliokwenda kwenye nyumba ya Luli Lukeresha na kuichoma.

“Baada ya kufanya unyama huo, vijana hao walikwenda tena katika miji mingine ambayo waliichoma na kutoweka ingawa wananchi walitoa taarifa polisi Igunga,” amesema.
Na Robert Kakwesi, Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search