Thursday, 19 April 2018

Wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge PAC na LAAC wapinga wanaojibu ripotiya CAG kabla ya kupelekwa Bungeni

Wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge PAC na LAAC wametoa utaratibu ambao ripoti ya CAG hupitia kabla ya kuletwa bungeni.
  • Magufuli na Serikali kupitia maafisa masuhuli wake hupewa siku 21 na CAG ya kupinga ripoti yake. Kwa mujibu wa maelezo ya wenyeviti hao maafisa masuhuli walishindwa kuelewana na hatimaye kushindwa kumshawishi CAG kwa kushindwa kujieleza kwa ushahidi wa 1.5 Trillion ziko wapi na zimetumika vipi.
  • Kamati za kudumu za Bunge PAC na LAAC kuwahoji maafisa masuhuli kuhusu hoja zilizoshindwa kujibiwa kwa CAG na endapo ushahidi utatolea basi ripoti hurudishwa kwa CAG na akiridhika hufunga ripoti na kuipeleka bungeni. Baada ya hapo ripoti hiyo haiwezi kujibiwa tena na mtu yeyote. Polepole kazi unayofanya ilishafungwa.


Kwa mujibu wa Wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge PAC na LAAC , serikali iliiitwa na wataalamu wake kutoa ushaihidi wa vielelezo ni wapi zipo 1.5 Trillion walishindwa kufanya hivyo. Ukiona manyoya ujue ameliwa. Video nyingine unaweza tembelea instagram hapo chini

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search