Thursday, 19 April 2018

ZARI AMMWAGIA MATUSI DIAMOND PLATNUMZ MTANDAONI

Aliyekuwa mpenzi wa Diamond Platinumz ambaye ni mama wa watoto wawili wa msanii huyo, Zari The Boss Lady ameshindwa kuficha hasira zake na kumshambulia kwa matusi mtandaoni.

Mashambulizi ya Zari aliyoyatoa kupitia snapchat, muda mfupi kabla hajaelekea kanisani yalionekana yakihusishwa na ujumbe ambao Diamond aliuandika kwenye Instagram kuhusu wanawake akipigia debe tukio linalofanywa  na Zamaradi Mketema.

“Ikiwa Mama yangu alinilea Pekee hadi kufika hapa…Naamini Mwanamke ni Kiongozi bora Mwenye kuweza kuleta Maendeleo na Furaha ya Kweli Ulimwenguni….Please Tag wanake wote Wapambanaji na Wapenda Maendeleo waambie @zamaradimketemaKawaandalia jambo Kesho [leo],” aliandika Diamond.

Dakika chache baadaye, Zari aliweka ujumbe wake uliojaa hasira akitumia maneno makali na kumuita Diamond ‘mjinga’. Ingawa hakumtaja jina, kitendo cha kumkosoa kwa kushindwa kuwaona watoto wake kwa muda mrefu kinaonesha kuwa anayezungumziwa ni baba Tifah.
Baadaye, Zari aliweka picha inayomuonesha akiwa mbele ya kioo na nguo nyingi na kuandika ujumbe kuwa ni muda wa kanisani.

“Some manages need to do quality assurance before their artist alter nonsense for public whatever… when last did you see your kids I believe they forgot all about you dummy… Think before you caption. Idiot. Mxuiiii,” aliandika.

Kwa tafsiri isiyo rasmi, “Mameneja wengine wanapaswa kuhakikisha ubora kabla wasanii wao hawajaweka upuuzi kwenye mitandao ya kijamii kwa kupata kiki kivyovyote… hivi ni lini mara ya mwisho umewaona wanao.. Nina amini wamesahau yote kuhusu wewe mpuuzi…. fikiria kabla ya kuandika kwenye picha. Mjinga.”

Zari alitangaza kuachana na Diamond, akaiachia rasmi funguo za ikulu ya WCB ya Madale na kuhamia nchini Afrika Kusini.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search