Tuesday, 22 May 2018

AJALI YAUA WATENDAJI WA TIC

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa ajali maeneo ya Msoga wilayani Chalinze na kusababisha vifo vya watu wawili na mmoja kujeruhiwa.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shana amesema ajali hiyo imehusisha gari ya serikali STK 5923 aina ya Toyota land cruiser lililongana na Scania T620 AQV ambaye dereva wake alitoweka kusikojulikana na waliofariki ni watendaji wa kituo cha uwekezaji TIC walikuwa wakielekea Jijini Dodoma.

Kamanda Shana amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Gari ndogo alikuwa akikwepa mashimo yaliyokuwa barabarani na kwakuwa lilikuwa kwenye mwendo mkali liliparamia lori.

Kamanda amewataja waliofariki kuwa ni Martin Lawrence (36) na Zacharia Nalinga (49) ambao wote walikuwa kwenye gari aina ya STK pamoja na Dereva wao ambaye yuko mahtuti.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search