Wednesday, 23 May 2018

ASKARI WANNE WANASWA NA TAKUKURU KWA RUSHWA

Image result for askari wa wanyama pori
Askari wanne wa pori la akiba la Mkungunero Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh5 milioni za wafugaji wa Kijiji cha Irkiushiboir Kata ya Makame Wilaya ya Kiteto mkoani Mnyara.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Mei 22, 2018 Kamanda wa Takukuru wilayani Kiteto, Julius Chacha amesema askari hao wamekamatwa Mei 20, 2018 wakiwa na bunduki nne aina ya SMG huku wakiwa na mifugo 200.

Amewataja askari hao kuwa ni Godfrey Matheas, Martenus Mahoka, Augustino Sadiki na Aphrahimu Polepole.

Amebainisha kuwa baada ya mmoja wa wafugaji kuombwa rushwa na watu hao, uliwekwa mtego na kukamatwa askari hao wakiwa wamepokea kiasi hicho cha fedha na kwamba walikuwa na mifugo zaidi ya 200 mali ya familia saba za wilayani Kiteto.

“Mtego huo uliwekwa kabla ya askari hao kuikabidhi mifugo kwa wenyewe. Tuliwakamata wahusika wakiwa wameshikilia mifugo hiyo katika kitongoji cha Ilchura kijiji cha Irkiushiboir wilayani Kiteto,"amesema Chacha.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search