Friday, 18 May 2018

Balozi Possi awasilisha hati za utambulisho kwa Papa Francis, Vatican

Possi.jpg
UTAMBULISHO RASMI: Balozi wa Tanzania, Dkt. Abdallah Saleh Possi, amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican jana Mei 17.

Balozi Possi ambaye kituo chake cha kazi ni nchini Ujerumani katika mji wa Berlin pia utahudumia maeneo mengine tisa ya uwakilishi, ikiwemo Vatican.

Kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na viongozi muhimu wa Vatikani, wakiwemo Askofu mkuu, Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na ushirikiano wa kimataifa, Askofu Mkuu Angelo Becciu na Katibu Mkuu Msaidizi wa Vatican.

Baada ya uwasilishaji hati, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na jumuia ya Watanzania waishio Vatican.

Dkt. Possi aliwaeleza Watanzania hao kwamba wana jukumu kubwa la kutumia, nafasi zao kuhakikisha nchi ya Tanzania inadumu katika misingi ya uadilifu, umoja na amani ambavyo ni misingi muhimu ya maendeleo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search