Monday, 28 May 2018

BOKO AFUNGUKA HAYA

NAHODHA wa Simba, John Bocco amekiri kuwa uhamisho wake kutoka Azam umemfungulia dunia na kuona kuwa alikuwa na uwezo mkubwa bado wa kuendelea kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara.

Tangu Bocco aanze kucheza Ligi Kuu Bara akiwa na Azam FC, hakuwahi kuihama timu hiyo kwa miaka tisa kabla ya kutimka mwaka jana na kujiunga na Simba aliyoiongoza kutwaa ubingwa msimu huu, akiwa kama nahodha.

Bocco aliliambia Mwanaspoti kwamba Simba ni klabu yenye ushindani wa ubingwa na inatazama fursa za kucheza klabu bingwa Afrika, kitendo ambacho anadai kimempa nguvu ya kutambua uwezo wake na kupata hamu ya kujituma zaidi.

“Simba ni timu yangu ya pili kuichezea Ligi Kuu na msimu huu kwangu umekuwa wa kunipa hatua ya kutamani kufanya zaidi ya mchango nilioutoa. “Kufunga mabao 14 mpaka sasa si haba, bila shaka nitakuwa nimeweka rekodi ya kukumbukwa na wengine ambao watakuja nyuma yetu, lakini kubwa zaidi imeniongezea ari ya kujiamini kwamba nina kiwango cha kuendelea kuonyesha ufundi wangu,” alisema.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search