Thursday, 10 May 2018

BREAKING NEWS:- MBUNGE SUGU NA KATIBU WA CHADEMA KANDA YA NYASA WAMEACHIWA HURU


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiwa huru leo Alhamis Mei 10,2018 jijini Mbeya.
Image may contain: 2 people, people smiling, people sitting and indoor
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kulia), Mbunge wa Mbeya Mjini 'Sugu' (katikati) na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wakiwa nyumbani kwa Sugu baada ya kutoka jela
Awali Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda na viongozi wengine wa chama hicho wamefika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya kuwapokea Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.


Image may contain: 7 people, people smiling, outdoor
Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search