Tuesday, 22 May 2018

CHADEMA YAFUKUZA WANACHAMA KWA USALITI

Image result for chadema
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama watatu wa chama hicho kwa kile kilichodaiwa kuwa ni usaliti ndani ya chama.

Waliofutwa uanachama ni pamoja na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Getrude Ndibalema na Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Kilimanjaro, Dickson Kibona. 

Akizungumza leo Mei 22,2018 katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha, Ole Sosopi amesema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kufuata taratibu zote za kuwahoji kupitia tume iliyoundwa.

Amesema viongozi hao wamehojiwa baada ya kuwepo tuhuma za usaliti ambazo ni kosa kwenye chama hicho, Sosopi amesema Bavicha imeridhia kuwaondoa wanachama hao baada ya kujiridhisha kwa makosa waliyoyafanya.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search