Wednesday, 2 May 2018

FAMILIA YA HECHE YAKUBALI KUMZIKA NDUGU YAO

Familia ya Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, John Heche imekubali kuuzika mwili wa mdogo wake Suguta Chacha baada ya kijana huyo kufariki kwa kuchomwa kisu na Polisi usiku wa Aprili 26 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Heche amesema familia itaweka wakili ili kuhakikisha haki ya marehemu Suguta Chacha inapatikana.

Aidha Mh. Heche ameweka wazi kwamba kama familia hawahitaji fidia yoyote kutoka kwa Jeshi la Polisi kutokana na tukio hilo.

Pamoja na hayo Mbunge huyo ameonyeshwa kushangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba kutoguswa na msiba huo ikiwa ni pamoja na kushindwa kumpa pole.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search