Tuesday, 22 May 2018

Harry na Meghan watoa picha rasmi za harusi yao

group photograph of Prince Harry and Meghan surrounded by bridesmaids and pageboysHaki miliki ya pichaDUKE AND DUCHESS OF SUSSEX
Image captionKulikuwa na watoto wasimamizi wa harusi kumi wakiwemo Bintimfalme Charlotte na Mwanamfalme George
Mtawala na Mke Mtawala wa Sussex, hary na Meghan, wametoa picha rasmi za harusi yao ambayo ilifanyika Jumamosi.
Picha hizo ambazo zilipigwa na Alexi Lubomirski zinajumuisha picha moja ya pamoja inayowashirikisha watoto waliosimamia harusi hiyo pamoja na jamaa za karibu, wakiwemo wazazi na Malkia.
Wawili hao wangependa kushukuru kila mmoja aliyehudhuria sherehe yao Jumamosi, Kasri la Kensington imesema.
"Wamefurahishwa sana na picha hizi rasmi," taarifa hiyo imeongeza.
Harry and Meghan on the stepsHaki miliki ya pichaDUKE AND DUCHESS OF SUSSEX
Bw Lubomirski, aliyepiga picha rasmi za kuchumbiana kwa wawili hao alisema imekuwa heshima kubwa kwake kupiga picha na kunakili "safari yao ya mapenzi".
"Hii imekuwa sura ya kupendeza sana katika maisha yangu kikazi na kimaisha, ambayo sitaisahau kamwe," amesema.
group photograph of Prince Harry and Meghan surrounded by familyHaki miliki ya pichaTHE DUKE AND DUCHESS OF SUSSEX
Image captionMeghan's mother Doria Ragland was the only member of her family to attend the wedding

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search