Thursday, 31 May 2018

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT MUJIBU WA SHERIA 2018 TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limefanya uteuzi wa wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kutoka shule zote za Tanzania Bara kwa mwaka 2018, kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.


Sanjari na uteuzi huo, JKT limewapangia Makambi ya JKT watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01-10 June 2018.

Wahitimu hao, wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, Nachingwea- Lindi na JKT Mtabila – Kigoma.

Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya Ruvu JKT iliyopo mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia wa jamii hiyo.

Vijana watakaochaguliwa watatakiwa kujigharamia nauli za kwenda na kurudi kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa wakiwa na vifaa vifuatavyo:

  1. Bukta ya rangi ya Dark blue yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu. Aidha bukta za wanawake zinatakiwa kuwa na lastic magotini.
  2. Raba za michezo zenye rangi ya kijani.
  3. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  4. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  5. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangwa kwenye mikoa yenye baridi.
  6. Track Suit ya rangi ya kijana au bluu

Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote walioteuliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza Uzalendo, Umoja wa Kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na Utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

Orodha kamili ya majina ya vijana na makambi ya JKT waliyopangiwa vinapatikana kwenye tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI  KUANGALIA MAJINA YA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA KWANZA  2018  

  BULOMBORA JKT-KIGOMA                    RWAMKOMA JKT -MARA                  MSANGE JKT-TABORA

  KANEMBWA JKT-KIGOMA                      MTABILA-KIGOMA                            RUVU JKT-PWANI

  MAKUTUPORA JKT- DODOMA                MGAMBO JKT-TANGA                      MARAMBA JKT- TANGA

  MAFINGA JKT- IRINGA                          NACHINGWEA-LINDI                       MLALE JKT -RUVUMA

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search