Monday, 21 May 2018

HIZI NDIZO SABABU ZA ABDUL NONDO KUTOKUKATA RUFAA

Wakili wa Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Abdul Nondo, Jebra Kambole amefafanua kuwa sababu kubwa ya kutokata rufaa baada ya Hakimu wa kesi ya mteja wake kugoma kujitoa kwenye kesi hiyo ni kutokana na kuwa huo  ulikuwa ni uamuazi mdogo ndani ya kesi kuu. 

Akizungumza Wakili Kambole amesema kuwa ingawa hakimu huyo amegoma kujitoa kwenye kesi hiyo watasubiri mpaka mwisho wa shauri hilo ili kuona kama maamuzi hayatakuwa ya haki ndipo watakapokata rufaa ya shauri zima.

"Sheria zetu zinaruhusu kwamba hakimu ndiye mwenye kuamua kuendelea kuwepo au kujitoa. Lakini Hakimu Mpitanjia amesema kwamba atatenda haki. Sisi tumekubali na atujakata rufaa kwa sababu ni mjaamuzi madogo kwenye kesi kuu. Kama tutakata rufaa kwenye kesi kuu na haya manung'uniko pia tutayajumisha kwenye rufaa ya kesi kuu," Kambole.

Pamoja na hayo Kambole amesema sababu kuu iliyompelekea Nondo kuandika barua ya kutokuwa na imani na Hakimu ni kutokana na ukaribu aliokuwa nao Hakimu pamoja na Mkuu wa upelelezi kitu ambacho kinatia wasiwasi wa haki kutendeka.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search