Friday, 4 May 2018

Mahakama Kuu yazizuia Kanuni za Maudhui Mtandaoni kutumika hadi Mahakama itoe uamuzi

1EBA9018-D387-478E-ADCF-7B67DF19CF9D.jpeg
Mahakama Kuu kanda Mtwara leo imetoa zuio la muda(Temporary Injuction) dhidi ya matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulations) ambazo matumizi yake yamekwishaanza na tarehe ya mwisho ya bloga na mitandao kuridhia ilikuwa kesho tarehe 5 May 2018.

Maombi hayo yaliyowalishwa mahakamani na waombaji 6 wakiwemo Jamii Media, Legal and Human Rights Cente(LHRC), THRDC, MCT, TAMWA na TEF.

Katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo(Judicial review) washitakiwa ni Waziri wa Habari, Tanzania Communication Authority (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG).

Katika maombi ya msingi waombaji wameiomba Mahakama kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa vigezo hivi:
i) Waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake (Ultra vires)
ii) Zinakiuka kanuni za usawa (Natural justice)
iii) Kanuni hizo zinapingana na Uhuru wa kujieleza (Freedom of Expression) Haki ya kusikilizwa(Rights to be heard) na haki ya usiri( Right to Privacy)

Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa tarehe 10 Mei 2018
Mtwara.png Mtwara C.png

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search