Monday, 28 May 2018

MANYARA AKUMBUKA MANYANYASO YA YANGA

Afisa Habari wa Klabu Bingwa Tanzania Bara, 2018/2019Simba, Haji Manara leo amekumbukia machungu ya majina ya utani waliyokuwa wakipatiwa na watani zao wa jadi, Klabu ya Yanga na kuwauliza kama kwa sasa wana uwezo wa kuendelea na kuwaita majina hayo likiwepo lile la 'wa Matopeni'. 

Manara ameweka wazi kuwa amekumbuka kauli hizo na kwamba kwa sasa wanapaswa kutulia ili aweze kuwanyoosha kwani anaamini kuwa Mungu ni fundi kwenye kila jambo.

"Zama za kusema sisi wa matopeni nyie wa kimataifa bado zipo? nimekumbuka ile kauli ntasajili wachezaji wenu wote kazi yao iwe kwenda coco beach..au ile ya kumpokea kocha airport wakati wetu tunampokea Ubungo" Manara.

Manara ameongeza "Au niwakumbushe lile jina la kutuita cc wazee wa Yutong!! Hakika Mungu ni fundi sana..zamu yetu hivi sasa..tulieni kidume niwanyooshe..".

Utani wa Haji Manara kwa Yanga ni muendelezo wa utani wake tangu simba ilipotangazwa kuwa bingwa wa VPL 2018/2019 baada ya kuwavua ubingwa huo watani zao hao.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search