Thursday, 31 May 2018

MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI ABAKWA NA KISHA KUUAWA
Mtoto Sharon Mwende, mwenye umri wa miaka nane amebakwa na kisha kuuawa katika eneo la Kithimu-Embu nchini Kenya baada ya kupotea kwa siku moja.

Kwa mujibu wa Citizen Kenya, mwili wa Sharon ulipatikana Jumanne Mei 29, 2018, umbali wa takribani mita 50 kutoka nyumbani kwao, baada ya wazazi kutoa taarifa za kupotea kwa mtoto huyo katika kituo cha Polisi Embu na kituo cha redio Wimwaro Fm. 

Mtu mmoja aliyekuwa anatafuta kuni nje ya makazi yake ndiye aliuona mwili wa Sharon na kuamua kutoa taarifa kwa wanakijiji wenzake.

Sharon alikuwa mwanafunzi wa wa darasa la pili katika shule ya msingi Kithimu, na kwa mujibu wa baba wa mtoto Nicasio Njue, amesema kwamba mwanae Sharon, alirudi kutoka shule Jumatatu jioni Mei 28, 2018 na aliondoka lakini hakufanikiwa kurudi nyumbani. 

Akithibitisha taaarifa hiyo Kamanda wa Polisi, wa eneo la Embu, Muhamed Juma, amesema uchunguzi wa awali umeonesha kwama Sharon alibakwa kabla ya kuuliwa na kuongeza kuwa walikuta mwili wa mtoto huyo ukiwa na majeraha na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kumtamfuta mtuhumiwa.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search