Wednesday, 16 May 2018

MWANDISHI WA HABARI ATEKWA , ATESWA

Mwandishi wa habari wa kujitegemea jijini Arusha, Lucas Muyovera amenusurika kuuawa kwa kipigo baada ya kutekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumatatu Mei 14,2018.

Mwanahabari huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru akipatiwa matibabu inaelezwa hali yake ni mbaya baada ya watu hao wapatao watano kumteka Jana majira ya saa tatu usiku katika eneo la Ngulelo jijini Arusha.

Kwa mujibu wa Mwandishi huyo watu walimpakia kwenye gari yao na baadaye kumpeleka katika mto ambao hajaufahamu na kuanza kumshambulia wakiwa wamemvua nguo zote na kumdhalilisha.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha Claude Gwandu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

"Ni kweli Mwandishi mwenzetu,Lucas Myovela wa kituo cha Sunrise cha jijini hapa jana usiku alitekwa,akapigwa sana,akapigwa picha za video akiwa uchi na kisha akalazimishwa kutoa password ya simu yake wakampora pesa, Issue iko Polisi na watuhumiwa wamekamatwa,bado tunafuatilia kwa karibu",amesema Gwandu.

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limethibitisha tukio hilo likidai bado wanafanya uchunguzi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search