Thursday, 31 May 2018

NATAKA KUZAA -SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA


MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
Nilicheka sana.
Na hivyo ndivyo siku zetu zilivyokuwa na mwisho wa siku baba alinipigia simu.
“Sociolah mwanangu tumekumisi tunaomba urudi nyumbani.”
“Baba nafurahia sana kuwepo huku baba natamani kuendelea kuwepo zaidi
nimewamisi sana pia naomba uniongezee wiki moja tu.”
“Hapana mwanangu wiki moja ni nyingi zaidi naomba urudi nyumbani.”
“Nitarudi baba wala usijali.”
“Sawa.” Baba alikata simu lakini alionesha kutokuridhika.
Niliendelea kukaa na Frank Ifakara na familia yake walinipenda sana nilifanya kazi
zote za nyumbani ambazo hata kwetu sikuweza kuzifanya. Nilipika, nilifua nguo
za familia, nilifanya usafi, nilienda shamba, nilienda kazini kumsaidia mama kuuza
vitu sokoni na kufanya shughuli nyingine ndogondogo.
Watu wengi walikuwa wakinishangaa kwa maana sikuonekana kufanania na hali
hiyo, hata hivyo Frank alikuwa akijisifia sana na alipenda kutembea na mimi hicho
kitu ndicho kilikuwa kikinipa amani sana nilijiona kupendwa sikujali hali ya
maisha ilivyokuwa.
Kwa siku chache tulizokuwepo familia ilianza kupendeza.
Tuliweza kula chakula kizuri na hata mavazi pia yalikuwa mazuri mama yake
alinipenda sana.
Alinitembeza sehemu mbalimbali za Ifakara tulienda maeneo kama daraja la mto
Kilombero ambalo ndiyo kwanza lilikuwa limeanza kujengwa tukaenda na maeneo
mengine mazuri ya kuvutia hakika nilijisikia faraja sana hasa kuwa pembeni yake.
Mara kwa mara mama yangu alikuwa akinipigia simu.
“Mwanangu tumekumisi tunaomba urudi nyumbani.”
“Nitarudi mama wiki hii haiishi lazima niwe nimerudi.”
Niliendelea kuwatia moyo ingawa ilikuwa bado sikufikiria kurudi nyumbani.
Ilikuwa ni jioni ya siku moja tulikuwa tumekaa kwenye mkeka, Frank akiwa
amejilaza huku kichwa chake akikiegamia katika mapaja yangu. Mama yake alikaa
pembeni akisuka ukili, wakati wadogo zake wawili wa Frank, Furaha na Fiona
walikuwa wakicheza karata.Ilikuwa ni usiku mara baada ya kupata chakula cha jioni kwa vile nyumba ya kina
Frank haikuwa na umeme tulikuwa tukikaa nje kwenye mbalamwezi tukingojea
muda wa kulala.
Nilikuwa nikichezea nywele za Frank wakati simu yangu ilipoita, nilipotazama
alikuwa ni baba.
“Pokea simu.” Frank aliniambia.
“Ni baba huyo.”
“Pokea.”
Kila mtu alitega sikio kusikia, nilipokea.
“Haloo baba shikamoo .”
“Sociolah utani na wewe sasa umekwisha muda wa kurudi nyumbani umefika
nimekufungia ndani kwa muda mrefu ili ujirekebishe lakini umeonekana bado
hujajirekebisha umeshakaa sana na huyo mtu wako sasa ni muda wa kurudi
nyumbani usitegemee kwamba mimi ningekuwa mjinga kiasi hicho kuamini
kwamba uko mikumi, uko sijui udzungwa unatalii, ninafahamu fika kwamba uko
Ifakara naomba kesho ifikapo saa kumi na mbili jioni ufike hapa nyumbani sihitaji
maelezo.”
“Baba….” Simu ilishakatwa.
Mchanganyiko nilioupata kwenye akili yangu sikuwahi kuupata siku zote za
maisha yangu yaliyopita, nilishindwa cha kuongea machozi yalinitiririka bila
kukoma.
“Vipi?” Mama Frank aliniuliza, nilishindwa cha kuongea.
Frank alininyanyua na kunipeleka chubani, uso wangu wote ulikuwa umejawa na
furaha sasa hivi ulitawaliwa na huzuni. Machozi yalienea kila kona, uso wangu
ulipambwa na michirizi ya machozi kana kwamba ni eneo ambalo mto unaanzia.
“Baba anataka nirudi kesho.”
“Aaah Sociolah tumekaa hapa kwa muda wa wiki moja na nusu, you go back home
soon I will be back, likizo yenyewe imeshakaribia kuisha wala usijali.”
“Nisijali nini Frank? Siwezi kukaa mbali na wewe.”
“Sociolah lazima uangalie hali ya mazingira jinsi ilivyo ukileta ubishi baba
anaweza kuzuia hata baadae nishindwe kuishi na wewe please naomba urejee
nyumbani.”
Huku nikilia nilikubali kwa shingo upande.Nilianza kupanga vitu vyangu wakati huo Frank alienda kuwapa taarifa familia
yake wote walipatwa na huzuni sana sikuwa na jinsi siku iliyofuata nilirejea Dar es
salaam.
Niliogopa sana kufika nyumbani kwani baba alikuwa tayari alikuwa akifahamu
nilipokuwepo hata hivyo nilijipanga kupambana naye.
Nilipofika nilipokelewa vizuri na familia yangu yote hata baba alionekana
kunifurahia sana.
Pink na Pinto waliniambia kuwa walinimisi sana na walikuwa na wakati wa huzuni
sana kuwa mbali na mimi.
Amani ilirejea ndani ya yumba yetu sikuwa nikifungwa tena wala kubanwa
mwisho wa siku likizo iliisha na nilirejea chuoni.
Siku ya kwanza mama alinipeleka chuoni mwenyewe kwa gari. Sikutaka kuuliza ni
lini nitaenda bwenini kwetu niliamua kunyamaza kimya nione nini kinafuata.
Wakati tuko njiani tunarudi mama aliniambia.
“Sociolah lini unarudi bwenini kwenu?”
“Aanh nilikuwa napanga kwenda kesho mama.” Nilimuambia.
“Basi hakuna shida una kipindi saa ngapi?”
“Nina kipindi saa tatu.”
“Basi asubuhi utaenda Mabibo halafu utatokea kule kuja chuoni.”
“Sawa mama.” Niliongea kwa furaha sana.
Hata hivyo nilivyokumbuka hali yangu na Melania furaha yangu ilitoweka ghafla.
Siku ya kwanza Frank hakuwepo.
Ilipofika siku ya pili mama alinipeleka bwenini kwetu.
“Mimi nina safari ya kwenda mjini Kariakoo kwahiyo sidhani kama nitakupeleka
chuoni, wewe nenda mwenyewe nadhani unaweza kila kitu na hakuna shida yoyote
ukihitaji pesa niambie hakuna shida.”
Mama aliniambia, aliondoka na kuniacha.
Nilitoka moja kwa moja hadi chumbani kwa Frank niliwakuta wote wakiwa
wamesimama wanaongea huku wakicheka kwa sauti. Nilipoingia Frank alijongea
karibu yangu na kunikumbatia na kisha akanibusu kidogo mdomo nilihisi aibu
mbele ya marafiki zake.
“Karibu mke wangu, karibu malkia.”
“Ahsante.” Nilisema na kwenda kukaa kitandani.
“Sociolah kuna kadi ya mualiko hapa imetufikia tunataka kwenda kwenye sherehe
mwisho wa wiki, utakuwa pamoja nasi?”“Sherehe ya nini?”
“Huyu hapa rafiki yetu Innocent amepewa kadi ya mualiko kuhudhuria tukio fulani
hivi. Baba yake mdogo anamiliki kampuni, kampuni yao inatimiza miaka mitano
kwahiyo wanafanya anniversary.”
“Frank utaenda?”
“Ndiyo nitakuwepo.”
“Na mimi nitaenda.”
“Nitafurahi sana kuwa na wewe sociolah.”
“Woow tutaenda na malkia.”
Watu wote waliokuwepo kwenye kile chumba walifurahia sana kwamba
ningeungana pamoja nao.
Innocent naye alifurahi sana.
“Mimi ndiyo maana nakukubali sana sociolah yani ni msichana ambaye uko
kipekee sana.”
“Wala hata usijali.”
Nilimpigia mama simu na kumpa taarifa ya kuhudhuria kwenye sherehe hizo na
yeye bila hiyana aliniruhusu na aliniambia kwamba angemuambia baba.
Siku ya ijumaa niliondoka na Frank hadi Mlimani City kwa ajili ya kuchagua nguo
za kuendea kwenye sherehe hiyo.”
Nilichagua gauni jeupe zuri na yeye nilimchagulia shati jeupe ambalo kwa pamoja
tulionekana kufanana tulipojaribu nguo zetu tulionekna kufanana sana.
Hatimaye siku ya sherehe ilifika nilijiandaa mapema na mpaka kufikia saa kumi na
moja nilikuwa tayari. Nilijipulizia manukato yanayonukia sana.
Nilitoka moja kwa moja na kuelekea chumbani kwa kina Frank niliwakuta wote
wakiwa tayari wakinisubiri mimi.
“Madam tulijua utachelewa bwana.”
“I am always punctual.” Niliwaambia.
“I can see, kweli Frank amepata mwanamke.” Niliachia kicheko kidogo na baada
ya kuwasalimia nilielekea aliko Frank, nilimkumbatia na kisha tukaongea mawili
matatu.
“Tuondokeni.” Innocent aliongea.
“Gari linatusubiri.”
Tulipanda kwenye gari na kisha safari ya kuelekea Serena hotel ilianza.
Njiani kulikuwa na kelele nyingi hata hivyo nilitulia nikiongea na Frank wangu
kwa sauti ya chini sana wala sikushughulishwa na kelele zao.Kwa takribani lisaa limoja tuliweza kufika Serena hotel.
Tuliingia moja kwa moja ukumbini na tayari shughuli ilikuwa imeshaanza.
Vinywaji vilikuwa vya kila aina.
Frank hakuzoea kutumia vinywaji vikali hivyo na mimi sikupenda kutumia
kinywaji kikali siku hiyo niliamua kutumia vinywaji laini kama ilivyokuwa kwa
Frank.
Tulikaa kwenye meza yetu iliyokuwa na wtu takribani sita huku tukiongea
maswala mbalimbali.
Ratiba ziliendelea kufuatwa.
Tulipata chakula kizuri na wakati shughuli ikielekea mwishoni kabisa walifungua
muziki kwa ajili ya kucheza.
“Twende tukacheze.” Frank aliniambia.
“Unaweza…?” Nilimuuliza.
“Sasa kama ningekuwa siwezi ningekuita tukacheze, leo utajua kwamba nina kipaji
cha kucheza.”
“Hahaha..” Nilicheka.
“Ok twende ukanioneshe.”
Tulinyanyuka na kisha kuelekea katikati ambapo watu wengi walikuwa wakicheza.
Tulianza kucheza waliweka mzika laini ambapo ulipendeza sana kucheza
wapendanao.
Alinishika kiuno, akauchukua mkono wangu na kuugusanisha na wake na kisha
tukaanza kucheza kama mara nyingi wafanyavyo wazungu, nilikuwa nikipenda
sana kucheza hivyo na nilifurahia sana.
Tuliendelea kucheza huku nikizidi kuvutiwa na miziki hiyo, nilijikuta nikipoteza
uwiano nilikuwa nikimtazama Frank moja kwa moja machoni kwake. Hisia
zilinizidia nikajikuta nazidi kumsogelea usoni kwake hadi pua zetu zilipogusana.
Nilifumba macho kana kwamba ninayesinzia huku nikiwa tayari kwa kitu ambacho
kilikuwa kikitokea katika sekunde moja iliyobakia.
Ghafla niliguswa begani nilifumbua macho haraka sana macho yangu yaligongana
na Frank ambaye alikuwa ameshikwa na mshituko, niligeuka haraka na
kumuangalia mtu ambaye amenishika nikiwa na hasira zote kwa kunikatishia
starehe yangu
La haula!!Nilikutana moja kwa moja na baba, sikutaka kuamini macho yangu nilishindwa
cha kuongea midomo ilibaki ikitetemeka tu huku nikihisi haja ndogo ingenitoka
muda wowote ule.
INAENDELEA..............

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search