Thursday, 31 May 2018

NATAKA KUZAA -SEHEMU YA ISHIRINI

MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
La haula...!!
Mlango ulifunguka saa hizi.
“Mlango haujafungwa ngoja nijifanye napeleka vyombo.”
Nilibeba vyombo vyangu na kuvipeleka jikoni, wakati narudi nilijaribu
kuchungulia sebuleni ni akina nani wapo na kama kuna uwezekeano wa kusikia
wanachokiongea.
Nilimkuta mama akiwa amekaa peke yake alionekana kuwa na mawazo mengi
sana, hali hiyo iliniumiza nilinyata taratibu na kisha kwenda kukaa pale alipokuwa
amekaa mama.
Nilimgusa begani aligeuka uso wake ulionesha simanzi sana aliniangalia tu na
kisha kuendelea kutazama pale alipokuwa ametazama.
“Mama...”
Aligeuka na kuniangalia machozi yalionekana kumlenga.
“Kuna tatizo gani mama mbona nimechukuliwa chuoni kwa namna kama ile na
nimeletwa huku nimefungiwa ndani kuna nini ambacho sipaswi kukijua, kuna
tatizo gani mama niambie basi.”
Mama alivuta upande wa kanga ambao alikuwa amejifunga na kufuta machozi
yaliyokuwa yameanza kuchuruzika baada ya hapo alinitazama alinyanyua mkono
wake hadi shavuni kwangu.
“Mwanangu Sociolah.”
“Bee mama.”
Alitabasamu tabasamu lililoonesha machungu aliyokuwa nayo moyoni.
“Nakupenda sana mwanangu.” Mama aliniambia.
“Nakupenda pia mama, je hilo ni tatizo, kuna kitu unanificha mama naomba
uniambie.”“Sociolah niambie ni mwanaume gani mwenye mahusiano na wewe pale chuoni.”
Swali lake lilinishitusha sana sikutegemea kuulizwa swali kama hilo kwa wakati
kama huo.
“Mama ni nini hicho unaniuliza.”
“Hakuna cha kuficha Sociolah niambie ni nani?”
Nilipandwa na ghadhabu sana niliona kama familia nayo imeanza kuniingilia
katika mahusiano yangu na Frank.
“Mama mimi nimeshakuwa mtu mzima.” Nilianza kuongea kwa ghadhabu na
mimi.
“Hayo maswala mimi siwezi kukuambia na kama mmekaa na baba mnakuwa na
huzuni kwasababu ya hilo swala sijui, mimi nimeshakuwa mtu mzima naomba
mniache, mniache...”
Niliongea.
“Pumbavu....” Mama alinyanyuka kwa ghadhabu nilishangaa, alisimama mbele
yangu.
“Ninaongea na wewe kama binti yangu nikupendae unanijibu kama unaongea na
marafiki zako huku chuoni, sikia Sociolah lazima uwe na adabu mbele yangu.”
“Mama kwani nini nimekosa.” Nilimuingilia.
“Kosa langu mimi ni nini mnanichukua chuoni kama mnamchukua mhalifu nakuja
huku mnanifanyia mambo ya ajabu ajabu kwasababu gani? Eti kwasababu ya kuwa
na mahusiano na mtu kwani ni vibaya kuna shida gani hata kama ninaye.”
“Kelele...” Mama alinikatisha.
“Kuanzia leo hutotoka humu ndani, kwenda chuoni utaenda na mimi na
nitakurudisha mwenyewe na nitakuwekea mtu wa kukuangalizia mpaka pale
utakapo jirekebisha, hiyo ni amri kutoka kwa baba yako na amesema akisikia
ujinga ujinga wowote utamkosa huyo mwenzio pumbavu.” Mama aliongea na
kisha kuondoka.
Nilibaki nimechanganyikiwa nisijue hata cha kufanya. Niliendelea kukaa pale
sebuleni kana kwamba sina sehemu ya kwenda.
“Mungu wangu, Mungu wangu balaa gani tena hili mbona matatizo juu ya
matatizo.” Niliendelea kujiuliza.
“Mbona Mungu umeniacha mimi, huku Melania huku nako familia inanifanyia
hivi mimi nitaishije jamani.”
Niliendelea kuwaza, niliuma vidole mpaka nikahisi vitakatika. Nilinyanyuka
kiunyonge na kisha kuelekea chumbani.Usiku mzima nilikesha nikilia.
Nilishindwa kujua hatima yangu ni nini?
Niliamua kuacha kama ilivyo usiku ule nilichelewa sana kulala na asubuhi na
mapema ilinikuta niko macho.
Siku nzima nilishinda ndani simu yangu haikuwa na laini baba alitoa laini na kisha
kubaki nayo nilikaa tu nikiitazama simu yangu.
Muda wote nilikuwa ndani.
Afuheni ilikuwa ni kwamba kuanzia siku hiyo iliyofuatia sikuwa nikifungiwa
chumbani bali getini alibadilishwa mlinzi ambaye hata sikuwa nikimfahamu na
alipewa amri ya kutonifungulia geti hivyo nilikuwa nikikaa ndani nikichoka
ningetembea tembea humo bustanini muda wote.
Kwa kuwa baba na mama walikuwa kazini asubuhi hadi jioni wakati Pink na Pinto
walikuwa shuleni nilibaki na dada wa kazi mule ndani ambaye na yeye sikuwa
nimemzoea sana na wala sikutaka kuwa karibu naye.
Muda na siku vilienda nilishindwa kuonana na Frank wala kufanya naye
mawasiliano.
Melania aliendelea kunichukia.
Hali hiyo iliendelea hadi likizo ilipofika.
Ulikuwa ni mwezi wa tatu tarehe tatu. Bado sikuwa na ruhusa ya kutoka nyumbani
hata hivyo nilijitahidi sana kuwa binti mzuri ili niweze kuulainisha moyo wa baba
anisamehe kutoka katika kifungo hicho hakika alipendezwa sana.
Siku yake niliingiwa na ujasiri.
“Baba umenifungia kwa muda mrefu ni lini utaniachia huru.”
Niliongea kwa sauti ya upole.
“Oooh binti yangu nitaongea na mama yako na kisha nitakuja kukuambia nini
tumeamua.”
“Sawa baba nitafurahi kama utanikubalia.”
Nilirudi chumbani huku nikisherekea ushindi huo, najua kama mama angekubali
basi baba asingekuwa na tatizo lolote.
Baada ya nusu saa mama aliingia chumbani kwangu.
Nilikuwa nimekaa kitandani hiku nikisoma soma baadhi ya vitu.
“Sociolah.” Mama aliniita kwa upendo huku akinishika begani.
“Yes mama.” Nilimjibu.
“Unahitaji kutembelea sehemu gani na kiasi gani kwa ajili ya safari yako.”
Furaha iliyonijia nilitamani kuruka ruka ila nilijizuia.“Napenda kutembelea Morogoro na kiasi chochote tu.”
“Kuwa huru binti yangu nimeongea na baba yako vizuri kabisa amesema kipindi
chote ulichokuwepo humu ndani umebadilika naona na akili yako pia imerudi
tumekufungia sana ndani muda mrefu na saa hizi ni wakati wako wa kuwa huru
popote utakapotaka kwenda utaenda sawa mwanangu, usiwe na shaka sema
unahitaji kiasi gani?”
“Mama kwa kweli mimi chochote tu nitafurahi najua nyie ni watu mmetembea
sana, mimi sijawahi kwenda hayo maeneo kwahiyo sijui ni kiasi gani, naweza
nikakuambia kiasi gani halafu ikawa kidogo au nikakutajia kikubwa kuliko
unachoweza kunipa.”
Mama alicheka.
“Taja hicho kikubwa ambacho sisi hatuwezi kukupa tutakupa hichohicho.”
Nilicheka tu.
“Nipe laki saba mama.”
“Hakuna shida.” Nilishangaa sana.
Mama alienda na kurudi na kiasi chote cha fedha.
“Utaondoka lini?” Aaah nitaondoka siku yoyote tu.
“Ila nilipenda sana niende kesho kutwa.”
“Hakuna shida binti yangu kesho nitakukabidhi laini yako.”
“Ahsante mama.”
Mama alitoka chumbani kwangu na kisha kuondoka, nilifurahi sana nilichagua
nguo nzuri ambazo ningeweza kuzivaa katika safari yangu hiyo nilichukua begi
langu dogo na kisha kupanga, niliweka kila kitu changu tayari.
Kesho yake haikukawia, mama alinipa laini, sikutaka kuongea na mtu yoyote
niliweka simu yangu chaji na siku iliyofuata nilifanya safari yangu.
Niliondoka nyumbani saa kumi na mbili na nikapanda gari ya saa moja gari
lilikuwa likielekea Ifakara safari ilikuwa ndefu na ya kuchosha, nilikuwa sijazoea
kusafiri umbali mrefu kwa basi na katika barabara za vumbi nilifika Ifakara nikiwa
nimechoka sana.
Sikujua hata wapi nilekee nilitoa simu yangu na kutafuta jina la Frank la haula
halikuwepo.
Hata hivyo haikunisumbua kwasababu namba yake nilikuwa nayo kichwani
nilibonyeza na kumpigia.
“God, is it you Sociolah?”
“Ni mimi Frank.”“Nina malalamiko na wewe siku zote ulikuwa wapi?”
Alianza kutoa malalamiko yake bila kuchoka.
“Frank stop please.” Alinyamaza.
“Niko hapa Ifakara niko Stand naomba uje unichukue nimechoka.”
“Say what!!” Alionekana kushituka sana.
“Ndiyo Frank fanya haraka.”
“Sociolah acha utani bwana.”
“Kweli kwanini nikutanie, naomba uje unichukue.”
Hazikupita dakika nyingi alikuja.
Alifurahi sana kuniona alinikumbatia kwa nguvu zote.
“Sociolah kwanini umekuja bila kunitaarifu.”
“Hiyo ruhusa yenyewe kuipata ilikuwa shida. Nimekumisi sana Frank wangu
ndiyo maana nimekuja.”
“Sociolah unajua mimi kule naishi na mama.”
“Kwani mama ndiyo atatuzuia tusiwe wote.” Nilongea.
“Hamna hali ya kule.”
“Frank umesahau kwamba ulinihaidi siku utanileta Ifakara au kwasababu nimekuja
mwenyewe ndiyo umechukia hutaki nifike kwenu niambie kama hutaki nirudi Dar
sasa hivi.”
“Hapana lakini isingekuwa vizuri kama nitakupeleka kuishi mazingira kama yale.
“Mimi mwenyewe nimekuja nimeamua kuja wewe twende vingine tutajua huko
huko.” Tulichukua Taxi na kisha kuelekea maeneo ambayo Frank alikuwa akiishi.
Alikuwa akiishi maeneo ya mtaa wa Pogoro.
Maeneo hayo yalikuwa machafu na yenye msongamano wa watu. Kadri
tulivyokuwa tukikaribia kwao nilianza kuona ugumu wa kuishi huko hata hivyo
maji nilisha yavulia nguo sikuwa na budi kuyaoga.
Safari iliishia kwenye nyumba chakavu sana.
Nyumba iliyojengwa kwa matofali ya kuchoma ambayo haikuwa na sakafu ndani
yake. Ilikuwa na vyumba vitatu na sebule ambayo haikuonekana kama sebule.
Ndani ya sebule hiyo kulijazwa ndoo za maji, meza chakavu na baadhi ya vyombo
vichache huku baadhi ya picha zikining’inia ukutani.
Kulikuwa na viti vya mbao ambavyo vingemuumiza makalio ya mtu ambaye
angekalia.
Mazingira kwa ujumla yalikuwa machafu, choo kilikuwa nje, na hakikufaa kabisa
kwa matumizi ya binadamu kilikuwa choo cha shimo na mimi nilikuwa nikiogopasana kutumia vyoo vya shimo uwanja ulikuwa umezungushiwa kwa makuti na
hapo ndipo Frank alikuwa amekulia kwa kuwa ni mahali ambapo Frank alikuwa
akiishi sikuona shida.
Gari lilipaki mbele ya nyumba na kisha Frank alinishusha alinisaidia kubeba kibegi
changu kidogo na kisha kuelekea ndani. Hakukuwa na mtu ndani hapo.
Aliniingiza moja kwa moja hadi chumbani kwake kulikuwa na kitanda chakavu
cha futi nne kwa tano. Meza ndogo ambayo juu yake kulikuwa kuna taa aina ya
kibatari ,kiberiti, peni na baadhi ya vitu vidogovidogo. Ukutani kulikuwa kuna
misumari iliyokuwa imetundikwa nguo ambazo zilionekana kuwa ni za Frank.
Kulikuwa na masufuria makubwa ambayo ndani yake kulionekana kuwa na maji.
Pamoja na ndoo.
Frank alinikaribisha ndani ya chumba hicho sikuona sehemu ya kukaa isipokuwa
kitandani, nilikaa.
“Frank unahofia kufika kwenu.”
Wala hakutabasamu kama alivyozoea alikuja kukaa pembeni yangu.
“Sociolah unaweza kuishi katika mazingira kama haya.”
Nilivua viatu na kujilaza kitandani huku nikitabasamu wala hata sikumjibu.
“Nimechoka Frank nahitaji kwanza kwenda kuoga.” Alitoa macho.
“Nini nipeleke nikaoge bwana.” Nilimuambia.
“Hamna shida.”
Nilifungua begi langu na kutoa kanga mbili nikajifunga na kisha kuelekea bafuni.
Bafu ambalo lilikuwa limetengenezwa kwa makuti, ni choo kilichokuwa
kimetengenezwa kwa matofali ambacho juu kilikuwa akijaezekwa na bafu hilo
lilikuwa limewekwa matofali chini na lilioneka kuwa limechakaa sana na halikuwa
zuri kiafya.
Nilioga kana kwamba sioni nilirudi chumbani nikamkuta Frank akiwa amesimama
nahisi akiwaza cha kufanya.
“Nini unawaza?” Nilienda huku nikijaribu kumkumbatia kwa nyuma.
“Hakuna shida.”
“Mama atarudi muda wowote ule na pia wadogo zangu wapo shule.”
“Natamani sana kuwaona mpigie mama simu muambie awahi kurudi kwani yuko
wapi?”
“Aanh yuko kwenye majukumu yake.”
“Hakuna shida akirudi atakula nini?”
Alinyamaza kimya.“Sitaki kuamini kwamba unasubiri mama aje ndiyo apike acha tabia mbaya twende
jikoni.”
Tulitoka hadi nje kulikuwa na kibanda kilichokuwa kimeezekwa kwa majani na
palikuwa na mafiga yaliyokuwa meusi na pembeni yake kulikuwa na mfuko
mdogo uliokuwa na mkaa mchache ambao haukutosha kupika.
“Frank kuna nini cha kupika.”
Frank alibaki akiniangalia.
“Unaniangalia kana kwamba hunijui mimi ndiyo Sociolah.” Nilimuambia huku
nikicheka. Nilifungua wallet yangu na kisha kutoa noti mbili za elfu kumi.
“Kanunue mchele wa kutosha, kanunue na nyama na maharage na mboga yoyote
ya majani na mafuta na vitu vingine ambavyo havipo, mimi leo sitoki nimechoka.”
Nilivuta mkeka na kisha kukaa chini.
Frank aliondoka na baada ya dakika chache alirudi na vitu nilivyomuagiza nilianza
kupika kwenye jiko la kuni.
Ilikuwa ngumu sana kwasababu hata kupika kwenyewe nilikuwa sijui vizuri lakini
nilijitahidi kwa nguvu zote ili mama atakapokuja afurahie chakula changu.
“Frank tunakula au tunamsubiri mama?” Nilimuuliza mara baada ya kukamilisha
mapishi yangu.
“Mimi nina njaa Sociolah.” Aliongea huku akicheka.
“Lakini Frank unaonekana umepoteza kabisa amani yako.”
“Napotezaje wakati nipo na mke wangu pembeni.” Nilicheka sana.
“Hakuna shida.”
Tulikula huku tukiwaachia watu wa pale nyumbani chakula kilichobaki.
Tulikaa na baada ya muda mlango ulifunguliwa.
Wakati huo tulikuwa tumekaa mkekani mlango wa mbele ulifunguliwa.
“Frank.....” Sauti ya mwanamke iliita.
“Frank mama amekuja.”
Frank alinyanyuka na kisha kwenda.
Nilinyanyuka na kumfuatia kwa nyuma mama alikuwa amebeba mzigo mzito
kichwani, mizigo ambayo ilikuwa ndani ya ndoo nilishindwa kujua ni nini
alimpokea na kumtua mzigo ule.
Mama alionekana kuchoka sana nilimkimbilia na kisha kumshika na kumsaidia
kumkalisha kwenye viti vya mbao ambavyo vilikuwa pale sebuleni.
“Ahsante.” Alijibu kwa pole na kisha kunitazama.
“Karibu.” Aliniambia huku alimuangalia Frank.“Frank huyu ndiyo Sociolah?”
Nilishan gaa kujua mama mtu ananijua.
“Yeah mama ndiyo huyu.”
“Mbona amekuja bila taarifa si angesema anitaarifu nimuandalie chakula jamani.”
“Hakuna shida”
“Acha nikakuandalie chakula.”
Mama alitaka kunyanyuka.
“Usijali mama nimeshaandaa.”
Nilijibu.
Ngoja nikuwekee chakula ule au nikuchemshie maji.”
Alinitazama huku macho yake yakionesha upendo mwingi.
“Usijali mwanagu nitaoga tu maji ya baridi.”
“Maji ya moto ni mazuri mama.”
“Hakuna shida.” alinyanyuka huku akionekana kupata nguvu mpya.
Alioga na kisha kupata chakula huku akinisifia kuwa chakula kile kilikuwa kitamu
sana.
Baadae familia nzima ilirudi ilikuwa ni familia ndogo tu tulijumuika pamoja na
kisha kupata chakula cha usiku. Ilionekana tayari walikuwa wakinifahamu hivyo
haikuwa na haja ya utambulisho ilionekana ni familia ya kimasikini lakini yenye
upendo mwingi.
Tuliongea mambo mengi tulicheka ulikuwa ni wakati mzuri sana katika maisha
yangu yote niliyowahi kupitia nilifurahia sana kuwa pamoja na familia ya Frank.
“Mwanangu....” Mama aliniita siku moja.
“Unampenda Frank?” Aliniuliza.
“Ndiyo mama nampenda sana.”
Kwanini umeuliza?
“Kama unampenda changamoto zitakazokuijia ni nyingi sana, nakushauri
mwanangu usikate tamaa endelea kumpenda kwa moyo wote.”
Aliongea mama Frank huku uso wake ukibadilika kutoka kwenye mtu mwenye
furaha hadi kwenye nyuso ya huzuni.
“Mama.” Nilimuita huku nikisogea karibu yake.
“Nampenda sana Frank na kati ya watu wote nimeamua kumchagua yeye sitojali ni
nini tunapitia, sitamuacha Frank.” Alicheka.
“Usijali mwanangu.”
Alitabasamu kwa huzuni.“Mama itakuaje na Frank naye akiniacha.” Aligeuka.
“Eenhe Frank kanijia hapa kama amechanganyikiwa Sociolah….. Sociolah….
Sociolah, Sociolah ataniacha mimi mpaka analia.” Mama yake aliongea, nilicheka.
“Kweli Frank huwaga analia?”
“Mimi nilikuwa sijawahi kumuona ndiyo kwa mara ya kwanza kumuona analia.”
Nilicheka sana.
Na hivyo ndivyo siku zetu zilivyokuwa na mwisho wa siku baba alinipigia simu...................
INAENDELEA............

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search