Friday, 25 May 2018

NATAKA KUZAA -SEHEMU YA KUMI NA MBILI


MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
NAMBA YA SIMU: 0683777152
Mama aliingia na safari ya kwenda chuoni ilianza, nilikuwa nikiwaza maisha
yataendaje huko.Alinileta hadi kwenye madarasa yetu na mara zote yeye alikuwa akinifungulia
mlango wa gari. Alishuka watu wote macho walielekeza kulipo gari letu nilikuwa
nikiwaangalia tu kupitia dirishani mama alifungua mlango na kisha nikashuka.
“Uwe na siku njema mwanagu.” Aliongea na kisha akanikumabtia na kunibusu
shavuni na kisha akafunga mlango.
“Kuna tatizo lolote?”
“Hapana mama.”
“Unahitaji hela?”
“No.. Ninazo mama.”
“Sawa.” Nilipiga hatua za kivivu kuelekea darasani.
Nilikutana na Melania alikuja akanikumbatia kwa nguvu zote.
“Wewe mtoto umekaa nyumbani wiki moja tu umenenepa hivyo?”
“Nimekumisi sana Melania.”
“Jamani si urudi Hostel.”
“Mama kaniambia nirudi wiki ijayo.”
“Jamani tumekumisi.”
“Vipi mpo wote mmeshafika?”
“Yeah na Fety yupo yani kakumisi kweli na Monica wote.”
“Nitarudi bwana hata usijali sawa.”
Muda wa kipindi ulianza tuliingia darasani, nilijaribu kutupia jicho kila kona
kumtafuta Frank lakini sikumuona.
“Yuko wapi huyu?”
“Melania alihisi kwamba kuna mtu namtafuta na ilionekana darasani kwetu kote ni
Frank tu ndiye ambaye hakuwepo kwa maana darasa letu hallikuwa na watu wengi.
“Unamtafuta Frank?” Melania aliuliza.
“Nilicheka tu.”
“Hapana lakini simuoni.”
“Sijui yuko wapi?”
“Anaumwa.”
Mtu wa tatu aliitikia kutoka pale tulipokuwa tumekaa alikuwa ni Innocent
“Ooh Innocent I miss you, Frank anaumwa ?”
“Yeah anaumwa.”
“Anaumwa nini?”
“Hajisikiisikii anaona uchovuichovu anahisi ana malaria.”
“Ameenda hospital?”“Heeee…. Maswali yote hayo ya nini? Unataka kujua nini kuhusu Frank?”
Melania aliingilia.
“Kwani vibaya kumjulia mtu hali kama anaumwa?”
“Innocent alitabasamu.
‘Vizuri umejibu vizuri sana Sociolah.”
“Eenhe niambie ameenda hospitali?”
“Nimemuacha chumbani sijui kama ameenda hospital.”
“Aanh sawa.” Nilitaka kuongea neno lakini niliogopa uwepo wa Melania niliamua
kunyamaza.
Tulipotoka darasani nilianza kumkwepa Melania. Siku hiyo tulikuwa tukimaliza
vipindi vyetu saa kumi za jioni.
Nilimkwepa Melania dakika mbili tu tulikuwa tumepotezana nilikimbia haraka
Shuttle Point na kupanda gari za Mabibo.
Sikutaka kumuambia Frank kama kwake, nilitaka iwe surprise niliposhuka kwenye
gari pale Mabibo nilimnunulia juisi ya azam kubwa, nikamnunulia matunda aina
ya tufaha (Apple.), nikanunua na chakula, nilinunua Chipsi na kuku nusu na maji
ya kilimanjaro makubwa. Nikafikiria kitu gani ambacho sijanunua, nilikaa
nikawaza nimnunulie nini.
“Si anaumwa ngoja nimnunulie glucose.”
Nilienda kumnunulia glucose kisha nikakumbuka kujinunulia mafuta yangu ya
karafuu kwa ajili ya kujikandia na kutoka kisha kuelekea chumbani kwa Frank.
Nilifika pale niligonga mlango, nilifunguliwa na mtu mwingine ambaye sikuwa
nikimfahamu na ndiyo ilikuwa mara kwanza kuonana.
“Karibu mrembo.” Alinikaribisha kwa bashasha zote.
“Ahsante.”
Kabla sijaingia nilimuuliza.
“Frank yupo?”
“Yeah yupo.”
“Naweza kuingia kuja kumuona?” Niliongea kwa sauti ya chini wala sikutaka
Frank ajue kama niko hapa mlangoni.
“Ingia.”
Alishangaa sana kwa kweli, nahisi nilikuwa mtu wa kwanza kuja kumtafuta Frank
zaidi ya Innocent ambaye ndiye aliyekuwa rafiki yake, yeye peke yake. Mkaka
alibaki ameshangaa tu niliingia hadi kitangani kwa Frank ambapo alikuwa amelala
na kujifunika shuka mwili mzima nilikaa pembeni yake na kisha kumbukumbu yausiku ule ambao tulikuwa pamoja kitandani hapo ilinijia, nilibaki tu nikitabasamu.
Yule kaka alikuwa amesimama mlangoni na wala hakuwa amefunga mlango,
niligeuka na kumtazama nikaachia tabasamu alitabasamu na kisha kuja mpaka
kwenye meza. Alichukua chukua baadhi ya vitu, alikusanya vingine aliviweka
vizuri kisha akaniaga.
“Natoka.”
“Mbona unanikimbia.”
“Hamna nilikuwa najiandaa kutoka.”
“Aaah, sory Frank amekula?” Niliuliza.
“Hapana nilikuwa nataka pia nikamtafutie RB huko nje.”
“RB?” Nilicheka.
“Ok fine, nimemletea chakula usinunue, sawa.”
“Hamna shida.” Alisema na kuondoka.
Hata mimi pia nilitamani aondoke ili atuachie nafasi, aliondoka. Nilienda mlangoni
nikafunga mlango na kisha nikasogea pale kitandani alipo Frank,
“Frank.” Niliita wala hakutikisika, nilimvuta shuka bado hakuamka, nilimbusu
shavuni aliachia tabasamu.
“Sociolah.” Aliita akiwa bado hajafungua macho niliachia tu tabasamu. Alifungua
macho kichovu na kisha akageuka upande wangu.
“Yes darling.” Nilifurahia sana kuitwa hilo jina mwili mzima ulinisisimka.
“Hata hujaniambia kama unaumwa.” Alicheka tu.
“Sikutaka upate shida yoyote, siku ya kwanza kwenda chuo halafu upo nyumbani
isigekuwa vizuri.”
“Jamani nani kakuambia isingekuwa vizuri?”
“Sorry kama nimekosea.”
“Usijali, unajisikiaje?”
“Najisikia vizuri kwasababu umekuja.”
“Hauko serious.”
“Nilijisikia kuumwa sana lakini umekuja nimepata hata afadhali.”
“Hahaha…” Nilicheka.
“Amka ule basi mpenzi wangu.”
Alijitahidi kunyanyuka ingawa alionekana kama akipata maumivu.
“Frank what is wrong.”
“Mwili mzima unauma Sociolah..”
“oooh pole..”“Aaah.. Joto limekuwa kali sana.”
Chumbani kwao hakukuwa na feni.
“Utafanyeje? Uvue basi shati.”
“Eenh… yani mara nasikia baridi kali mara nasikia joto kali itakuwa ni malaria.”
“Nikupeleke hospitali?”
“Mimi naogopa sindano bwana.”
“Utakufa.”
“Eeenh najua nitakufa.”
“Usiseme hivyo bwana ukifa utaniacha mimi na nani?”
“Si na baba yako.”
“Hahaha…” Nilicheka.
“Ngoja nifungue mlango kidogo.”
Nilifungua mlango na kuacha nafasi kidogo ili hewa iingie mule ndani. Alivua
shati na kisha kubakia kifua wazi, alijitahidi kukaa pale kitandani na kisha
nilifungua chakula nilichokuwa nimemletea na kuanza kumlisha taratibu.
“Wewe Sociolah chakula kitamu.”
“Kula sasa upate nguvu mgonjwa sawa.”
“Nakula mama.”
Hakika alikuwa anakula kana kwamba ndiyo anakula siku ya kwanza.
“Frank kula taratibu basi.”
“Yani nahisi kama kitapotea vile.”
Nilicheka.
“Hebu kula bwana.”
Pamoja na ugonjwa wake alijitahidi sana kuchangamka, alikula kadri alivyoweza
na mara tu aliniambia kwamba nimetosheka.
“Frank.” Nilimuita.
“Unajisikiaje sasa?”
“Sasa najisikia afadhali ila mwili unauma uma.”
“Ok lala nikumassage.”
“Eeenh.. Unifanyeje?”
Nilicheka.
“Nikukande.”
“Sasa hapa hakuna heater ya kuchemshia maji au unataka unikande na maji ya
baridi.”
“No…. Nakukanda kwa mafuta.”“Mafuta gani? Mimi natumia baby care.”
“Ninayo ya kwangu usijali.”
Niliongea huku nikicheka.
“Ok, nilaleje sasa?”
“Lala kifudifudi.”
Alilala kifudifudi na kisha kugeukia ukutani.
Nilinyanyuka na kisha nikapandisha gauni langu juu na kisha kumkalia kiunoni.
“Unaumia.”
“Hapana.” Alijibu kwa sauti iliyofifia.
Nilifungua mafuta na kisha kujimwagia kwenye mikono na kuanza kumpaka yale
mafuta huku nikimsugua taratibu aliishia tu kuguna.
“Ukijisikia kuumia uniambie.”
“Aaah naumiaje na mikono yako ilivyo milaini hivyo.”
Nilicheka, niliendelea kummassage.
“Frank siku nyingine ukiwa unaumwa uniambie, sawa.”
“Nitakuambia usijali.”
“Sawa.”
“Umekunywa dawa yoyote.”
“Nimekunywa tu panado.”
“Lakini Frank kwanini umekataa kwenda hospital.”
“Nilisha kuambia naogopa sindano.”
Nilicheka tu.
“Sawa lakini I hope mpaka kesho utakuwa unajisikia vizuri unaweza ukaja chuoni,
mimi nimetoroka tu hapa mama atakuja kunichukua saa kumi.”
“Sociolah kwanini umetoroka?”
“Don’t ask me why.”
Alicheka kidogo tu na kisha akanyamaza kimya.
Niliendelea na kazi ya kumkanda nikimpapasa maeneo mbali mbali ya mwili wake
kwa ajili ya kuondoa uchovu.
Ghafla mlango ulifunguliwa kwa pupa na mtu ambaye alifungua mlango aliingia,
nilihisi tu ni yule mkaka ambaye nilimkuta hapo chumbani maana mambo yake
yalionekana kufanyika rafu rafu sana, hakupiga hodi wala nini aliingia tu.
“Hey what is wrong?” Niliongea huku nikijaribu kushusha gauni langu.
La haulaaa…!!!!!!!!Kinyume na matarajio yangu yule mtu hakuwa yule mkaka niliyemkuta pale
chumbani alikuwa ni Innocent..............
INAENDELEA.................

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search