Friday, 25 May 2018

NATAKA KUZAA -SEHEMU YA KUMI NA MOJA


MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
NAMBA YA SIMU: 0683777152
Pink alicheka kicheko cha kimbea na kisha kugonga mikono yake.
“Halooo…aya.. Sawa.”
Alitoka nje huku akicheka, nilisikitika tu.
Baba yetu mdogo aliyekuwa akiishi maeneo ya Kimara na baba yetu mkubwa
ambaye alikuwa akiishi Oysterbay.
Wote walikuwa ni watu waliokuwa na nafasi nzito serikalini, walikuwa wakijiweza
na mipango yao ilikuwa kwamba kila kwenye sherehe basi wanakwenda
kutembelea familia moja wapo.
Nilifika sebuleni na wala sikuwa hata nimejiandaa vizuri.
“Sociolah” Baba aliniita.
“Unaumwa?”
“Hamna baba sijisikii tu vizuri.”
“Basi pole, ungeenda kukaa nje upate hewa safi.”
“Usijali baba nitakuwa salama.”
“Kajiandae basi ujumuike na wageni.”
Niliondoka na kuelekea chumbani kwangu, nilioga na kisha kubadilisha nguo,
nilivaa nguo nzuri ambayo baba alininunulia kwa ajili ya sikukuu hizo.
Nikatoka nikaenda kujumuika nao sebuleni.
Wote kati yao niliwatambua isipokuwa mtu mmoja tu ambaye sikumtambua.
Katika siku kama hiyo huwa wanafanya kama sherehe fulani hivi fupi.
Walianza na utambulisho.
Baba alitutambulisha familia yake yote, baba mdogo alitambulisha familia yake
yote na kisha baba mkubwa alitambulisha familia yake.
Ni mtu ambaye sikumtambua alikuwa ni mvulana wa makamo alionekana kuwa na
maisha mazuri hakutambulishwa, nilibaki nimeshangaa.
“Sasa kama hajatambulishwa amekuja hapa kama nani?”
Baada ya kumaliza utambulisho baba alisimama.
“Mbona kuna mgeni mwingine hafahamiki hapa?”
“Huyu bwana ni mwenzangu tunataka kuanzisha naye biashara mpya ni kijana
mwenye mafanikio sana na alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu na sasa amerejeahivyo nimependa naye ajumuike pamoja nasi kwa maana muda si muda mtasikia
tunafanya mambo makubwa sana ni kijana mwenye hari ya mafanikio na mchapa
kazi, mimi binafsi namkubali sana.”
“Karibu sana kijana wangu.”
“Ahsante, naitwa Kelvin.”
Walipeana mikono na mama na watu wengine waliopenda kumpa mikono.
Baada ya salamu fupi ulifika muda wa maakuli, tulisogea mezani na kisha kuanza
kupata chakula, siku hiyo alipikwa mbuzi mzima.
Kulikuwa na vyakula vya aina mbali mbali hata sikufurahia kuvila.
“Sociolah, unaumwa mwanangu.”
“Hapana mama.”
“Hebu kakae nje upate upepo kidogo.”
“Pink alikuwa akiniangalia tu kwa macho yake makavu.”
“Huyu mtoto ana laana kweli.” Nilisema kimoyomoyo, nilinyanyuka bila hata
kugeuka na kuondoka zangu kuelekea nje.
Nilienda kukaa bustanini nikiwa nimeshikilia simu yangu, nilimtumia meseji Frank
lakini hakujibu.
Nilibaki nikiwa na lindi la mawazo yaliyochanganyika na huzuni na ghafla
niliguswa begani.
“Mama nahitaji kuwa peke yangu naomba uniache” Niliongea.
“Sociolah..”
Ilikuwa ni sauti ya kiume ambayo sikupata kuisikia kabla, niligeuka haraka na
kumuangalia, alikuwa ni Kelvin.
“Kelvin karibu.” Niliachia tabasamu la kulazimisha.
“Tayari nishakaribia.”
Alivuta kiti na kukaa mbele yangu, alikuwa akinitazama usoni, niliinamisha uso
wangu ambao ulikuwa umejawa na huzuni.
“Pole.”
“Pole ya nini?” Nilimuuliza.
“Pole ya mambo ambayo yanakukwaza.”
“Aanh.. Usijali nipo kawaida.”
“Nakuona haupo kawaida Sociolah, anyway. Mimi nafanya biashara na baba yako
na muda siyo mrefu tunataka kuanzisha kitu hapa nchini. Nimetokea Marekani
nilikiuwa nakaa kule na familia yangu yote ipo kule na ndiyo maana sikukuu ya
mwaka mpya sikuwa hata na sehemu kwenda nilikuwa sina kampani ndiyonimefika tu nchini, kwa kulitambua hilo baba yako aliamua tuungane kwa
pamoja.”
Sikuelewa mantiki ya vyote hivyo alivyokuwa akiniongelesha nilitabasamu tu
kumuonesha kwamba tuko pamoja ingawa sikuwa nikivutiwa na kile alichokuwa
akiongea.
“Sawa nashukuru.”
“Una ndoto gani Sociolah?”
Nilicheka.
“Unafahamu hata nini ninasomea?”
“Najua… Najua unasomea udaktari.”
“Sasa kuniuliza nina ndoto gani unamaanisha nini? Si unafahamu kabisa
ninasomea udaktari.”
“Hahaha…”
Alicheka kana kwamba ananicheka.
“Mbona mimi nina taaluma ya udaktari tena ni daktari mzuri tu wa upasuaji lakini
ninafanya biashara.”
“Aanh.”
“Sociolah mbali na kuwa daktari unataka nini?”
“Nataka kuzaa.”
Alishituka halafu akacheka.
“Unataka kuzaa?”
“Ndiyo.”
Alicheka kama anacheka kwa dharau na kisha akatikisa kichwa chake.
“Nilizani naweza kukusaidia kutimiza ndoto zako, sijui kama naweza.”
Niliachia kicheko cha nguvu.
“Ahsante nashukuru.”
Nafikiri yupo mtu ambaye atakuwezesha uzae Sociolah.”
“Yes..”
“Baba anamjua?”
Nilipojibu swali la mwisho nilijibu kwa bashasha zote lakini lile tabasamu
liligandia kati na kisha kutoweka kabisa, nilishindwa cha kumjibu, alitabasamu.
“Anyway not a problem, mimi siwezi kwenda kumuambia.”
“Hata kama nazani hawezi kupaniki sana kwasababu umri umeenda pia.”
“Sociolah wewe bado ni mdogo sana.”
“Udogo wangu nini mimi?”Alicheka.
“Anyway keep it up. Unampenda sana rafiki yako wa kiume.”
“Siyo rafiki yangu wa kiume ni mpenzi wangu.”
“Aanh sorry na ahsante kwa kunirekebisha, vizuri, mpende sana na hakika yeye
atakufanya utimize ndoto yako ya kuzaa.”
“Ooh well Thank you. Aanh…. What about your….”
“Mimi ndoto yangu ni…”
“Sijaongelea kuhusu ndoto.”
Nilimkatisha, alicheka.
“Ok uanongelea kuhusu swala la familia si ndiyo?”
“Ndiyo.”
“Aanh kwa sasa hivi…. Hahaha….”
Alicheka na kisha kuishia kati.
“Unataka kunidanganya?”
Nilianza kumzoea.
“Hapana, ni kwamba baba yangu na mama yangu wote ni watanzania na baba
yangu ni daktari. Muda mrefu sana baba yangu alikuwa akifanya kazi Tanzania.
Niliondoka Tanzania nikiwa mdogo sana yapata nikiwa kama nina miaka mitano,
nilielekea Marekani, nimeishi kule miaka yote na mara chache nilikuwa nakuja
likizo kutembelea ndugu jamaa na marafiki. Nilikutana na baba yako pia muda
mrefu kidogo uliopita wakati huo ndiyo naanza masomo yangu ya udaktari. Lakini
kwa vile tulikuwa na ndoto za kufanana tulikuwa tunawasiliana muda mwingi na
hatimaye tukaweza kupanga kitu ambacho tunataka kukifanya na mpaka sasa
nimeweza kumaliza masomo yangu. Nimeajiriwa na maisha yangu najitegemea
nimeamua kuja Tanzani ili nifanye kitu ambacho nilikuwa nataka kufanya na baba
yako, lakini kitu kikubwa sana nampenda mama yangu.”
“Huyu mbona anaanza kujibu maswali ambayo mimi sijamuuliza.” Niliongea
mwenyewe na nafsi yangu, ila niliendelea tu kumsikiliza mwisho wake ulikuwa ni
nini.
“Mama yangu ni mwanamke ambaye wa utofauti sana kati ya wote amabao
nimewahi kuishi nao uko marekani hivyo nataka kuoa mwanamke wa kitanzania.
“Hahaha…” Nilicheka wala sikuwa najua kama huo ndiyo ulikuwa mwisho wa
hadithi yake.
“Ooh nice, Nakutakia kila lakheri.” Niliongea.
“Kelvin…” Baba aliita.“Naona ushapata rafiki.”
“Yeah Sociolah is so Charming, nimefurahi sana kumfahamu.”
“Naona hata homa imepoa.”
“Hamna baba, nimefurahi pia kumjua Kelvin.”
Baba alikaa pembeni yetu tulizungumza mawili matatu.
“Unajisikiaje saa hizi mwanangu.”
“Basi twendeni ndani tukaendelee na mazungumzo yetu.”
Tulinyanyuka wote kwa pamoja na kuelekea ndani
“Naona Sociolah amepata rafiki maana anakuwa mpweke sana.”
“Mpweke tena! Inamaanisha baba amemleta Kelvin ili awe rafiki yangu fine
lakini.”
Muda ulizidi kwenda na hatimaye tulifungua chuo, tulifungua ilikuwa ni siku ya
jumatatu yapata kama tarehe tano hivi mwaka 2016.
Ilikuwa ni furaha kurejea chuoni kwangu mimi ingawa mama hakutaka kabisa.
“Sociolah mwanangu vutavuta kidogo. kwani kuna nini mimi nitakuwa nakupeleka
chuoni.”
“Mama nimewamisi hata marafiki zangu, na pia nataka tukaanze kusoma mama.”
“Sociolah kwani mimi nikikutoa hapa nyumbani kukupeleka chuoni na
kukurudisha utakuwa husomi?”
“Mama nitakosa majadili na wenzangu.”
“Utajadili na nitakuwa nikikusubiri mwanangu.”
“Aanh…” Nilishindwa cha kujitetea.
“Kaa tu hata wiki moja tu halafu wiki ijayo unarudi sawa.”
“Sawa mama.” Niliitikia kwa shingo upande.
Nilitoka na kwenda chumbani kwangu.
Siku iliyofuata asubuhi kabisa mama alikuja kuniamsha.
“Jiandae twende chuo.”
Niliamka kiuvivu uvivu nikaoga nikavaa vizuri nikabeba begi langu la madaftari.
Nikapanda kwenye gari. Mara zote mama yangu alipenda nikae kwenye siti za
nyuma kwa maana yeye alikuwa anasema kwamba wewe mwanangu ni mtoto wa
mfalme na malkia hivyo hupaswi kukaa mbele. Siti ya nyuma ni sehemu ambayo
wanatakiwa wakae watoto wa kifalme. Na mimi nilifurahia sana, nilifungua
mlango wa nyuma na kisha kuketi.
Mama aliingia na safari ya kwenda chuoni ilianza, nilikuwa nikiwaza maisha
yataendaje huko..................
INAENDELEA.....................

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search