Thursday, 31 May 2018

NATAKA KUZAA -SEHEMU YA KUMI NA NANE

MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
Kila mtu mule mgahawani alishangaa hakuna aliyejua sababu yake na mimi
niliamua kumpotezea na kuendelea kuongea na Frank kana kwamba sikumuona.
Tuliendelea na vipindi hadi vilipoisha.
Nilimuacha Melania awahi kuondoka nilimsubiri Frank huku nikimchelewesha ili
tusiwahi kuondoka.
“Kwanini hutaki kuondoka?”
“Mimi sitaki kuongozana na Melania na wala sitaki kwenda kule chumbani kwetu
si unajua tuna ugomvi.”
“Basi twende ukakae chumbani kwetu.” Aliongea.
“Ni wazo nzuri.”
Tuliondoka hadi mabibo na kisha tukaingia Complex kwa ajili ya kupata chakula
cha mchana. Tulikula chakula cha mchana na kisha kuelekea chumbani kwa Frank.
Marafiki zake walikuwepo.
“Aaah jamaa umependeza kweli yani leo kila mtu darasani anakuzungumzia wewe
wasichana sio kujigonga huko aisee jamaa una nyota kweli.”
Aliongea mmoja wapo kati ya watu ambao ni wakazi wa chumba cha Frank kabla
ya kuniona nikiingia.
“Niliachia tu kicheko.”
“Shukrani zote zimuendee mama hapa.” Aliongea Frank huku akinioneshea mimi
niliinama kwa aibu.
“Aaah...Aisee... Huyu ni bonge la mke Frank usiache.”“Naanzaje asa kwa mfano?” Aliongea.
Niliachia tu kicheko huku nikitazama chini.
Nilikaa chumbani kwa Frank hadi wakati wa usiku ulipofika.
“Nataka kupumzika nimechoka.” Nilimuambia Frank.
“Hakuna shida ngoja nikupeleke.”
Alinisindikiza hadi nje ya chumba chetu, alinibusu na kisha kunitakia usiku
mwema.
Akaondoka.
Nilimuangalia hadi alipopotelezea huku nikitabasamu mwenyewe.
“Hakika hapa nimefika nampenda sana Frank.” Niliongea.
Niligeuka na kushika kitasa cha mlango ili nifungue kwa ajili ya kuingia ndani
nilipominya kitasa cha mlango ulifunguka na kisha nikasikia kilichokuwa
kikiongeleka mule ndani.
“Yeye si anajifanya mjanja nitamkomesha.”
Nilivutiwa kujua ni nani tena ameingia kwenye ugomvi na Melania.
“Hamna usimfanyie kitu kibaya.” Fetty alisema.
“Nyamaza.. Mimi ndiyo Melania sishindani na vitoto vidogo.”
Nilifunga mlango nikijiuliza maswali yasiyo na majibu.
“Melania amegombana na nani tena, kumbe ana tabia za ugomvi hivi? Kama ni
hivi sitaweza kupambana naye namuacha kama alivyo akiamua kunisikiliza
nikiomba yaishe sawa asipoamua sitajali.”
Nilifungua mlango na kuingia sikujua wanaongea nini lakini wote watatu Melania,
Fetty na Monica walikuwa wameinamia simu ya Fetty kuangalia walichooneshwa
na Fetty.
Nilipoingia kila mtu alikurupuka kwa haraka na kuanza kufanya vitu ambavyo
havikuleta maana, nilibaki nimeduwaa.
Hali niliyoikuta mule chumbani ilinitisha sana, nilishindwa kuelewa na kubaki
nimesimama tu katikati ya chumba nikiwa kama mtu nisiye sina muelekeo.
Monica alitoka pale walipokuwa wameinama wakiangalia kitu na kukimbia moja
kwa moja kwenye kitanda changu alichukua shuka langu na kisha kujifunika mwili
mzima.
Melania alinyanyuka pale alipokuwa amesimama na kisha kuelekea kwenye
makabati na badala ya kufungua kabati lake alifungua kabati la Fetty na kisha
alijiweka bize kana kwamba kuna kitu anakitafuta kwenye kabati la Fetty.Fetty aliiziba simu yake kwa nyuma, aliiweka nyuma yake ili nisione ni nini
kilichokuwa kinatokea, nilibaki nimeshangaa. Kila mtu alijiweka bize kama vile
hawakutaka nijue ni nini kilichokuwa kikiendelea mule chumbani.
“Unatafuta nini kwenye kabati langu?” Fetty alimuambia Melania.
“Aaah... Eeee....Mmmh ...”
Melania aliishia kuguna tu na kisha alifunga kabati la Fetty na kufunga kabati lake.
Hali hiyo ndiyo ilizidi kunichanganya zaidi, nilifungua mlango na kuubamiza kwa
nguvu na kisha kuondoka sikutaka kuendelea kuwepo mahali pale.
Niliondoka moja kwa moja hadi chumbani kwa Frank, nilifungua mlango bila
kubisha hodi.
Frank alikuwa yupo kifua wazi huku chini akiwa amevaa kaptula ya michezo.
Niliingia na kwenda moja kwa moja kitandani kwa Frank nilikaa na kujiinamia
huku nimefumbata uso wangu katika viganja vya mikono yangu.
“Nini Sociolah kuna nini?” Frank aliniuliza sikutaka hata kumjibu.
“Niambie mama kuna nini?” Alikuja kukaa pembeni yangu.
“Hapana Frank naomba nipe muda nipumzike nitakuambia kila kitu.”
Niliwakuta watu wote waliokuwa wakiishi katika chumba cha Frank nadhani na
wao pia walitaka kujua nini kimetokea kwa maana waliacha kufanya walichokuwa
wakikifanya na kuniangalia mimi.
“Ok basi pumzika.” Frank alisema.
Alinilaza pale kitandani na kisha kunifunika shuka nilipitiwa na usingizi.
Nilikuja kushitushwa baada ya kuota ndoto ya kutisha na muda ulikuwa
umeshaenda sana.
“Nini?” Frank aliniambia baada ya kushituka usingizini.
“Sociolah una nini lakini?”
“Frank nimeota ndoto ya kutisha sana.”
“Ndoto gani?”
“Umeota nyoka wanakukimbiza.”
“Bora hata angekuwa nyoka.”
“Nini hiko ulichoota niambie basi Sociolah.”
Alinyanyuka pale alipokuwa amekaa na kuja kitandani alininyanyua na kisha
kuzungusha mkono wake begani kwangu.
“Niambie basi kuna nini?”
“Nimeota unanisaliti, tena na Melania.”
“Aaah...” Alicheka sana.“Hiko kitu hakiwezi kutokea Sociolah hata siku moja naomba uniamini mke
wangu kwanza mimi siwezi kutoka na mwanamke kama yule, mwanamke kama
mwanaume.”
Nilishindwa kujizuia ilinibidi kucheka nilisahau shida zote zilizokuwa zikitokea
katika chumba chetu.
“Frank mimi sielewi hali ya kule chumbani kwetu.”
“Kuna nini kwani?”
“Nimekuja nimekuta kuna kitu wanaoneshana kwenye simu ya Fetty halafu ghafla
wote wakaanza kukimbia na kuanza kuact differently, ilinishangaza sana
inaonekana kuna kitu walikuwa wakikiangalia kwenye simu ya Fetty na hawataki
nijue.”
“Mmmh nini iko?”
“Sijui kwa kweli mimi nashindwa kuelewa.”
Frank alikuna kichwa kana kwamba akijaribu kutafuta majibu, nilibaki tu
nikimuangalia ili niweze kusoma alichokuwa akikifikiria sikuweza kufanikiwa.
“Twende tukamalizie siku chumbani kwenu.”
Wazo lake lilinifurahisha sana kwa maana kwa kufanya hivyo ningeweza
kumuumiza roho Melania.
Tulitoka na Frank hadi chumbani kwetu nilifungua mlango na kuingia, kila mtu
alishangaa.
Frank alikuwa kama malaika.
Monica alikuwa bado amelala kitandani kwangu.
“Monii.... Monii....” Nilimuamsha.
“Niache...”
“Monii...”
“Niache nimesema.”
“Monii... Toka kitandani kwangu.” Nilimuambia kwa sauti Frank alicheka.
Alifunua shuka ghafla na kuamka.
“Aaah samahani nilikuwa sijui kama nimelala kitandani kwako.”
Nilicheka tu na kisha kumuacha.
“Aya toka.”
Alitoka na kisha kupanda kitandani kwake.
Mimi na Frank tuliingia kitandani kwetu na kukaa.
Tuliongea mawili matatu kwa sauti ya chini ambayo haikusikiwa na mtu yoyote na
kisha tukajifunika shuka na kujilaza, tukio hilo lilionekana kuwakera sana.Kila mtu alipanda kitandani kwake.
Tukiwepo kitandani tuliweza kuongea mambo mengi huku tukicheka kwa sauti
walichokuwa wakisikia ni kicheko tu hakuna sauti iliyotoka.
Tuliendelea kuongea hadi muda ulipokuwa umeenda sana.
“Twende tukatafute chakula tule halafu unipeleke kulala.”
Kabla sijajibu Melania aliachia msonyo wa hali ya juu.
Nilitabasamu tu na kisha nikaitikia kwa sauti zote.
“Sawa.”
Nikambusu kidogo mdomoni na kisha kutoka pale kitandani, alitoka kitandani na
kisha kuketi katika kingo za kitanda.
Nilinyanyuka na kuelekea kabatini kwangu nilifungua kabati na kutoa shati jingine.
“Nikivaa hili si nitapendeza?” Nilimuuliza Frank.
Kila mtu aligeuza macho yake.
“Yes umependeza, unapendeza katika kila kitu Sociolah.” Frank alisema.
Nilivua shati Frank aliachia tu tabasamu na kisha nikavaa shati lile jingine
nililokuwa nimelichagua na baada ya kuvaa nilikusanya vitu vichache na kisha
kutoka.
Tulielekea Complex kupata chakula cha jioni.
Tulikula huku tukiongea mawili matatu kila mtu alikuwa akituangalia, tulipiga
stori huku tukicheka sana na baada ya hapo nilimsindikiza hadi maegesho ya
magari.
Tuliongea mawili matatu na kisha tukaachana alielekea chumbani kwake na mimi
nilielekea chumbani kwangu.
Nilipofika mlangoni kwangu kilichokuwa kikiongelewa pale sikutaka kuamini
masiko yangu, nilihisi masikio yangu yakinidanganya kwa maana sikutegemea
kusikia kitu kama hicho.
Bila shaka ndani ya chumba chetu kulikuwa kuna ugomvi uliokuwa unaendelea
bila kuambiwa niliweza kujua kwamba Melania hayupo mule chumbani.
Ni ugomvi uliokuwa ukiendelea kati ya Fetty na Monica sikuwahi kuhisi kama
Monica na Fetty wangeweza kugombana kiasi hiko kwanza walikuwa wote ni
wapole.
Kwa kiasi fulani mimi na Melania tulionekana tumechangamka sana mbele yao
lakini ugomvi ule uliokuwa ukiendelea mule chumani ulinifungua macho kwamba
rafiki siyo mtu yoyote yule unayekutana naye ili mtu awe rafiki yako inabidikusiwe na sababu ya urafiki wenu kwani ile sababu ikipotea hakutakuwa tena na
urafiki kati yenu.
Nilisimama hapo mlangoni muda mrefu, walianzia mbali sana hadi kufikia kwenye
ugomvi wao.
“Aaanh kwa uzuri huo lazima tu agombane naye hata ningekuwa mimi lazima
ningeingia kwenye ugomvi naye.”
“Mimi ndiyo ninaingia naye kwenye ugomvi.” Fetty alisema.
“Eenhe.. Tutabanana hapo hapo hata mimi siachi.”
“Nini..? Unaongea nini?”
“Yani nakuambia hivi Melania si amesema lazima atoke na huyo Frank na mimi
niko hapo hapo.” Alijibu Monica kwa msisitizo.
“Sikia usitake kujifanya unamjua sana Frank, sisi Frank tunamjua tangu siku ya
kwanza hivyo tunaomba ukae mbali naye.”
“Yani hilo utanisamehe kwa kweli mwanaume mzuri kama Frank nani atakubali
amuache.”
“Monica huwezi kunitisha kwa chochote pambana na hali yako na mimi
nipambane na hali yangu fyuuu.... Tuone kama atakuchukua mtu mwenyewe kama
wewe.”
“Tutajua hapo hapo.”
Waliendelea kutamkiana maneno ya kashfa na ya ajabu nilishindwa kuelewa
inamaanisha chanzo cha ugomvi wote huu ni kwamba hawa watu wanamtaka
Frank. Hilo lilianza mbali kuwahi kuingia katika akili yangu.
“Inamaanisha Melania kumchukia Frank kote ni kwamba alikuwa anamtaka.
Kwanini asingemchukua mapema mpaka unafikia wakati mimi na Frank tuko naye
kwenye mahusiano na hata hivyo siwezi kuruhusu hiyo hali nitapambana naye
mpaka mwisho na kuanzia sasa nitamkomesha.”
Sikuingia chumbani niliondoka, nilitoka hadi kwenye maegesho ya magari na
kisha nikampigia simu Frank.
“Mama umeshanimisi?” Alianza kuongea mara baada ya kupokea simu yangu.
Nilicheka.
“Frank njoo, njoo parking nakusubiri kuna kitu nataka niongee na wewe.”
“Si tumeachana sasa hivi tu jamani.”
“Ndiyo naomba uje.”
Alishuka hadi maegesho ya magari.
“Tutafute sehemu tukae.”Ilikuwa mida ya saa nne.
Tulikaa nilimsimulia kila kitu nilichokisikia chumbani kwetu, alivuta pumzi na
kuzishusha......................
INAENDELEA.............

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search