Friday, 25 May 2018

NATAKA KUZAA- SEHEMU YA KUMI NA NNEMTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
Tuliingia kwenye kipindi cha saa sita na hapo tulikutana na Franklin, alikuwa
amevaa zile nguo ambazo nilimnunulia siku ya krismasi hakika alionekana
mtanashati, Melania hakuamini macho yake, niliona alipomuona aliachia mdomo
huku akiwa ametoa macho na kushindwa kuongea chochote wala kupiga hatua
alibaki amesimama.
Frank aliachia tabasamu nilishindwa kujizuia nilitamani sana kujifanya hatuko
pamoja lakini ilishindikana.
“You look very nice today.”“Thank you.” Frank alijibu, tabasamu lake lilikuwa zuri sana.
Watu waliacha walichokuwa wakifanya na kutuangalia.
Alibaki amesimama tu akinitazama na mimi wala sikuondoka tulibaki tumesimama
kama majitu.
Innocent alinijia.
“Haa.. Aisee...!! Ngoja niwapige picha ya ukumbusho.”
Watu wote walinigeukia na kunitazama, alitoa simu yake nzuri aina ya Samsung na
kutupiga picha. Tukaweka mapozi nikamsogelea Franklin nikamuegamia kifuani
nguo zake zilikuwa zimefanana kidogo na nguo nilizokuwa nimevaa siku hiyo,
nilikuwa nimevaa suruali nyeusi iliyonibana vizuri na shati ambalo lilikuwa
limekaa kifasheni jeupe lenye maua ya maruni na chini nilivaa viatu vya wazi
vyeusi tulipendeza hakika.
Tuliweka mapozi mbalimbali ya kupiga picha hakuna mtu ambaye alionekana
kufanya jambo jingine zaidi ya yote watu wote walikuwa wakituangalia sisi
wengine walidiriki kutoa simu zao na kutupiga picha pia.
Melania alishikwa na bumbuwazi tu asijue afanye nini, tulipiga picha hadi zoezi
lilipoonekana kumalizika.
Innocent alituletea picha ambazo alitupiga ili tuangalie, zilikuwa picha nzuri sana.
“Jamani naziomba.” Nilimuambia.
Melania aliniangalia kwa jicho kali na kisha kuingia darasani.
“Aya mimi nawaacha.” Innocent aliongea nakuondoka, nilitabasamu na
kumuangalia Innocent mpaka alipopotelea na kisha nikamgeukia Frank.
“Mambo?”
“Poa.”
“Unaendeleaje leo?”
“Naendelea vizuri, Sociolah ahsante for you company.”
Nilicheka tu.
“Ok.”
“Naenda.”
“Sawa.” Nilijibu.
Ni kama nilikuwa nikulazimisha uelewa wangu kwenda mbali na Frank.
Wakati tunapishana nilishindwa hata kuacha nafasi kati yetu nilijikuta namgonga,
nilirudi nyuma kidogo na kumtazama usoni, aliachia tabasamu na mimi niliachia
tabasamu pia, akasogea pembeni na mimi nikasogea pembeni.“Pita.”
“Pita wewe.”
“Hahaaa...” Nilicheka.
“Basi tupite wote.”
“Sawa.”
Tulibaki tumesimama tu tulicheka na kisha tukapita.
Niliingia darasani na yeye alitoka nje sikutaka kwenda kukaa na Melania ambaye
alikaa nyuma, nilitafuta siti ya mbele na kisha kukaa.
Baada ya muda Frank alirejea alikuja kukaa kiti cha pili kutoka kwangu,
nilimuangalia halafu nikaachia tabasamu hali kati yetu niliweka begi langu na yeye
aliweka la kwake.
Mwalimu aliingia.
Baada ya kipindi kuisha, kipindi ambacho kilikuwa cha mwisho kwa siku hiyo
watu walianza kutoka darasani kwa mafungu na kisha kuondoka kabisa.
Sikuonyesha dalili yoyote ya kuondoka wala Frank hakuonesha dalili yoyote ya
kuondoka, niliona watu wamepungua darasani nikamgeukia Frank alikuwa
akiniangalia tu muda mrefu.
“Oooh kuna nini?” Nilimuuliza.
“Umependeza.” Aliniambia.
“Aaah sijakuzidi wewe.”
“Hahaa...”
Alicheka tu.
Nilikuwa napenda sana alivyokua akicheka cheko zuri sana.
Nilimgeukia na yeye alinigeukia, akanyoosha mikono yake kwa ishara ya kutaka
nimpe mikono, nilimpa.
“Nakupenda sana Sociolah.” Aliniambia.
“Nakupenda pia.”
“Nafurahia sana umekuja katika maisha yangu ingawa....”
Nilimziba mdomo kwa mkono wangu.
“Hakuna kilichoharibika wala kitakachoharibika, kila kitu kitakuwa sawa.”
“Jana uliniogopesha sana Sociolah.” Frank aliongea.
“Kwanini?”
“Nimepiga simu umepokea nakuita baby huitikii halafu ghafla nasikia unagombana
na mtoto.”Nilicheka.
“Simu alipokea mdogo wangu anaitwa Pink, kuna siku nitakukutanisha naye.”
“Sawa nitafurahi sana kumuona inaonekana ni mtu ambaye anapenda utani
naamini tutafurahi kuwa pamoja.”
“Hahaha..... Hamna shaka usijali tutaonana sawa.”
“Ok.”
Alitupia macho nyuma yangu na mimi nilitupia macho nyuma yake hakukuwa na
mtu tuliona kama nafasi, tulisogeleana karibu na kutaka kubusiana.
“Hey stop...” Sauti kali ilipenya kwenye masikio yetu tuligutuka na kugeuka kule
sauti ilipotokea.
Kumbe wakati wote Melania hakuwa ameondoka alikuwa amekaa pale pale
alipokuawa amekaa na akituangalia.
“Unafanya nini Sociolah?”
“Hahaha...” Nilicheka
“Nothing..”
“Nothing...! Unamaanisha ulichokuwa unafanya hapa eti ni nothing Sociolah usiwe
mjinga. Wewe toka hapa, uko kama kinyago.”
“Hey.... Shut up...” Nilimuambia
“Shut up nini siwezi kuvumilia kuona upuuzi kama huu toka mbele yangu.”
Alimfukuza Frank.
Frank alibeba begi lake na kisha kuondoka.
“Sociolah unachanganyikiwa eeeh?!”
“Hapana kwani kuna nini kibaya?”
“Ulitaka kufanya nini pale?”
“Nothing.”
Nilibeba begi langu na kuondoka.
Moja kwa moja nilienda nyumbani wala sikutaka kuulizia kumsikiliza Melania.
Nilipofika tu Fetty alinitafuta.
“Umemfanya nini na Melania wewe?”
“Kuna nini kwani?”
“Melania kasema anakuchukia.”
“Haaa! Kwani nimefanya nini?”
“Mimi sijui.”
“Any way nikija naamini tutasolve ni maugomvi tu ya kawaida.”“Sawa take care.”
“Hamna shida.”
Mwishoni mwa wiki mama aliniambia niwapeleke watoto beach nilichukia sana
maana nilikuwa sipendi kutembea na wakina Pink
“Mnataka beach gani?”
“Tunataka utupeleke Mikadi.”
“Mtaenda wenyewe mimi simpeleki mtu Mikadi.”
“Nini.... Mama kasema utupeleke.”
“Mkitaka kwenda beach nawapeleka Kunduchi huko kwingine mtajua wenyewe
sipeleki mtoto wa mtu.” Niliongea.
“Aaah... Mama kasema utupeleke.”
“Mtajua sasa kama mnataka kwenda beach twendeni.”
Pinto akaitikia, “Twende.”
“Mimi hata nilikuwa sitaki kwenda Kunduchi.”
“Mimi sitaki kuendesha gari umbali mrefu.”
Walijiandaa, nikawabeba na kisha kuwapeleka.
Tulienda moja kwa moja mpaka kunduchi beach, walibadilisha nguo zao na kasha
kuanza kuogelea.
Pink na Pinto walikuwa wakipenda sana kuogelea na zaidi ya sana walikuwa
wakipenda kuogelea baharini.
Waliogelea huku nikiwa nimekaa pembeni nilitandika kitenge changu na kisha
nikatoa dompo nikawa nakunywa taratibu kabisa huku nikichat.
Nilimtafuta Frank lakini hakuwepo hewani nikawa nachat tu kwenye makundi
mbalimbali.
Mara ghafla Pink na Pinto walikuja huku wakikimbia kwa kasi.
“Dada..... Dada.... Tukuchekeshe.”
“Mnichekeshe nini?”
“Angalia pembeni yako.”
Nilitupia macho pembeni ambapo Pink na Pinto walikuwa wanapazungumzia nusu
nizirai.
Sikutaka kuamini macho yangu kwamba alikuwa ni Frank.
“Mungu wangu! Amefuata nini huyu hapa, kwanini hajaniambia kama anakuja
huku, haaa!”
Akili yangu ilichanganyikiwa sana.Na hapo hapo Frank aligeuza macho yake na yaligongana na ya kwangu
nilikimbiza ya kwangu pembeni haraka nilikuwa nimeshachelewa.
Frank alinyanyuka pale alipokuwa na kusogea upande wetu.
Kila mara nilipokuwa nikimuona huyu mwanaume moyo wangu ulijawa na furaha
sana sikusita kunyanyuka na kumkimbilia kisha tukakumbatiana na kuninyanyua
na kunizungusha baada ya kunishusha alinibusu kidogo mdomoni.
“Naona uko na watoto, ndiyo wakina Pink wenyewe?”
“Yes, njoo ujuane nao.”
Tulivyofika pale Pink alibaki ametoa macho tu kama haamini.
“Shikamoo anko.” Pinto alisalimia.
“Marhaba.” Frank alimshika shavu Pinto, Pink alicheka.
“Shikamoo.” Pink alisalimia.
“Marhabaa wewe ndiyo utakuwa Pink si ndiyo.”
“Ndiyo mimi.” Alimjibu.
“Mzoee tu Pink.” Pink aliniangalia kana kwamba anataka kuniambia kitu
nilimuangalia.
“Nini?”
“Hamna kitu.”
“Hahaha...” Nilicheka.
“Karibu tukae, nyie nendeni mkaoge.”
Pink aliniangalia ni kama ana jambo alikuwa anataka kuniambia na kisha
akaondoka..........
INAENDELEA..............

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search