Friday, 25 May 2018

NATAKA KUZAA -SEHEMU YA KUMI NA SITAMTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
Tulizunguka zunguka hadi muda ulipokuwa umeenda sana na kisha tukarejea pale
tulipokuwa tumewaacha wakina Pink.
“Mpo salama.”
“Ndiyo.”
“Ok.”
“Tunaondoka saa hizi tunarudi nyumbani sawa.”
“Eeeh dada mimi nimechoka.” Pinto alisema.
“Sawa na anko Frank tunaenda naye?” Pinto alisema baada ya kuona tunaelekea
kwenye gari.
“Ndiyo.”
“Anaenda mpaka nyumbani?” Nilicheka.
“Eee tunaenda naye.”
“Haaa! Pink alihamaki.
“Nini na wewe.”“Eehe dada huyu hapo ndiyo yule ambaye my oga eeh?” Aliuliza.
Nilicheka nilicheka sana mpaka nilishindwa kujizuia nikaegamia usukani mara
baada ya kuingia kwenye gari huku nikiendelea kucheka, Frank naye alicheka.
“Pink unapenda sana utani.”
“Mimi sitanii.” aliongea huku akionesha msisitizo.
“Eeee.. Ndiyo yeye.” Niliitikia.
“Ooh.. Ila anafanana na na....” Aliamua kuishia kati.
“Halafu dada huyu si ndiyo.....” Pinto alimziba mdomo.
“Nini.... Nini.... Pink usije ukanifanya nikakupiga hapa sasa hivi unataka kuongea
nini?”
“Akaa nimekosea twende.” Aliongea.
Nilijuta sana kuwa na mdogo ambaye ana maneno mengi kama Pink mara mia
Pinto nilichukia nilishika usukani wa gari na kuondoa gari kutoka pale Kunduchi
beach.
“Sikia Pink nampeleka kwanza Franklin hostel.”
“Si umesema tunaenda naye nyumbani.”
“Nilijua tu hatuwezi kwenda naye, mmmh heri ninyamaze.” Pink aliongea.
Niliamua kucheka ili kumpa imani Frank naye alicheka baada ya kuniona mimi
nimechaka.“Pink bwana una utani sana.” Alicheka tu Pink na kisha hali ya ukimya ilitawala
katika gari.
Niliendesha gari kwa umakini sana huku nikiwa na mawazo mengi hadi tulipofika
katika mabweni ya mabibo.
Niliingiza gari hadi ndani kabisa giza lilikuwa tayari limeisha ingia nilizima taa za
kwenye gari na kisha kumbusu Frank mdomoni.
“Byee.”
“Ok byee.”
“Aya.”
Frank alishuka huku kuonyesha kutoridhika hata mimi nilitamani kuendelea kuwa
naye.
Niligeuza gari na safari ya kuelekea nyumbani ilianza, kila nilipokuwa
nikimuangalia Pink kupitia kioo cha pale mbele alikuwa tu akiangalia dirishani.
“Pink.” Nilimuita.
“Bee dada.”
“Unajisikiaje?”
“Nahisi usingizi dada,”
“Usijali tutafika nyumbani sasa hivi na utaenda kupumzika mdogo wangu sawa,
usiongee kitu chochote kuhusu anko Frank.”
Ni kama nilimshitusha Pinto.“Kwanini dada mbona mzuri au kwasababu baba atamjua ndiyo Matranka.”
Aliongea.
“Kelele.... Nishawambia siyo Matranka niliwambia anaitwa Frank.”
Pink hakujibu chochote alionekana kuelemewa na usingizi.
Hii ilikuwa mbaya sana kwangu kama asingenisikia angeweza kuongea.
Tuliendelea na safari hadi tulipofika nyumbani na baada ya kufika nyumbani
wakina Pink walikuwa wamechoka sana, walioga na kisha kulala.
Asubuhi ya siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya ijumaa nilienda chuoni kama kawaida
Melania hakutaka kuniongelesha kabisa. Ulipofika wakati wa mwenda kunywa
chai nilimkuta Fetty akiwa anatusubiri nilikuwa wa kwanza kumfikia Fetty na
Melania alikuja na kutupita tu.
“Mmmh shosti hali mbaya.” Fetty aliongea.
“Yani Melania usiku kucha anaongea tu anakutukana, analia.”
“Sasa mimi nimefanyaje lakini.” Niliongea sijui.
“Kwa kweli na wala hata sijui nifanyeje hali mbaya nitakuja jumapili tutasolve
hayo mambo yote.”
“Sociolah usijidanganye kwama Melania atakusikiliza mi naona ukija ugonge mara
mbili.”
“Weee...!”
“Kweli mtafute Monica akuambie kila kitu hali ni mbaya anasema yani lazima
akufanyie kitu kibaya.”“Mungu wangu! Amepatwa na nini Melania kwani shida iko wapi si ni jambo tu la
kukaa chini na kuongea.”
“Kasema hataki kusikia chochote kuhusu wewe.”
“Shit... Nitakuja na nitahakikisha tatizo linaisha,”
“Mmmh...Sawa.” Melania alikaa mbali na sisi siku hiyo.
Nilikunywa chai tukiwa na Fetty tukiongea mawili matatu, na baada ya hapo
niliachana na Fetty na kisha kuelekea darasani.
Melania aligoma kabisa kuzungumza na mimi, watu wengi walikuwa wakiongea
kuhusu sisi kila mtu akitaja sababu yake nilinyamaza tu kimya bila kuongea
chochote.
Nilirudi nyumbani baada ya vipindi kuisha, nashukuru Mungu Pink ana Pinto
hawakuwa wameongea chochote kile.
Siku ya jumapili mama alinipeleka hostel.
Nilikuwa naogopa, alinishusha mpaka nje ya bweni letu.
“Nakupeleka mpaka chumbani kwenu.”
“Nilihofia hali ambayo mama anaweza akaikuta kule.”
“Aaah.. Mama usijali unaweza tu ukaenda nashukuru nimefika salama naweza
kubeba na mabegi haya na nikafika usijali mama.”
“Sawa uwe na wakati mwema mwangu, kuwa makini sawa eee.”
“Aya mama usijali.”“Sawa.” Alinivuta karibu na kisha kunibusu kwenye paji la uso mara nyingi mama
alikuwa anapenda sana kunibusu kwenye paji la uso aliniambia inaonesha ni kiasi
gani ananipenda.
Nilimuangalia hadi alipopanda kwenye gani na kisha kuondoka, nilivuta begi langu
kivivu na kiunyonge kuelekea chumbani kwetu.
Nilipofika mlangoni nilisita kufungua malango.
Na wakati najiuliza niingia au nifanyeje mlango ulifunguliwa na kisha Melania
alichomoza.
Alinipandisha na kunishusha na kisha akaachia msonyo ambao hata sikuwahi
kujua kama Melania alikuwa akiweza kuachia msonyo wa aina ile. Alinisukuma na
kisha alipita kuendelea na safari yake.
Nilibaki tu nimeshikilia begi langu, nilisimama mlangoni kwa dakika kadhaa.
Alipita moja ya watu ambao walikuwa katika vyumba vya jirani.
“Aaah Sociolah umerudi mbona umesimama tu hapo mlangoni?”
Mlango ulifunguliwa na kisha Monica alitoka.
“Sociolah....” Alinifuata na kunikumbatia. Nilimkumbatia.
“Mbona huingii?”
“Naingia.”
“Umekutana na Melania?” Aliniuliza.
“Yeah nimekutana naye.”
“Vipi kakusalimia?”
“Hamna kanipita tu.”
“Oooh pole, ingia ndani basi upumzike.”
Nikaingia ndani.
Monica kwa kifupi alianza kuniambia hali halisi ilivyo humu ndani. Alieleza jinsi
ambavyo Melania alikuwa akiongelea kuhusu ugomvi uliokuwa baina yetu,
alielezea vitisho vyote ambavyo Melania alikuwa akiwaambia kuhusu mimi na
mwisho aliniambia kwamba nina wakati mgumu sana.
“Sociolah sijui kama amani itakuwepo humu ndani.”
“Aah achana naye mimi naamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa wala hata
usijali.”
Nilipanga vitu vyangu haraka kwenye kabati na kisha kutoka.“Nitarudi muda si mrefu.” Nilimuaga na kuondoka.
Nilitoka moja kwa moja hadi chumbani kwa kina Frank sikutaka hata kumuambia
kama nimefika. Niligonga mlango na kisha kuingia ndani.................
INAENDELEA..............

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search