Friday, 25 May 2018

NATAKA KUZAA- SEHEMU YA KUMI NA TANO


MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
Pink aliniangalia ni kama ana jambo alikuwa anataka kuniambia na kisha
akaondoka.
Frank alilala pembeni yangu tukawa tunaongea mambo mbalimbali yaliyokuwa
yakituhusu.
“Frank mimi nataka tukimaliza kusoma tukae pamoja.”
“Inategemea Sociolah.”
“Lakini Frank hujawai kuniambia kuhusu familia yenu.”
“Kwahiyo unataka nikuambie hapa sasa hivi?”
“Kama inawezekana”
“Ok mimi nakaa na mama yangu ni mkulima tunaishi zetu huko Ifakara.”
“Aaah.. Sasa wewe ni kabila gani?”
“Mimi ni msukuma, mama yangu alihamia Ifakara kwasababu alisikia ardhi ya
kule ina rutuba sana kwahiyo alienda kule kwa ajili ya kufanya kilimo.”“Ok, mpo wangapi kwenu?”
“Tuko watatu na mimi ndiyo wa kwanza.”
“Woow..”
“Na wadogo zangu wawili wakike na wa kiume.”
“Well.”
“Mmoja anaitwa Fiona na mwingine anaitwa Furaha.”
“Aahaa, sasa kati ya hao nani wa kiume.”
“Furaha ndiyo wa kiume.”
“Hahaha... Mbona mmempa jina la kike.”
“Mmmh jina la kike kwani lina matiti?”
Nilicheka sana.
“Wewe Frank wewe acha utani.”
“Serious nakuambia.”
“Aya bwana nimefurahi kujua familia yako, si kunasiku utapenda twende Ifakara.”
“Aaah lakini haiwezekani acha tu.”
“Kwanini haiwezekani Frank.”
“Wewe unaweza kwenda Ifakara? Umezoea vumbi wewe?”
“Hahaha vumbi tu, Sema kingine.”
“Kuna kuchota maji utaweza wewe?”
“Nitaweza.”
“Aya unakaribishwa.”
“Ahsante nitakuja.”
“Nitafurahi sana.”
“Ok.”
Tuliendelea kufurahi, kwa kweli siku yangu ilikuwa ya furaha sana.
“Frank kesho naweza kurudi Hostel.”
“Kweli?”
“Yeah.”
“Basi itakuwa vizuri.”
Mara Pink na Pinto walirudi.
“Vipi?”
“Tumekuja kupumzika kidogo.”
“Mimi nataka kutembea tembea.” Niliwaambia.
“Mnaenda wapi sasa?”“Tunazunguka hapo tu kidogo.”
“Mmmh... Sisi tunataka kula Icecream.” Walianza kulalamika.
“Mnataka hela?” Niliwapa elfu kumi.
“Mbona unawapa hela kubwa hivyo.”
“Wataenda kunisemea kwa mama nimewanyima hela we waache tu.”
“Nyie kwenu mnadekezwa sana.”
“Hamna kawaida tu.”
“Frank kwanini hujaniambia kuhusu baba yako.” Aligeukia pembeni.
“Baba... Baba alifariki wakati tuko wadogo kabisa.”
“Oooh pole.... Pole sikutegemea kukuumiza.”
“Wala hata hujaniumiza ila utaniumiza tu endapoo.... Aaah.... Twende basi
tukatembee.”
“Endapo nini mbona humalizii.”
“Twende tukatembee.”
“Mmmh sawa.”
Tulinyanyuka na kuanza kupiga hatua za kichovu kutembea.
Tulitembea na kila mtu aliyetuona hakuacha kuhisi kwamba sisi ni wapendanao wa
muda mrefu, tulitembea huku tumeshikana mikono na mara nyingine nilikuwa
nikicheka na kumuegamia kifuani Frank.
Wakati mwingine alikuwa akinikumbatia kutokea nyuma na tukitembea kama
kumbikumbi, mara nyingine alinibeba, alinibusu, alitangulia mbele yangu
akanishika mikono huku akinitazama na kisha kunivuta, mara nyingine
tulikimbizana ilikuwa ni furaha sana tupo pamoja.
Wakati huo kwa pemeni kulikuwa ni kama watu wakifanya sherehe tulipita
pembeni yao huku tukiendelea kukimbizana kama watoto.
“Sociolah...”
“Yes Frank.”
Nilimgeukia Frank ambaye nilihisi alikuwa ameniita, nilimkuta Frank ameshikwa
na bumbuwazi tu.
“Nini...?” Alinigeukia na kunitazama mimi.
“Si umeniita.”
Frank hakunijibu.
“Bae si umeniita mbona usemi kitu?”
Alitikisa kichwa kwa ishara ya kukataa.“Hasa kaniita nani au nimesikia vibaya?”
Alinyanyua mkono wake ishara ya kunioneshea wapi mtu aliyeniita alitokea,
niligeuza macho yangu na kutazama kule ambapo Frank alikuwa akinionyesha.
Nilihisi kizunguzungu kana kwamba ningepoteza fahamu muda wowote ule.
Nilijishika kichwa kwa kuwa sikuamini mtu ambaye nilikuwa nikimuona mbele
yangu. Kitu cha kwanza kilichofanya nisijiamini nilikuwa sina neno la kumuambia
kwa wakati huo, ningemuambia nini katika mazingira hayo ambayo alinikuta nayo,
ambayo bila shaka yalionesha kwamba nina uhusiano wa kimapenzi na Frank.
Ningemuelezea nini hadi anielewe, ningefanya maamuzi gani ya haraka hapo.
Hakika lilikuwa tukio la kuchanganya akili zangu, nilijikaza.
Wala haikuhitaji maelezo aliyekuwa mbele yangu alikuwa ni Patrick, ingawa kwa
wakati huo sikuwa nikimpenda kabisa Patrick, kukutana naye katika hali kama
hiyo kulinishtua.
“Sociolah unafanya nini hapa na wewe ni nani?” Aliniuliza.
Nilimuangalia Franklin uso wake ulionekana kuhamanika sana alishindwa kitu cha
kuongea.
Nilipatwa na ujasiri wa aina yake ambao mpaka leo sikumbuki niliupataje
“Oooh Patrick mambo?” Nilimuuliza alishindwa kunijibu alikuwa akiniangalia
mimi na kisha akimuangalia Franklin.
“Sociolah mimi sielewi nielezee.”
“Aaah Patrick kitu gani ambacho huelewi?”
“Huyu ni nani? Nijibu Sociolah.”
“Aaah usipaniki nisikilize kwa makini Patrick, mimi kutoka kwako sikuwa
nikihitaji hela kwa sababu kama hela kwetu tunazo zinatutosha. Kutoka kwako
nilikuwa nahitaji mapenzi na muda wako lakini wewe hivyo vyote hukuvijali sijui
ulikuwa unaniwazia nini sawa kuna wakati nilikuwa sina hela na nikaja kwako
kukuomba hela lakini haimaniishi kwamba nilikuwa sina uwezo wa kupata hizohela nilikuwa nao sana, kitu ambacho nilikuwa nikikihitaji kutoka kwako ni faraja
na muda wako lakini wewe huna mimi siwezi. Nimeenda sehemu ambayo ninapata
faraja na pia ninapewa muda.”
“Sociolah...” Alionekana kuchanganyikiwa hadi ashindwe cha kuongea.
“Si ungeniambia tu mama mimi nakupenda.”
“Hapana, hakuna nafasi tena, am sorry Patrick, bye....”
Niliondoka alinivuta Frank naye alinivuta upande mwingine.
“Muachie nimekwambia.” Patrick aliongea kwa hasira.
Frank aliachia tabasamu lake lililonimaliza kabisa ingawa nilikuwa radhi kuelekea
kwa Frank lakini moyo wangu haukuwa umefanya chaguo.
“Muache mke wangu.” Frank aliongea.
“Si ameishakuambia, kuna cha ziada ambacho unataka kumuuliza muulize kiupole
ama sivyo hali ya hewa itabadilika sasa hivi.” Aliongea Frank kwa msisitizo.
Patrick alionekana kutetereka, nilimjua alikuwa siyo mgomvi wala hawezi
maswala ya ugomvi, kwa upande wa Frank sikuwa nikijua kama alikuwa akiongea
siriazi ingawa alionesha kuwa hatanii.
“Muache..” Frank alirudia.
Patrick aliniangalia.
“Sociolah ndiyo kusema.....”
“Tumeachana.”Aliishia kati na kushindwa kuendelea na mimi niliamua kumalizia ili kuondoa
utata.
“Sitaki kuamini macho yangu.” Aliniachia mkono wangu na kisha kufunika macho
yake kwa viganja vyake alipokuja kufunua macho yake Frank alikuwa amenishika
kiuno na tulikuwa mita kadhaa kutoka pale alipokuwa tulishaondoka muda mrefu.
“Sociolah....” Alibakia akiniita, nilipunga mkono bila kugeuka huku tukizidi
kuongea kwa ishara ya kwaheri.
Tulizunguka zunguka hadi muda ulipokuwa umeenda sana na kisha tukarejea pale
tulipokuwa tumewaacha wakina Pink.....................
INAENDELEA.....................

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search