Friday, 25 May 2018

NATAKA KUZAA SEHEMU YA KUMI NA TATU


MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
NAMBA YA SIMU: 0683777152
Kinyume na matarajio yangu yule mtu hakuwa yule mkaka niliyemkuta pale
chumbani alikuwa ni Innocent. Hakika alipigwa na butwaa sana kuniona mule
chumbani kwa maana alibaki ameachia mdomo wazi huku amesimama pale
mlangoni kana kwamba mtu ambaye anataka kukimbia lakini akaishiwa nguvu.
“Sociolah...” Alipata nguvu ya kuongea niliachia tabasamu.
“Yes..”
“Unafanya nini hapa?”
Huku nikiwa na tabasamu lililoupamba uso wangu.
“Kwani kuna tatizo lolote mimi kuwepo hapa?”
Alishangaa tu.
Mkononi alikuwa ameshika mfuko alifunga mlango na kisha kusimama.
“Sijaelewa maana ya uwepo wako hapa, umekuja kufanya nini?Nani aliyekuita
humu? Na umeingiaje kwenye hiki chumba? Na umejuaje kama Frank anakaa
humu?”
Aliuliza maswali mfululizo na ambayo yalionesha hayana mwisho.
“Hey stop... Mimi ni CR nimekuja kumuangalia memba wangu wa Darasa
anaumwa.”
“Aaah Sociolah!!” Alishindwa tena kuendelea kuniongelesha.
“Au bado mnania mbaya na Frank umekuja kumfanyia nini?”
“Eeeh.... Eeeh....” Frank anageuka na kumtazama.
“Kama angekuwa na nia mbaya wewe unafikiri angenishinda?”
“Anafanya nini sasa hapa?”
Frank aliachia tabasamu tu, nilinyanyuka mgongoni kwake na kisha kukaa.
Frank naye alijitahidi kunyanyuka akakaa na kisha akazungusha mkono wake
kiunoni kwangu akanivutia kwake, nikamuegamia begani.
“Sapraizi...” Frank aliongea.
“Whaat?!..... Mimi sielewi mnataka kujaribu kunionesha nini? Am i dreaming?”
“Vyovyote vile.”
“Ahaa... Kwanza Frank si unaumwa.”
Innocent alianza kuishiwa point alipiga hatua zilizoonesha kuchoka hadi karibu na
meza alivuta kiti na kukaa huku akitutazama.
“Ndiyo anaumwa.” Nilijibu.
“Sociolah mimi bado nashindwa kuelewa hebu basi nielezeeni niwaelewe.”
“Am.... Dating.... Frank” Nilijibu.
“Tangu lini?”“Tuna about a month.”
“Aaah!” Huku akijawa na mshangao aliachia tabasamu.
“Aisee... Mimi siamini acheni kunidanganya.”
“Unataka tufanye nini ili uamini?”
“You guys kissing each other....”
Nikamuangalia Frank alikuwa ameachia tabasamu lake zuri kabisa kwa kweli
nilisahau kama pembeni kuna mtu ingawa katika hali ya kawaida ningeona aibu.
Nilimvuta Frank karibu yangu na kisha tukafuatia na busu zito na refu sana,
tulijisahau kama pembeni yetu kuna mtu.
Aaah.... Basi inatosha inatosha.”
Innocent alisema na hapo akatushitua.
“Kwahiyo mnafanya kama mnanikomesha vile.”
“Aaah.... Hamna wewe si hutaki kuamini.”
“Aaah kwahiyo ilikuaje kuaje hasa.”
Nilicheka.
“Unataka ujue ili iweje yani?”
“Mimi bado mmeniacha na bumbuwazi nashangaa sana hata sijawahi kuhisi na
ndugu yangu Frank hata kuniambia!”
Aliongea Innocent kwa bashasha zote.
“Nilikuwa nasubiri kitu kama hiki kitokee.”
“Hongera sana Sociolah mama, wewe ni mtu mzima.”
“Mmmhh..” Niliachia tu kicheko.
“Ok basi kama umepata mtu wa kukuangalia acha mimi niondoke.”
“Aaah no mimi nimetoroka tu chuoni.”
“Hata mimi nimetoroka maana Frank alinitumia meseji hajisikii vizuri nimemletea
dawa hizi hapa atumie.”
“Kwasababu uko naye hapo unamuangalia acha mimi nirudi chuoni kuliko tukae
hapa tukakosa vipindi wote.”
“Hahaha... Aya nenda kasome halafu mimi utakuja kunielekeza si eti eeh.”
Niliongea.
“Sawa bwana.”
Alindoka nilifungua baadhi ya dawa na kumpatia Frank.
Tuliendelea kupiga stori za hapa na pale huku tukiwa tumejilaza pale kitandani.
“Frank kuna kitu ulisema unataka kuniambia.”
Alicheka.“Mimi naumwa bwana unaniambia vitu gani hivyo badala ya kunifariji unaanza
kuleta mambo ya ajabu.”
“Hasa kwani hicho si unakijua wewe mimi sijui kama ni cha ajabu pengine ni
kizuri kinaweza kukufanya upone.”
“Hahaha aya bwana nitakwambia siku yake mama usiwe na papara sawa.”
“Aaah.. Hasa siku yake siku gani?”
“Sikia Sociolah yani ni kama embe saa hizi halijaiva litakuwa chungu lina uchachu
subiri liive na utakula.”
“Bwana sasa si bora usingeniambia ukasubiri siku ambayo unataka kuniambia.”
“Sorry mama kwa hilo samahani.”
“Mmmh mimi nimekasirika.”
“Usikasirike basi mke wangu.”
Nilishituka na kumgeukia na kumuangalia.
“Umeniita nani?”
“Sociolah.”
“Bwana siyo hivyo.”
“Kweli nimekuita Sociolah.”
“Hamna hujaniita hivyo yani kama umesikia kitu kingine basi ni mawazo yako
mimi nimekuita Sociolah.”
Alinifanya niamini kweli ameongea hivyo.
“Mmmh mimi sidhani bwana halafu wewe unapenda sana utani.”
“Sasa kama umenisikia unataka tena nini.”
“Hahaha.” Nilicheka.
“Mimi nataka tu urudie, rudia basi mpenzi wangu.”
“Nimekuita Sociolah.”
“Bwana siyo hivyo.”
“Sasa umuamini mume wako?”
Niligeuka na kumtazama nikashindwa cha kuongea.
“Eti mke wangu huniamini.”
“ahaa...” Nilitabasamu tu.
“Nakuamimi mume wangu.”
“Sawa nakupenda.”
“Nakupenda pia.”
Nikajilaza kifuani wake ghafla simu yangu ilita.Niliivuta haraka haraka nilijua tu ni Melania alikuwa akinitafuta, hakuwa ni
Melania alikuwa ni mama.
“Mwanangu...” Aliniita tu nilivyopokea simu.
“Yes mom.”
“Nimepatwa na dharula naelekea ofisini kwa baba yako kwahiyo naomba uchukue
usafiri utakaokurudisha nyumbani kama huna hela ya kutosha niambie nikutumie.”
“No mom ninayo hela ya kutosha.”
“Ok fanya hivyo mwanangu sorry kwa usumbufu.”
“Usijali mama naelewa.”
“Aya ahsante binti yangu uwe na wakati mwema.”
Aliongea na kukata simu, hakujua tu kuwa amenipa furaha sana nilijua tu kama
mama angechelewa kurudi nyumbani hivyo nilikuwa na muda mrefu wa kukaa na
Frank siku hiyo.
Nilikaa hadi jioni na kisha nilitoka na kurudi nyumbani niliwakuta wakina Pink na
dada Linah.
“Baba mbona hajarudi wala mama.”
“Mama na baba wameenda kazini.”
“Oooh mimi nimeshawamisi.”
“Umewamisi nini?”
Pink na Pinto walianza kujibizana niliwaacha tu na kuelekea chumbani kwangu.
Niliingia chumbani kwangu na kupitiliza bafuni kwakuwa bafu lilikuwa lilikuwa
chumbani kwangu yani master bedroom.
Nilioga kuondoa uchovu na nilitoka nilimkuta Pink alikuwa ameshikilia simu
yangu sikioni.
“Aaah..! Pink unafanya nini?” Niliongea.
“Baby wako alipiga.” Huku akinipa simu yangu.
“Nini?!!”
Aliongea, “Mimi nimeingia nimekuta simu yako inaita umeandika my oga, oga si
maana yake Oxygen eeenh.”
“Haaa..!!”
“Nimepokea akaniambia baby, hii hapa.”
Simu ilikatika.
“Jesus..!!!!”
“Pink..... Pink.... Nakuomba usiseme usimuambie baba kitu chochote sawa.”
Alipandisha mabega juu na kubinua mdomo wake na kisha alitoka nje.Siku iliyofuata asubuhi na mapema mama alinipeleka chuoni.
Tulifika alinishusha kama kawaida mbele ya darasa letu watu wengi walikuwa
wamesimama mbele ya darasa letu wakituangalia, nilishuka moja kwa moja
Melania alikuwa akinisubiri.
“Sociolah..” Aliniita, nilihisi kama tayari wameshapata taarifa kuhusian na
kilichotekea jana ambacho Innocent alikishuhudia.
“Are you fine?”
“Yes i am.”
“Uliyekuwa unamuulizia amekuja mwanafunzi wa darasa lako.”
Nilicheka tu.
“Kama amekuja basi ni vizuri.”
“Jana ulienda wapi?”
“Aaah...” Nilishindwa cha kumjibu.
“Aaah... Hata sijisikii vizuri leo.” Niliamua tu kumchanganyia mada.
“Una nini kwani?”
“Hamna sina kitu ila tu najihisi kuchoka choka.”
“Basi pole tulia usizungukezunguke sawa eeeh.”
Nilikuwa nikipenda sana jinsi ambavyo walikuwa wakinijali.
“Nimemmisi sana Fetty.”
“Jana si ulikimbia wenzako tumeenda mgahawani tukajua tutakuwa pamoja
hukuwepo.”
“Ila leo nitakuwepo tutakula pamoja.”
Na kweli ulipowadia muda wa kwenda kunywa chai tuliondoka pamoja na
kumkuta Fetty akitusubiri, alinikumbatia kwa nguvu zote watu wote walikuwa
wanajua ni kiasi gani tulikuwa tukipendana. Tulipata chakula na kisha tuliendelea
na ratiba nyingine za chuoni.
Tuliingia kwenye kipindi cha saa sita na hapo tulikutana na Franklin, alikuwa
amevaa zile nguo ambazo nilimnunulia siku ya krismasi hakika alionekana
mtanashati, Melania hakuamini macho yake, niliona alipomuona aliachia mdomo
huku akiwa ametoa macho na kushindwa kuongea chochote wala kupiga hatua
alibaki amesimama.................
INAENDELEA.................

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search