Thursday, 31 May 2018

NATAKA KUZAA- SEHEMU YA KUMI NA TISA

MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
Ilikuwa mida ya saa nne.
Tulikaa nilimsimulia kila kitu nilichokisikia chumbani kwetu, alivuta pumzi na
kuzishusha.
“Hao watu wamechanganyikiwa nini, hivi wanafikiri mimi nitaweza kukuacha
wewe Sociolah kwasababu ya wale, sikia nikuambie kitu Sociolah wewe
ulinipenda wakati mimi sina kitu chochote, ulinipenda wakati nikiwa sina hadhi
yoyote hata mbele za watu, ulinipenda wakati kila mtu ananidharau siwezi
nikakuacha hata iweje nakupenda sana.”
Maneno yake yalinitia nguvu na jeuri.
“Nashukuru Frank.”
“Nataka tuwaoneshe kwamba mimi na wewe hatutoachana sawa.” Aliongea huku
akitabasamu.
“Nitafurahi sana.”
“Usijali.”
Tulitoka pale hadi chumbani, chumba kilikuwa kipo kimya niliingia.
Melania alikuwa amerudi huku kila mtu alikuwa anaendelea na shughuli zake
kimya kimya hakukuonekana dalili ya usalama wala amani mule ndani.
Niliingia na kisha Frank alifuatia nyuma yangu alikuwa amenishika kiuno huku
tukitembea kama kumbikumbi.
Frank alikuwa akinitekenya.
“Niache.”
Kila mtu alinigeukia na kuniangalia nilimuona jinsi ambavyo Melania alikuwa
amechukia.
Tulienda mpaka kitandani akakaa na kisha nikamkalia kwa juu nikamgeukia na
kumtazama na kisha lilifuatiwa na busu refu.
“Aaanh,.. Nakupenda.” Aliniambia Frank mara baada ya kukatisha busu hilo.
“Nakupenda pia.”
Alinichapa kofi kidogo.
“Nini lakini.”
Tuliendelea kuongea mawili matatu huku tukicheka kwa sauti.
“Nahisi usingizi.”
“Kesho tusiende chuo.” Nilimuambia.
“Kweli eeehe.”
“Eeenh...”
Aliitikia, “Hamna shida hatutaenda.”Nilisahau kama kesho ni mwisho wa wiki (Ijumaa) hivyo nilitakiwa niende
nyumbani na mama baada ya kutoka chuoni.
Aliniaga na kusimama na kisha kutembea hadi mlangoni nilisimama na kisha
kujongea mahali alipokuwa amesimama pale mlangoni, nilisogea hadi karibu yake
alinyanyua mikono yake na kisha kuizungusha kwenye kiuno changu nilichukua
mikono yamgu na kuizungushia begani kwake.
Alinibusu na busu hilo lilichukua muda mrefu kidogo. Baada ya sekunde kadhaa
aliniachia.
“Uwe na usiku mwema.” Aliniambia.
“Sawa, same.”
Aliondoka nilivuta pumzi na kuishusha na kisha kufunga mlango na kuuegamia
macho sita ya watu watatu yalikuwa yakinitazama mimi.
Nilivua nguo zangu na kisha nikachemsha maji na kuelekea bafuni kuoga,
niliporudi nilivaa gauni langu jepesi la kulalia la rangi ya pink na kisha
niliukumbatia mdori wangu na kisha kulala huku nikitabasamu sikutaka hata
kusikia wanaongea nini wala nini kinaendelea.
Asubuhi nilipoamka hakukuwepo na mtu hata mmoja na simu yangu alikuwa akiita.
“Sociolaha umenisaliti.” Ilikuwa ni sauti ya Frank mara baada ya kupokea simu
yake.
“Kwanini?”
“Si tumekubaliana leo tusiende chuoni, kwanini umeenda?”
“Mimi nipo ndiyo kwanza naamka.”
“Mmmh sasa unakuja huku kwangu au nije huko kwako?”
“Njoo huku bwana mimi ndiyo kwanza nimeamka.”
“Aya sawa.”
Baada ya dakika kadhaa Frank alikuwa amefika chumbani kwetu.
Tulicheza michezo mbalimbali, tulitekenyana, tukakimbizana humo humo
chumbani, tuliongea, tukapiga stori, tukalala, tukaamka, tulisahau hadi kula mpaka
ilipofika mchana mwingi.
Nilimuita mmoja kati ya wafanya usafi pale kwenye mabweni yetu na kumuagiza
atuletee chakula.
Tulikula humohumo ndani tukaendelea na michezo mbalimbali hakika siku hiyo
ilikuwa ya furaha sana nilisahau kurudi nyumbani.
Takribani wiki mbili zilipita bila kurejea nyumbani mawasiliano na mama
yalikuwa finyu sana.Mara nyingi kila akipiga simu wakati niko na Frank sikupokea ama ningetoa
sababu yoyote ile ya kutokupokea simu yake.
Wiki ya tatu iliingia.
Wala sikuwa nikikumbuka kurejea nyumbani siku hiyo haikuwa ya kawaida Frank
alinijia na sura ya kichovu sana asubuhi wakati akinipitia kuelekea chuoni.
Ni siku hiyo ndiyo tuliamua kwenda chuoni baada ya kupita wiki takribani mbili
mara baada ya kumaliza mtihani hatukuhudhuria tena chuoni.
Tuliwahi kufika mapema mara baada ya vipindi kuisha nilitoka nilimuacha Frank
ndani akiongea na baadhi ya watu huku nikiwahi kutoka kwenda kumsubiria nje.
La haula!
Nilikutana na mama amepaki gari lake mbele ya darasa letu huku amesimama nje
ya gari akiwa amefura.
Haikuhitaji maelezo kwamba alikuja kunifuata alikuja alisimama pale huku
akionekana ana hasira sana.
Nilisimama mwenyewe na kuelekea pale.
“Ingia kwenye gari.”
Nilifungua malango wa gari na kuweka begi langu na kisha kupanda sikupata hata
muda wa kumuaga Frank.
Safari ya kuelekea nyumbani ilianza.
“Naomba simu yako.”
Nilipojaribu kuchukua meseji nimtumie Frank mama aliniomba simu.
Nilikata haraka na kumpa simu yangu, aliichukua na kuiweka mbele kwenye
sehemu ambayo alizoea kuweka simu yake, nilijua tu mambo siyo mazuri.
Tulifika nyumbani hali niliyomkuta nayo baba iliashiria kwamba kuna kitu hakipo
sawa.
Haikuwa kawaida kuikuta familia yetu kwa namna hiyo hali hiyo iliniogopesha.
Sebuleni alikuwepo baba, Kelvin na Linah dada yetu wa kazi. Mama hakuniweka
hata niongee nao neno moja alinipitisha moja kwa moja hadi chumbani. Niliingia
chumbani alinikalisha kitandani
“Pumzika mwanangu.” Aliongea na kisha kutoka nje.
Nilishangaa, nilikaa takribani nusu saa nzima. Nikafikiria jambo.
“Ngoja nimfuate mama anipe simu yangu.” Nilinyanyuka hadi mlangoni.
Nilipojaribu kufungua mlango niligundua kwamba mlango umefungwa kwa nje na
funguo haukuwepo. Nilirudi na kukaa kitandani.
“Mama anamaanisha nini kunifungia mlango humu ndani, nikipatwa na shida je?”Niliita.
“Mama....”
Niliita watu wote waliokuwepo humo ndani kwa sauti kubwa hata nilihisi sauti
yangu inataka kukauka lakini hakuna aliyeitika wala kunifungulia mlango.
Nilijua tu mambo yamekua mabaya, nilikaa mule ndani, nilizunguka, nilisimama,
nikakaa chini, nikarudi kitandani, nikaenda kusimama dirishani, niliingia bafuni na
kutoka, nilikuwa sina cha kufanya nilihangaika hadi nilipopitiwa na usingizi.
Nilikuja kuamshwa baada ya kuhisi mlango wa chumbani kwangu umefunguliwa
giza tayari lilikuwa limeshaingia.
Waliingia Pink na Pinto nilikuwa nina uchovu mwili mzima nilinyanyuka na kisha
kukaa nikafikicha macho yangu na kuwatazama.
“Shikamoo dada.”
“Marhabaa.” Niliitikia kiuchovu.
“Mama kaseme tuje tukuulize utakula nini.”
Nilikasirika sana nilijua mama anahitaji kuniletea simu yangu kumbe anakuja
kuniambia kuhusu maswala ya chakula.
“Fyuuu...” Nilisonya mwenyewe.
“Kwani alifikiri mimi nitaishi kwa ajili ya chakula tu mwambie chochote.”
Niliongea kwa hasira.
Pink alicheka na kisha walitoka nje, nilijaribu kwenda kufungua mlango nilikuta
umefungwa tena.
Nilikaa mwenyewe takribani lisaa lizima lilipita nilitegemea usiku huu
nitafunguliwa kwa ajili ya kujumuika na familia nzima kwa ajili ya chakula cha
usiku nilichoka kuwaza na kuwazua nini kinaendelea.
“Je baba ameshamjua Frank? Je hicho ni kitu ambacho kinamchukiza? Je Melania
ameongea na mama kuhusu mahusiano yangu na Frank au kuna nini kinaendela?”
Nilishindwa kupata majibu ya haraka.
Muda ulijongea, nilikaa kitandani kwangu pasi na kitu cha kufanya na mara ghafla
niliona mlango ulizungushwa kwa ishara ya kwamba mtu anahitaji kuingia nilikaa
kitako kuja kujua ni nana alikuwa akiiingia nilipanga kumuuliza maswali yote
kwanini nimefungiwa humo ndani kuna nini.
Nilikasirika sana kuona ni Pink na Pinto wakiingia.
Waliingia wakiwa wamebeba vitu mbali mbali vilivyoonesha ni chakula cha usiku
waliviweka kitandani.
“Dada chakula.” Pink aliongea na kisha walitoka haraka haraka.“We Pink...” Niliita.
“Baba kasema tusikae huku.”
Nilishangaa.
“Kuna tatizo gani!”
Walitoka haraka haraka.
Mama alikuwa ameniandalia chakula kizuri sana ambacho bila shaka ni yeye
mwenyewe aliyekipika niliweza kutofautisha kati ya chakula cha mama na kile
kilichoandaliwa na dada yetu wa kazi Linah.
Aliniandalia chakula nikipendacho sana ndizi nyama.
Kulikuwa na sahani ya matunda pembeni pamoja na maji ya matunda ya maembe
na glasi moja ya maji.
Wala hata sikutamani kuingiza kile chakula mdomoni hata hivyo nilikumbuka
kuwa sijala kitu tangu asubuhi ilinibidi kujilazimisha huku nikiwa na mawazo
mengi.
Nilijaribu kula kile chakula ambacho kilionekana kuendelea kunishinda na ghafla
mlango ulifunguliwa tena waliingia Pink na Pinto huku wakicheka.
“Mnacheka nini?” Niliwambia.
Pink alikuwa anatembea kana kwamba anamuigizia mtu mwenye nguvu nyingi,
aliingia ndani na kisha Pinto alifunga mlango haraka haraka.
Pink alionekana kama mtu mwenye hasira sana alifura kana kwamba kuna mtu
amemuudhi nani kama mtu mwenye umuhimu mkubwa, ni sawa na bosi ambaye
amechukizwa na mfanyakazi wake.
Niliendelea kutazama vituko vyake huku nikihisi kucheka.
Alivimba huku akitanua mikono yake kuonesha kiasi gani ameshikwa na hasira.
Pinto alisimama pembeni akimuangalia huku akicheka na mimi niliungana naye
kucheka.
Ghafla Pink aliongea kitu ambacho kilinichanganya sana.
“Nikimjua nitatenganisha kichwa chake na kiwiliwili.”
“Wewe Pink unaongea nini?” Nilimuuliza ghafla.
Maneno ya Pink yalinichanganya sana.
“Baba kasema tukuletee simu yako.”
“Hebu njoo kwanza subiri nikuulize.”
“Baba kaniambia nisikae humu ndani.” Walitoka nje.
“Baba alikuwa anamzungumzia nani?” Nilishindwa kuelewa hata hivyo uwepo wa
Kelvin ulinipa mwanganza inawezekana kuwa ni mfanyabiashara mwenzieamemuudhi ninamjua baba yangu akiwa na hasira anaweza kuongea vitu vya ajabu
sana na wakati mwingine anaweza kufanya jambo la ajabu pia.
Niliendelea kujilazimisha kula huku maneno ya Pink yakizidi kunisumbua moyoni
mwangu ni nani huyu nilizidi kujiuliza maswali.
Nilikula kile chakula nilishindwa kukimaliza nikabaki nimekiangalia tu uwepo
wake pale ulianza kunikera harufu yake tayari ilishakuwa mbaya kwangu
nilitamani kuvitoa vile vyombo lakini nilikumbuka kwamba mlango umefungwa,
ningewezaje kuvitoa?
Nilinyanyuka kwa hasira huku nikizungukazunguka mule chumbani nilienda
kwenye mlango na kuufungua kwa hasira zote huku nikitoa ukelele wa ghadhabu.
La haula...!!
Mlango ulifunguka saa hizi.
“Mlango haujafungwa ngoja nijifanye napeleka vyombo.”
Nilibeba vyombo vyangu na kuvipeleka jikoni, wakati narudi nilijaribu
kuchungulia sebuleni ni akina nani wapo na kama kuna uwezekeano wa kusikia
wanachokiongea.........................
INAENDELEA....................

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search