Friday, 25 May 2018

NATAKA KUZAA -SEHEMU YA KUMI


MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
NAMBA YA SIMU: 0683777152
Baada ya kuoga pamoja nilimchukua Frank hadi bwenini, nikamshusha mbele ya
block yao na kutoka kuelekea nyumbani sikutaka kupokea simu hadi nifike.
Nilipokaribia kufika niliamua kuizima kabisa, nilipiga honi na geti lilifunguliwa
mara moja, familia nzima ilitoka na kusimama nje kana kwamba walikuwa
wakinisubiria mimi.
“Sociolah uko salama mwanangu.”
Mama aliniambia.
“Niko salama mama.”
Mwili wangu ulikuwa na uchovu sana sikutaka mama agundue hilo.
“Nenda ndani kapumzike.” Nilienda ndani.
Nilioga na kisha kulala.
Mama aliniacha nilale.
Niliamka baadae, uchovu ulikuwa umeniisha hakuna aliyeniuliza nilikuwa wapi
wala kwanini sikurudi usiku uliopita, nadhani mama alikuwa ana mashaka sana na
hali yangu huko nilipo, katika hali kama hizo mama huwa haniulizi.
Siku zilipita na hakuna aliyeuliza kuhusu mahali nilipokuwepo.
Uhusiano wangu na Frank ulizidi kustawi.
Siku moja tulikuwa tukiongea na Frank.
“Frank unajua nakupenda halafu hata sijui ni kwanini.”
“Love doesn’t ask why.” Aliniuliza.
“Unanipenda?” Nilimuuliza.
“Nakupenda lakini….” Alimalizia na viemoji vilivyokuwa vikionesha huzuni.
“Kuna nini?”
“Kuna kitu nataka nikuambie Sociolah.”
“Nini Frank niambie.”
Subiri usiwe na haraka…
“Nitakuambia tu wala usijali.”
“Ndiyo ninakusikia niambie.”
“Hiki nitakuambia siku nyingine ngoja leo nikuambiae kingine.”
Nikacheka.“Sasa ndiyo nini?”
“Ok, nikuulize kitu?”
“Hivi umejiandaaje na maisha baada ya kurudi chuoni?”
“Aanh wewe niachie mimi nitajua jinsi ya kufanya.”
“Mmmh, sawa, ila mimi ningependelea tusiwe na ukaribu kabisa watu wasije
wakahisi chochote kati yetu.”
“Frank niachie mimi najua jinsi ya kufanya, chochote kile nitakachofanya wakati
tukiwa chuoni wewe kichukulie kama ni maamuzi yangu sawa.”
“Haya.”
“Mwaka mpya tutatoka tena au vipi?”
“Wee.. Kazi ya kuomba ruhusa nyumbani unaijua ilivyo ngumu.”
“Hahaha.. Mmmh… Toroka uje.”
“Bwana.., unataka mimi nifukuzwe nyumbani, sijui lakini nikipata nafasi tutakuwa
pamoja.”
“Nilienjoy sana ile siku Sociolah natamani ijirudie tena.”
“Hata mimi pia, sijui kama nitapata hiyo nafasi.”
“Sociolah…” Niliitwa na baba.
“Nitakupigia baba kaniita.”
“Hahaha… Haya msalimie baba mkwe.”
“Wee…eenhe.”
Alicheka tu na mimi nilikacheka na kukata simu.
Niliondoka hadi sebuleni ambapo baba alikuwa akiniita.
“Haya niambie una udhuru gani?”
“Kwanini baba?” Niliongea huku nikicheka.
“Mwaka mpya tutakuwa na wageni hapa nyumbani.”
“Aaah.. Nitakuwepo baba nilijua tunaenda sehemu.”
“Kwahiyo kama tungekuwa tunaenda sehemu inamaanisha usingeenda.”
“Hapana baba nilikuambia kwamba udhuru hautojitokeza tena, nitakuwepo na
wala tungekuwa tunaenda popote pale tungekwenda.”
“Sawa binti yangu, jiandae tu kwa ajili ya kupokea wageni.”
“Sawa.”
Siku zilijongea na hatimaye sikukuu ya mwaka mpya ilifika.
Nilipewa kazi ya kufanya usafi nyumbani kuhakikisha mazingira yote yako safi na
ya kupendeza kwa ajili ya wageni ambao waliotarajia kufika hapo mchana.Binafsi nilikuwa napenda sana swala la usafi na nadhani ndiyo sababu kubwa
iliyomfunya mama akanipa hiyo shughuli.
Mama na dada Linah waliingia jikoni wakati baba alikuwa amekaa nje barazani
alisoma magazeti.
Nilifanya kazi zangu pole pole kwa kuwa sikuwa na haraka yoyote, nilisafisha
mazingira ya nje, nikasafisha ndani na kisha nikaanza kupamba sebuleni kwetu
kwa ajili ya wageni nikitayarisha vitu mbalimbali ambavyo vingetumika na wageni
katika siku hiyo.
“Nyie nini?” Nilimsikia mama akiongea, nilijua tayari wakina Pink tayari
wameshafanya mambo.
“Hawa watoto bwana wajinga kweli.” Niliongea
“Nini…? Kuna nini?” Mama alikuwa akionge.
“Ona… Ona… Sikia huyu hapa mbishi.” Pink aliongea.
“Kafanyeje?” Mama alimjibu.
Sikusikia sauti zao tena ingawa nilivutiwa sana na mazungumzo yao nilikuwa
nakitaka kujua wamefanya kitiu gani.
Niliendelea na shughuli zangu, wakati huo nilisogea chumba cha maakuli kwa ajili
ya kupanga vyombo ambavyo vingetumika kwa ajili ya maakuli siku hiyo, hapo
niliweza kusikia kilichokuwa kikiongeleka kule jikoni.
“Huyu anabisha kwenye hii simu ya dada Sociolah huyu siyo Matranka.”
“Mungu wangu! Wamepataje simu yangu hawa?!”
“Siyo yeye.”
“Muangalie vizuri, wewe si unamkumbuka?”
Sikusikia mama akiongea chochote.
Nilisogea hadi kwenye mlango wa kuingilia jikoni na kisha kuchungulia kwakuwa
ulikuwa wazi kidogo, mama alichukua simu na kisha kuangalia, kama alikuwa
akivuta fikra.
“Anafanana naye.”
“Ni yeye mama.”
“Ni yeye, Pinto mbishi kweli.”
“Halafu huyu hapa ndiyo alikuwa anaongea….” Nikaingia ghafla.
“Kuna nini kwenye simu yangu?”
Mama alikata haraka na kisha akanipa.
“Sijui hawa watoto walikuwa wanachezea simu yako.” Aliongea mama na kisha
kugeukia upande mwingine na kuendelea na shughuli zake.“Wewe Pink mara ngapi nimekuambia kuhusu swala la kuchezea simu yangu
kwanini hunisikii.”
“Pinto huyo ndiyo mbishi, mimi nilimuambia huyo Matranka anabisha ndiyo
nikaja kumuuliza mama.”
Nilishindwa cha kuongea, nilitoka nje haraka na kuelekea chumbani kwangu na
kisha kujifungia. Baada ya muda mama aliingia chumbani kwangu, alinikuta kama
niliyechanganyikiwa.
“Sociolah nini mwanangu?”
“Hamna kitu mama.”
“Najua kuwa hamna kitu lakini kwanini hali yako imebadilika ghafla.”
“Mama mimi sipendi jinsi wakina Pink wanavyowadharau watu, kwani Matranka
ana nini na akiwepo kwenye simu yangu kuna nini si ni mwanafunzi mwenzangu
na pia haitwi Matranka anaitwa Frank, kwanini lakini anakuwa hivi na wewe kama
mama badala ya kuzuia unawasapoti watoto.”
“Sasa mwanangu mimi nifanyeje wewe umeacha simu yako bila kuweka password
na watoto wameifikia wanaichezea, sasa mimi nifanyeje.”
“Hata kama mama lazima kuwakemea.”
“Sijui tu kwanini unamtetea huyo Frank.”
“Hapana mama naweza kumtetea mtu mwingine yoyote.”
“Sijawahi kukuona katika hali hii Sociolah, mimi ni mama yako.” Mama
aliniambia.
Niliamua kunyamaza na kugeukia upande mwingine.
Sikutaka tena kuendelea kukaa sebuleni.
Wageni walifika hata sikutoka kuwasalimia nadhani waliniulizia maana muda
kidogo Pink aliingia chumbani kwangu kuniita.
“Wewe dada unaitwa na baba mdogo, kasema hajakuona siku nyingi kakumisi.”
“Nakuja.” Alitaka kutoka nikamuita.
“Wewe Pink njoo, ulikuwa unatafuta nini kwenye simu yangu.”
“Si nilikuambia, Pinto alikua anabisha yule siyo yule mkaka tuliyemkuta na
matranka siku tuliyokuja mara ya kwanza chuoni kwenu.”
“Kwahiyo kama ndiyo yeye ndiyo inakuaje.”
“Huyo Matranka…...”
“Siyo Matranka, Frank.”
“Matranka.”
Pink alinibishia, nilishikwa na hasira kiasi cha kutaka kumpiga kofi.“Matranka, mimi namjua Matranka majina mengine siyajui.” Aliongea.
Nilivuta hasira zangu, nilitamani kukitafuna kiumbe kile lakini nilishindwa.
“Ok nenda ila usiseme chochote kama nimekuuliza.”
“Kwani dada amefuata nini kwenye simu yako au na wewe unataka matranka?”
“Ndiyo nataka tranka niwekee nguo zangu.”
Pink alicheka kicheko cha kimbea na kisha kugonga mikono yake.
“Halooo…aya.. Sawa.”
Alitoka nje huku akicheka, nilisikitika tu......................
INAENDELEA...................

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search