Wednesday, 16 May 2018

NATAKA KUZAA -SEHEMU YA NANE


MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
NAMBA YA SIMU: 0683777152
Nilitembea hatua za kivivu hadi getini mama yangu alikuwa amesimama getini
akinisubiri, alinipokea mkoba wangu.
“Ulikuwa salama mwanangu.” Aliniuliza.
“Ndiyo mama.”
Tulienda mpaka kwenye gari, alinifungulia mlango wa gari nikaingia ndani na
kisha akaingia kwenye siti ya dereva na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.
Mahusiano yetu yalizidi kustawi tulikuwa tukitumiana jumbe fupi mara kwa mara
huku tukiongea mambo mbalimbali, Frank alikuwa ni mcheshi sana na nilifurahia
nyakati zote tulizokuwa pamoja tulikuwa tukiongea kuhusu maswala mbalimbali
na alikuwa akinichekesha sana, nilipenda sana kuwa karibu naye.
Siku moja kabla ya siku kuu ya krismasi nyakati za jioni nilikuwa nikiongea na
Frank.
“Frank naomba tutoke kesho.”
“Tunaenda wapi Sociolah.”
“It will be a surprise.” Nilimuambia.
“Unataka nikakutie aibu huko unakoenda.”
Nilicheka “Hahahah….. Kwanini?”
“Sociolah mimi na wewe tunaendana kweli?”
“Haaa.. Usijali kuhusu hilo wewe sema kama uko tayari.”
“Mimi niko tayari, lakini….”
“Usiseme lakini kama umekubali kubali tu.”
“Sawa niko tayari.”
“Vizuri.”
“Lakini mimi sina nguo ya kuvaa Sociolah nitakutia aibu.”“Aisee ukikubali sema umekubali usitoe lakini sawa, vyovyote vile utakavyo vaa
mimi sitakuwa na shida navyo.”
“Aaah wewe unasema tu wewe ngojea hiyo kesho wewe mwenyewe utajuta.”
“Hahahah kwanini?”
“Sociolah….” Sauti ya baba ikitokea ndani iliniita.
“Frank I will call you later.” Nilimwambia. Nilikata simu na kisha kuelekea ndani.
“Yes dad.”
“Kesho tutaenda kusherekea sikukuu ya krismasi kwa baba yako mkubwa
Oysterbay.”
“Noo dad.” Niliongea.
“Nini… Kuna nini?”
“Baba mimi siwezi kwenda Oysterbay.”
“Kwanini…? Utaenda.” Aliongea baba na kisha kuondoka.
“Baba….. Baba….” Niliita hakugeuka, nilibaki nimekaa tu, machozi yalianza
kunitoka na kisha kilio cha chini chini kilianza kusikika.
“Sociolah …. Sociolah una nini mwanangu, unalia nini? Kuna tatizo? Baba
amekupiga?”
“Mama mimi nilikuwa na udhuru kwamba kesho sitaenda Oyster boy.”
“Kwanini Sociolah hujui familia nzima tunatakiwa tuwepo.”
“Hapana mama nilitamani niwepo lakini nina sehemu ninataka kwenda.”
“Sehemu gani? Huwezi ukaahirisha ukaenda siku nyingine Sociolah huoni
umuhimu wa siku ya kesho kuwepo kule.”
“Mama kuna sherehe ya rafiki yangu na mimi ndiyo namsimamia.” Ilinibidi
kudanganya.
“Baba yako amesemaje?”
“Baba hajataka hata kunisikiliza ameondoka tu.”
“Ngoja nitajaribu kuongea naye halafu nitakuja kukwambia.”
Nilitoa tabasamu la ushindi nilijua tu hakuna kitakachoharibika, baba huwa
hasumbui mbele ya mama anampenda sana.
Nilifurahia na kisha kuelekea chumani kwangu, nilibeba wallet yangu na kisha
kuelekea Mlimani City. Nilichukua bajaji ambayo ilinifikisha kwa haraka Mlimani
City.
Nilimchagulia Fank nguo nzuri ambazo nilihisi ni saizi yake na zingeweza
kumtosha nilimchagulia Suruali nyeusi nzuri, shati la mikono mirefu la rangi yaMaruni, tai nyeusi na kiatu kizuri sana cheusi niliamini vingempendeza sana
nikamnunulia na vest pamoja na marashi na boxer nzuri nikavifunga vizuri na
kisha kuelekea nyumbani.
Nilipofika chumbani kwangu mama alikuja.
“Eenh umetuletea zawadi gani?”
“Aanh hamna mama hizi ni zawadi kwa ajili ya sherehe ya kesho.”
“Aanh sawa baba yako amekuruhusu uende ila amesikitika sana kwamba
hutokuwepo kule.”
“Mama hata mimi pia nilitamani kuwepo lakini ndiyo hivyo tu mama naomba
umuambia baba anisamehe siku nyingine haitotokea tena nilimuambia mama.”
“Sawa.”
Mama aliondoka alipoondoka tu Pink aliingia chumbani kwangu.
“Wewe kwanini umeingia chumbani kwangu bila hodi ukinikuta sijavaa?”
“Si umeingia sasa hivi hujavaa hujavaa nini.” Pink aliongea, nilicheka tu kwa
maana alikuwa ni mkorofi na mwenye maneno mengi sana kuliko pacha wake
Pinto. Pinto alikuwa mpole tu ila alikuwa mtundu na mara nyingi sana akiwa na
Pink basi hapo mambo lazima yaharibike, mara nyingi sikupenda kuongozana nao
hao wote wawili kwa maana lazima tukio litokee.
“Aya niambie umefuata nini?”
“Wewe dada nilikusikia unasema kesho utatoka out na mtu kwenye simu.”
aliniambia.
“Keleleee…, Nyau wewe.”
“Aaah mama amekataza kuniita nyau.” Pink alisema.
“Toka chumbani kwangu.”
Mama aliita kwa sauti kutokea jikoni. “Kuna nini..?”
“Mama dada Sociolah ananiita….” Nikamziba mdomo haraka.
“Kelele.. Usimuambie mama chochote hata usimuambie kama umenisikia
nikiongea kwenye simu umesikia.”
“Nipe hela.” Alisema, sikuwa na jinsi. Pink kwa ninavyomjua angeenda kusema.
Nilitoa noti ya elfu kumi na kumpa.
“Usiseme sawa.” Alitoka chumbani kwangu. Mama aliongea.
“Kuna nini?”
“Hamna Pink alikuwa ananisumbua sumbua kidogo.”“Huyu Pink naye bwana.” Mama alitoka na kisha kuendelea na shughuli zake.
Siku hiyo usiku huo tulielekea kanisani kwa ajili ya mkesha wa sherehe za
krismasi tulisali na baada ya hapo ilipofika saa sita kamili nilitoka kanisani na
kumpigia simu Frank
“Marry Christmas.”
“Oooh thank you, niko kanisani hapa nimetoka nje mara moja tu na simu yako
imeingia.”
“Kanisa gani umeenda?”
“Aanh niko tu kwenye jumuiya ya hapa hapa Mabibo kuna baadhi ya watu wapo
hapa tumekutana.”
“Aanh ibada ilikuwaje iko?”
“Vizuri tu nimefurahia na wewe uko wapi?” Frank aliniuliza.
“Niko kanisani nimetoka mara moja, hata hivyo ibada imeisha tunaelekea
nyumbani.”
“Ok Sociolah uwe na usiku mwema, ahsante sana.”
“Ahsante pia.” Nilikata simu.
Safari ya kuelekea nyumbani ilianza njia nzima niliwaza siku ya kesho, sijui
itakuwaje, nitafurahi sana kuwa karibu yake.
Tulitoka.
Usiku huo ulipita.
Asubuhi, mama, baba, Pink, Pinto na dada wa kazi Linah walijiandaa na kisha
kuondoka.
“Unaweza kutumia hiyo gari nyingine.” Baba alisema.
Waliondoka na kisha kuniacha peke yangu nilioga huku nikiimba nyimbo
mbalimbali, nilizunguka zunguka nikatafuta chai nikanywa.
Nilipanga mtoko wetu uanze saa nane za mchana hivyo nilijizungusha zungusha
hapo nyumbani muda ulipowadia niliaandaa vitu vyangu, niliandaa gauni zuri sana
lenye kitambaa chepesi ya rangi ya Maruni nilinunua katika moja ya maduka ya
Mlimani City lilikuwa ni gauni zuri sana nilivaa gauni hilo na kiatu kirefu sana cha
rangi nyeusi, nilijipulizia marashi mazuri ya kike na shingoni nikavaa cheni
niliyopewa zawadi na mama yangu ambayo ilikuwa imenakishiwa kwa dhahabu.
Nilitoka na kuelekea mabweni ya Mabibo nilielekea moja kwa moja hadi
chumbani kwa Frank, nilimkuta Frank amevaa fulana kubwa kubwa nyeusi yenye
maandishi meupe ambayo sikujishughulisha hata kuyasoma, alikuwa amevaa nasuruali ya kitambaa ambayo haikufika vizuri kwenye vifundo vya miguu kwa
kweli nilishindwa kujizuia ilibidi kucheka.
“Unacheka nini sasa?” Aliongea kwa sauti yake nzuri ya kiume.
“Sasa ndiyo umevaa nini?”
“Mimi si nilikwambia.”
“Kwahiyo hapo ndiyo umeshajiandaa kwa ajili ya mtoko?” Niliongea huku
nikicheka.
“Eenh hapa bado kuweka viatu tu alivuta viatu vyake raba nyeupe, nilicheka
nikamrushia ule mfuko.
“Vaa hivyo.”
Alifungua.
“Woow nguo nzuri hivyo umepata wapi?”
“Punguza maswali bwana Frank vaa tuondoke muda unaenda.” Niliongea,
alitabasamu tu.
Alijizungusha mara mbili mule chumbani kisha akanijia.
“Sociolah unaweza kunipisha nivae.” Nilicheka.
“Unaniogopa au unanionea aibu mimi?”
“Nina aibu.” Aliongea huku akiinama.
“Vaa tu wala hamna shida.” Alivua nguo mbele yangu na kisha kuvaa, hakika
alipendeza sana zaidi ya sana.
Nilitoa yale marashi niliyomnunulia na kisha nikampulizia.
“Aah.. Sociolah ndiyo nini hivyo.” Nilicheka.
“Si ili unukie vizuri.”
“Aisee kweli nimekuwa nanukia kama maua fulani hivi.”
Nilicheka tu.
Alipendeza sana zaidi ya sana, mtu yoyote ambaye angemuona angehisi ni
mvulana mtanashati kutoka kwenye familia tajiri. Hata hivyo nywele zake
hazikuniridhisha tulitoka bwenini, nadhani watu walishindwa kumtambua kama ni
Franklin yule aliyekuja na tranka chuoni.
Tulipofika nje nilitafuta saluni nzuri ya kiume, tuliingia humo akatengenezwa
nywele zake ambazo zilipunguzwa kwa mtindo mzuri, zilipakwa mafuta na
kung’aa. Alipunguza nywele za pembeni na kisha nywele za kati kati ziliachwa
kwa wingi hakika alipendeza sana, baada ya hapo alifanyiwa Scrub alionekanakuwa kamili, Frank alikuwa amependeza, niliona Frank ni mwanaume mzuri
kuliko wote ambao nimekutana nao kila mtu aliyetuona nahisi alitutamania.
Tuliondoka na kuelekea Blue pearl Hotel pale Ubungo. Tulipofika tulichagua
sehemu nzuri iliyokuwa pweke ingawa siku hiyo ya sikukuu watu walikuwepo hata
hivyo tulikuwa tumejitenga na watu.............

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search