Wednesday, 16 May 2018

NATAKA KUZAA SEHEMU YA SABA

MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
NAMBA YA SIMU: 0683777152
“Naomba tu usirejee nyumbani maana huku njiani hapafai ni maafuriko kila kona
kuna magari yamesombwa hapo na abiria, ningeweza kuja kukufuata mwanangu
lakini nahofia usala wako na wangu pia, kama uko salama endelea kukaa mvua
itakapoisha nitakuja mwenyewe kukuchukua mwanangu, sawa.” Mama aliongea
na kisha simu ikakata ghafla, simu ya Frank nayo ilikuwa imezima chaji.
“Oooh…” Nilivuta pumzi na kuzishusha.
Baridi ilianza kuwa kali ilinilazimu kupanda kitandani kabisa, nilivua viatu vyangu
na kisha nikasogea hadi mwisho wa kitanda.
Frank naye alianza kutetemeka nilimuonea huruma.
“Frank…” Nilimuita, alinigeukia.
“Unahisi baridi?”
“Hapana, kawaida tu.” Alijinyoosha kuonesha kuwa yuko kawaida ingawa
nilimuona kabisa alikuwa akiteswa na baridi ile.
Radi ziliendelea kupiga nilizidi kupiga kelele.
“Sasa Socialah kelele za nini?”
“Wewe huoni radi zinapiga?”
“Kwahiyo ukipiga kelele ndiyo radi zinaacha?” Niliamua kunyamaza tu kimya.
Giza lilizidi kuwa zito mule ndani.“Frank giza linazidi.”
Alinyanyuka bila kuongea chochote, alienda kufungua kabati lake na kisha kutoa
kompyuta yake ndogo, alikuja na kuiweka pale kitandani, aliiwasha na kisha
kuweka filamu ya kiamerika.
Filamu hiyo ilikuwa ikiitwa “Perfect Match.”
Kwa kiasi Fulani mwanga wa kompyuta ile ulileta mwangaza mule ndani.
“Sogea huko.” Aliniambia.
Nilisogea na kisha akaja kukaa pembeni yangu, nilimuonea huruma jinsi
alivyokuwa akitetemeka.
“Chukua blanketi.” Nilimuambia.
“Hapana, usijali niko salama.” Aliongea.
Muda ulizidi kwenda filamu ilikuwa nzuri sana ambayo ilinifanya muda mwingine
niachie kicheko cha nguvu, alikuwa akinitazama tu.
Muda ulizidi kwenda nilianza kuhisi kuchoka, usingizi ulianza kunivamia kwa kasi.
Nilishindwa kuendelea kujizuia, nilijikuta nimedondokea begani kwake na kisha
nikadondokea moja kwa moja kwenye mapaja yake.
Miale ya jua isiyo na nguvu iliniamsha kutoka usingizini, kabla sijafungua mboni
za macho yangu niliachia tabasamu ambalo ni kwa nadra sana kuonekana usoni
kwangu. Niliendelea kutabasamu hali ya kumbukumbu ya kilichotokea usiku
uliopita ikipita katika akili yangu.
USIKU ULIOPITA
Usingizi mwingi ulinielemea, nadondokea begani mwa Frank na mwishowe
ninadondokea mapajani kwake. Sijui ni nini lakini nahisi ni nguvu ya asili kati ya
mwanamke na mwanaume.
Frank alisogeza kompyuta, akaiweka juu ya meza na kunisogeza vizuri ili nilale
vizuri. Wakati huo niliweza kufumbua macho yangu, nilikuwa nikimtazama
Franklin kwa ukaribu zaidi. Hakika alionekana ni kiumbe kipya mbele yangu.
Franklin uzuri wake ulizidi mara elfu ya jinsi alivyo, macho yake makubwa, pua
yake ndogo iliyopamba vyema uso wake pamoja na lipsi zake pana ambazo muda
wote zilionekana kung’aa lakini kutokana na matunzo hafifu mara nyingi ulikuwa
ukipauka.
Usiku huo uling’aa mithili ya Tanzanite.
Alikuwa na nyusi nyingi zilizojaza vyema juu ya macho yake, rangi yake nyeupe
ya kuvutia ilizidi kumpamba, alikuwa na nywele nyingi nyeusi ambazo hakuzinyoakatika mitindo ya ajabu, nywele zake zilikuwa zimenyolewa kwa msawazo na
wakati huo zilikuwa zimekuwa kidogo, ziliongeza haiba yake vizuri.
Bila kutaraji nilijikuta nimemshika shingoni tulitazamana kwa muda hakuna
aliyeweza kuongea lolote niliweza kuzihisi pumzi zake na bila shaka na yeye
aliweza kuzihisi za kwangu.
Nilishindwa tena kuendelea kumtazama nilimvutia kwangu na yeye alikuja kama
aliyekuwa akisubiri kuanzwa.
Frank aliufanya usiku wangu uwe ni wa kukumbukwa ingawa alionekana
mshamba lakini alikuwa mjuvi.
“You are awesome.” Niliongea kwa sauti ya kukata kata pale tulipofika mwisho.
“Thanks.” Aliongea.
Nilijihisi nimekamatika kwenye mikono yake. Na kama ni kuzama penzini basi
kwa wakati huo nilikuwa nimezama kabisa.
Sikujali kelele alizokuwa anapigiwa Franklin, sikujali dharau zote wala sikujali
nini ambacho kimetokea kabla ya wakati huo. Sikujali watu wangenichukuliaje
wala sikujali maisha baada ya hapo na pia sikujali muonekano wa Franklin
nilichokuwa nikikifahamu kwa wakati huo ni kwamba ninampenda Franklin
ingawa nilishindwa kumwambia.
Baada ya safari hiyo Franklin alinibusu kwenye papi za midomo yangu na kisha
akanibusu kwenye paji langu la uso na kunilaza kifuani kwake na hapo ndipo
nilipoamkia asubuhi iliyofuata.
Baada ya kumbukumbu hiyo kupita kwenye akili yangu hatimaye nilifumbua
macho. Nilimsawili mwili wake uliojengeka vyema nadhani ni kutokana na
shughuli za hapa na pale.
Franklin hakuwa na mwili wenye manyama uzembe kama ilivyokuwa kwa Patrick,
alikuwa na mwili uliojengenga vyema ambao vijana wa saa hizi wamezoea kuita
wa “Six pack.”
Alikuwa haishi hamu kumtazama tofauti na vile alivyokuwa akionekana katika
mavazi yake ya ajabu ajabu. Franklin alikuwa ni aina ya wanaume ambao
wangeweza kusumbua mjini kama tu angejali muonekano wake.
Baada ya kuridhika na utalii wangu katika mwili wa Franklin niligeuka na
kumtazama machoni hali nimelala kifuani kwake.Alionekana kama mtu mwenye dalili za kutoka usingizini na mara si mara
alifumbua macho nilikwepesha macho yangu na kuyafumba kwa kuwa sikutaka
ajue kwamba niliwahi kuamka.
Alinibusu kwenye paji la uso.
“Nimekuona.” Akaniambia nilishindwa kujizuia nikacheka na kisha nikafumbua
macho.
“Umenionaje?” Niliuliza kwa aibu za kike.
“Nimekuona usingizini.” Nilicheka.
“Usiku wako ulikuwaje?” Nilimuuliza.
“Best.” Alijibu.
“Wa kwako je?” Aliniongeza na swali jingine.”
“Awesome.”
“Well, umeamka poa mama?” Aliongea kwa sauti nzito ya kiume.
“Ndio.” Nilijibu na kisha nikaachia tabasamu la mwaka.
Alinibusu tena kwenye paji la uso na kisha alinyanyuka kutoka kitandani.
Franklin alikuwa amevaa boksa chakavu nilimtazama alivyokuwa akitembea kana
kwamba ni mfalme aliyekuwa akiingia katika hekalu lake, alitembea kwa hatua za
pole pole hadi kwenye kabati lake, alifungua na alitumia dakika kadhaa hapo kabla
ya kuondoka na kurudi tena kitandani.
Sikuwa najua haswa ni nini alienda kufanya, alirudi akakaa pembeni yangu.
Wakati huo nilikuwa na nguo ya ndani pekee na shuka lililonistiri, nilikuwa
nimelishikilia kifuani kwangu nikiwa nimekaa pembezoni mwa kitanda. Alikuja na
kuniangalia akaachia tabasamu nikatabasamu pia. Akanyanyuka na kisha
akaelekea mahali ambapo zilikuwa zimetundikwa nguo kadhaa. Alichukua bukta
akavaa iliyoonyesha miguu yake mizuri iliyojaa vyema kisha akachukua na shati
ambalo lilikuwa na mikono mifupi akavaa, alitoka na ndoo mbili za maji.
“Frank….” Nilimuita
“Yes.” Aligeuka.
Nilichukua tshirt kubwa kubwa lililokuwa katika nguo zilizokuwa zimetundikwa
mahali hapo nikampelekea.
“Vaa ili.” Alicheka tu, akachukua akalivaa na kisha akatoka nje.
Nilirudi na kukaa pale nilipokuwa nimekaa nikitabasamu tu bila mpangilio wala
sababu ya msingi.
Dakika kama tano zilipita Frank aliingia, alikuwa amebeba ndoo mbili zenye maji.“Sociolah hamna watu huku kwahiyo ungeenda kuoga, nitakupeleka.”
“Lakini sina mswaki wa ziada.”
“Sijui unaweza kusubiri niende kufuata kule nje.”
Niliachia lile shuka lililokuwa likinistiri na kunyanyuka.
Frank alitoa macho kana kwamba hakutarajia kuniona mimi katika hali ya utupu,
hilo nililitarajia. Nilipiga hatua za kiuvivu nikijongea upande wake, nilimkaribia na
kusimama karibu yake kana kwamba aliyekuwa akinisubiri, Frank alinipokea kwa
mikono miwili alinivuta karibu yake nikiwa na nguo ya ndani pekee.
Alinishika kiuno mikono yake ya kiume ilikamata kiuno changu sawia nilihisi
kutetereka.
“Frank…..” Niliita kwa sauti iliyopwaya.
“Nitaoga, nitapiga mswaki nikifika nyumbani usijali.” Hakunijibu.
Alinivuta na kisha tukapeana busu refu bila kujali hatukuwa tumeswaki asubuhi
hiyo, lilikuwa zuri sana sikutamani aniachie lakini busu lile lilidumu kwa sekunde
chache tu na kisha Frank aliniachia.
“Sociolah, umeme umesharudi weka simu chaji uwasiliane na mama.”
Kama alinizindua usingizini, niliondoka na kisha nikalifuata shuka langu,
nikalichukua na kisha kujistiri. Nikachomoa chaja kutoka kwenye pochi yangu na
kisha nikachomeka simu yangu chaji.
Baada ya kuanza kuingiza chaji nilitafuta nguo zangu, nikavaa na baada ya hapo
nilisogea pale ilipo simu yangu ilikuwa ikipeleka chaji kwa haraka sana niliamua
kuiwasha hivyohivyo. Nilipoiwasha tu meseji kadhaa ziliingia kulikuwa na kiasi
kama meseji kumi na tano wakati meseji tisa zote zilikuwa ni za mama,
sikujishughulisha kusoma. Nikaingia kwenye orodha ya majina na kulitafuta jina la
mama. Kabla sijabonyeza simu iliita alikuwa ni mama nilipokea harakaharaka.
“Hello Sociolah, uko wapi? Mwanangu nimeshafika hapa Mabibo.” Aliongea kwa
haraka.
Nilishikwa na kigugumizi nikashindwa cha kuongea, nikamtazama Frank alikuwa
amesimama pembeni yangu.
“Uko sehemu gani?” Nilimuuliza.
“Niko hapa nje getini.” Mama alisema.
“Ok, nipe dakika tano mama nakuja.”
“Sawa nakusubiri mwanangu.” Aliongea na kukata.
Niligeuka na kumtazama Frank.
“Nasikia mama yako ni mhadhiri wa pale UDSM.” Frank aliuliza.
“Yes.”
“Hongera.” Alisema.
Nilikusanya kila kitu changu na kisha nikasimama, nikamsogelea Franklin
alinibusu kwenye paji la uso.
“Bye.” Alinambia, nilitabasamu.
“Tutawasiliana.” Nikaongea
“Nikusindikize?” Aliniuliza wakati nilipofika mlangoni.
“Hapana usijali.” Niliongea kwa upole nikaachia na tabasamu kali na kisha
nikatoka.
Nilitembea hatua za kivivu hadi getini mama yangu alikuwa amesimama getini
akinisubiri, alinipokea mkoba wangu........

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search