Friday, 25 May 2018

NATAKA KUZAA -SEHEMU YA TISA


MTUNZI: JENNIFER ALPHONCE
NAMBA YA SIMU: 0683777152
Tuliondoka na kuelekea Blue pearl Hotel pale Ubungo. Tulipofika tulichagua
sehemu nzuri iliyokuwa pweke ingawa siku hiyo ya sikukuu watu walikuwepo hata
hivyo tulikuwa tumejitenga na watu.
Tuliagiza vyakula kadri tulivyoweza ingawa Frank alionekana mshamba mshamba
kwani tulipofika tu aliagiza pilau nyama nilicheka.
“Tuletee mbuzi choma na ndizi.” Nilisema.
“Aaah!!” Aliachia tu mdomo, nilicheka.
“Frank unatumia wine?”
“Aaah hapana wee…” Aliongea nilicheka. Muhudumu alishindwa kujizuia ilibidi
na yeye acheke.
“Mimi niletee tu pepsi.” Alisema, nilicheka.
“Ok, mimi naomba uniletee dompo.”
“Dompo!! Hiyo soda mbona sijawahi kuisikia.”
Nilisema “Frank shiiii….”
Muhudumu alicheka, nilimuambia
“Ok nenda tukikuhitaji tena tutakuita.” Aliondoka.
Tulikula, tulikunywa hadi jioni ilipofika. Giza lilianza kuingia.
Nilikuwa nikimshawishi sana Frank kunywa dompo.
“Nipe nionje kidogo.”
Alikunywa.
“Mmmh chungu ila tamu.”
Nilicheka.
“Kunywa bwana.”
“Kwani imetengenezwa na nini?”
“Acha maswali maswali bwana wewe kunywa.”
“Sasa si najua tu lakini Sociolah.”
“Kunywa bwana aanh, ayo maswali mengine kamuulize mhadhiri.”
Alicheka, aliendelea kunywa. Haukipita muda alianza safari za kwenda chooni kila
muda, niliishia tu kucheka.
“Sociolah mimi nahisi usingizi.”
“Usingizi…!!” Hebu jikaze turudi bwenini.”
“Siwezi Sociolah nahisi usingizi sana.” Alianza kulalia meza.“Mmh…” Niliguna.
“Muhudumu….” Nilimuita muhudumu aliyepita karibu yangu.
“Naomba utuchukulie chumba.”
Nilichukua chumba kwa ajili yetu na kisha nilimuomba muhudumu anisaidie
kumkokota Frank hadi chumbani kwetu.
Tulifika chumbani Frank alijilaza kitandani, alifumbua macho na kuachia
tabasamu.
“Frank.” Nilimuita.
“Vipi?” Aliongea kwa sauti iliyoonesha kilevi.
“Unajisikiaje?”
“Niko fresh tu.”
Alinyanyuka na kusimama.
“Aaanh Frank siyo wewe uliyekuwa umelewa?”
“Nilikuwa tu nina usingizi mimi sijalewa.”
“Oh God, sitaki kuamini, nini hasa lengo lako?”
“Kulala.”
Macho yangu yalikuwa kama yakiishiwa nuru, nilimtazama Frank katika macho
yaliyokuwa yakisinzia.
“Frank.” Nilimuita, hakunijibu badala yake alianza kupiga hatua za polepole
akisogea upande wangu, nilirudi nyuma hatua moja kumzuia asifike.
“Frank.” Nilimuita lakini hakuitikia ,alizidi kusogea na mimi nilizidi kurudi hadi
nilipogota ukutani
“Frank.” Alizidi kuja upande wangu.
Nilinyoosha mikono yangu kumzuia.
“Frank.”
Aliidaka mikono yangu na kisha kuibabatiza ukutani na kisha alisogeza midomo
yake karibu na ya kwangu.
Lilifuatiwa na busu refu lililodumu kwa dakika chache na kisha aliniachia.
“Sociolah.” Aliniita.
Nilishindwa kujibu wala kunyanyua uso wangu.
“Say something.” Aliniambia.
“Nakupenda.” Nilijibu kwa sauti ya pole pole.
Alinifuata akaninyanyua na kisha kunitupia kitandani, alivua nguo zake na kisha
kunifuata pale kitandani nilihisi aibu sana hata hivyo nilifurahia kitendo kile
kilichokuwa kikitendeka pale.Frank alinipa kile ambacho nilikuwa nikistahili kukipata, hakika ulikuwa usiku wa
kukumbukwa sana.
Tulipomaliza kufanya kile kilichotokana na asili ya maumbile nilijilaza kifuani
kwake.
“Frank… Nakupenda.”
“Sociolah.” Aliniita.
“Yes.”
“Ooh… Basi.” Alinyamaza.
“Nakupenda pia.” Alijibu.
“Frank kuna kitu ulikuwa unataka kuniambia ni nini?”
“Hamna kitu mama.”
“Bwana niambie.”
“Sogea huku nikuambie.”
Nilitoka kifuani kwake na kisha kulala pembeni yake.
“Aanh nilitaka kukuambia…..”
Alinivuta na kisha ndimi zetu zikakutana, baada ya busu hilo refu aliniachia.
“Mmmh…” Nilishindwa hata cha kuongea.
“Umefurahi.” Nilicheka tu, nikampiga kofi dogo shavuni.
Na kisha usiku ule ulipita, wala sikukumbuka kurejea nyumbani usiku huo.
Nilikuja kuamka ilikuwa asubuhi siku iliyofuata saa nne, niliamshwa na mlio wa
simu.
Frank alikuwa bado amelala niliamka na kuvuta simu yangu ambayo ilikatika
muda huo huo. Ilikuwa ni simu kutoka kwa mama nilishituka.
“Kumbe sikurejea nyumbani usiku uliopita mbona mama atanitafuna, nitaenda
kumuambia nini?”
Kuhamaki nilikuta simu zisizopokelewa 52 na meseji 72 na zote zilikuwa za mama
“Mungu wangu…. Mungu wangu…..”
“Frank…. Frank….” Niliita.
“Mmmh” Aliitikia tu kwa kukoroma.
“Niache nilale Sociolah nina usingizi.”
“Saa nne saa hizi.” Aligutuka.
“Sasa usiku huu unataka uende wapi?”
“Siyo saa nne ya usiku Frank ni saa nne asubuhu, Frank be serious…” Niliongea.Alishituka na kisha akanigeukia, alinitazama kana kwamba anaona
mwandawazimu na kisha aligeuka pembeni na kuvuta simu yake na kuangalia
muda.
“Aanh! Saa nne asubuhi!” Alibaki tu ameshangaa.
“Frank ona.” Nilimuonesha simu zisizopokelewa kutoka kwa mama pamoja na
meseji zake.
“Ooh God! Aisee wewe Sociolah unapendwa, simu zote hizo na meseji kibao
kutoka kwa mama yako, yani ningekuwa mimi nisingepata hata meseji.”
Ilinibidi kucheka maana nilishindwa kujizuia na kisha nikamchapa kofi dogo
shavuni.
“Frank hivi unafikiria is it fan…. Naenda kumuambia nini mama?!”
“Aaah sory.” Aliongea huku akiinama chini.
Nilisikitika.
“Nifundishe cha kwenda kuongea nyumbani basi.”
“Sociolah…” Aliniita.
“Eee..” Niligeuka na kumtazama, kila mara macho yetu yalipogongana nilihisi
macho yangu yakipotelewa na nuru.
Kana kwamba alikuwa akitaka kuongea kitu halafu ghafla akaghairi tulibaki tu
tukitazamana.
Sikuwa na kitu chochote mwilini mwangu zaidi ya shuka lililokuwa limenistiri,
alisogeza mkono wake hadi kwenye mapaja yangu, nilifumba macho.
Mkono wake mwingine ulitua moja kwa moja tumboni kwangu na kuanza kutalii
maeneo mbalimbali.
Sikuweza kuzuia kitu chochote na hatimaye tulifanya tena kitendo kile.
Tulipomaliza nikiwa kifuani kwake.
“Frank, niambie basi nikamwambie nini mama.”
“Kwani uliagaje?”
“Nilimuambia naenda kwenye party.”
“Muambie party ilichelewa kuisha ikabidi ulale huko huko kwasababu uliona
ingekuwa siyo vizuri kurudi usiku nyumbani.”
“Mmh sijui atanielewa.”
“Wewe kamjaribu kumuambia hivyo.”
“Poa nitafanya hivyo, ngoja nijiandae niondoke.”
“Ok poa.”
Nilifungua wallet yangu na kumpatia laki moja na nusu.“Take care of your appearance.” Alicheka.
“Hahahaaa.. Si ulipenda boga, penda na ua lake.”
“Bwana acha utani.” Nilisema
“Mimi sitanii.”
“Sawa.”
Baada ya kuoga pamoja nilimchukua Frank hadi bwenini, nikamshusha mbele ya
block yao na kutoka kuelekea nyumbani sikutaka kupokea simu hadi nifike.
Nilipokaribia kufika niliamua kuizima kabisa, nilipiga honi na geti lilifunguliwa
mara moja, familia nzima ilitoka na kusimama nje kana kwamba walikuwa
wakinisubiria mimi....................
INAENDELEA................

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search