Friday, 4 May 2018

RAIS MAGUFULI AZISHUKIA SHULE BINAFSIRais wa Jamhuri a Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, amefunguka juu ya kutofurahishwa na mfumo wa shule binafsi hapa nchini, ambao unaonekana kutowatendea haki wanafunzi wote. 

Rais Magufuli amesema kitendo cha shule binafsi kuwachuja wanafunzi na kuchukua wale wenye uwezo mkubwa zaidi na kuwacha wale wenye uwezo mdogo ni ubaguzi, kitendo ambacho hakiwezi kufanywa na shule za serikali, kwani watoto wote wana haki ya kupata elimu. 
Rais Magufuli amesema shule binafsi lengo lake kubwa ni kutengeneza jina na kupata pesa, na sio kufundisha watoto wa kitanzania wawe na elimu sawa. 
Shule za private wanachujwa, wale vilaza wanaachwa na kuchukua wale cream ili kusudi wa-secure waonekane wao ndio wanaongoza, serikali inayopenda watu wake haiwezi ikafanya mambo ya kipumbavu hivi. Inachukua watoto wote, ukiangalia tangu mwaka 83 mpaka mwaka huu shule zinazoongoza 10 bora utakuta ni private, kama imebahatika serikali ni moja, tisa ni private, ni kwa sababu ya mlolongo wa wanavyofanya private. Hawako na interest ya kumsomesha kila mtanzania, interest yao ni pesa na kutengeneza jina, hiyo haiwezi kuwa point”, amesema Rais Magufuli. 
Ikumbukwe kwamba hivi karibuni uliibuka mvutano bungeni baina ya Wabunge wakilaumu serikali kuminya shule binafsi, na kuzifanya kutoweza kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search