Friday, 4 May 2018

RAIS WA CAF AIPONGEZA SERENGETI BOYS KWA KUTWAA UBINGWA

Baada ya kuwanikiwa kuutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la CECAFA (U17) huko Burundi kwa kuitwanga Somalia jumla ya mabao 2-0, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, Ahmad Ahmad, amekipongeza kikosi cha timu ya taifa ya vijana, Serengeti Boys.

Kwa mujibu wa Rais wa TFF, Wallace Karia, amesema kuwa amepokea pongezi za Ahmad akieleza kuwa amefurahia kikosi hicho cha vijana kulibebea taji hilo.

Karia ameeleza kuwa Rais huyo wa CAF amesema kutwaa ubingwa kwa Serengeti Boys ni manufaa makubwa kwa soka la Tanzania haswa kuandaa vijana ambao watakuwa msaada katika timu ijayo ya taifa.

Mbali na Rais wa CAF, Karia naye ameeleza kuwa siku zote katika mpira nchi haiwezi kufanya vizuri bila kuwa na kikosi cha vijana.

Kufanya vizuri kwa vijana hao, Karia amesema itabidi nguvu kubwa ziwekezwe kwa soka la vijana ili kuandaa wachezaji wazuri wa baadaye kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search