Friday, 18 May 2018

RC Paul Makonda ayakana makontena 20 yaliyokwama bandarini

IMG_20180518_115311.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amesema hajui chochote kile kuhusu kudaiwa au makontena yaliyokamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Hivi karibuni Mamlaka ya Mapato (TRA), imetangaza kusudio la kupiga mnada kontena 20 za Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa atashindwa kuzilipia ushuru na kuzichukua ndani ya siku 30 kuanzia Jumatatu.

Kontena hizo za Makonda ambazo zimesubiri utaratibu wa kuzitoa TRA kwa zaidi ya siku 90 zinazokubalika kwa mujibu wa sheria za kodi, zimesheheni samani za ndani na ofisini.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search