Monday, 28 May 2018

SERGIO RAMOS AMUOMBEA MO SALAH

Beki wa Mabingwa wa Kombe la UEFA Champions League, Sergio Ramos amesema kuwa hakudhamiria kumuumiza mshambuliaji wa Liverpol, Mohamed Salah katika mchezo wao wa fainali uliochezwa usiku wa kumkia leo.

Ramos ameeleza hayo kupitia ukurasa wake maalum wa kijamii baada ya mamia ya mashabiki wa soka ulimwenguni kumlaumu mchezaji huyo kuwa alikusudia kimakusudi kumfanyia madhambi mwenzake kwa kuwa kile kilichoonekana sio cha kawaida.

"Muda mwingine mchezo wa mpira wa miguu unakuonyesha upande wako uliokuwa mzuri na muda mwingine vilevile unakuonyesha upande mbaya. Zaidi ya yote sisi ni wamoja. Nakuombea upone mapema Salah", ameandika Sergio Ramos.

Salah aliumizwa na mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos na kutolewa dakika ya 31 baada ya kushindwa kuendelea na mchezo ambapo timu hizo zilikuwa bado hazijafungana. Baada ya Salah kutoka Real Madrid walifanikiwa kushinda kipindi cha pili kwa mabao 3-1 na kutwaa ubingwa wa 13 na wa taatu mfululizo chini ya kocha Zinedine Zidane ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo.

Mbali na hilo, Daktari wa timu ya taifa ya Misri Dkt. Mohammed Abu Ola amesema nyota huyo ana nafasi kubwa ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018 linalotarajiwa kuanza siku chache kutoka sasa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search