Friday, 11 May 2018

SIMABMABINGWA WAPYA WA LIGI KUU TANZANIA BARA -2017/2018

Image result for simba sc
Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imekabidhi rasmi ubingwa kwa watani wao wa Jadi, Simba SC baada ya kuchapwa bao 2-0 na wenyeji wao Tanzania Prisons 'wajela jela' mchezo ulichezwa katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya jioni ya leo Mei 10, 2018.

Bao la kwanza la wajela jela limepatikana mnamo mwa dakika 58 katika kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Eliuter Mpepo baada ya mchezaji wa Yanga Thaban Kamusoko kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Kama hiyo haitoshi ilipofikia dakika 83 za mchezo huo Tanzania Prisons walipata bao la pili kupitia Juma Abdul krosi iliyotengenezwa na Mohamed Rashis baada ya vuta ni kuvute na walinzi wa lango la Yanga.

Kutokana na ushindi huo wa Tanzania Prisons wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga yanaipa rasmi Simba SC ubingwa wa moja kwa moja wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/ 2018 na kuifanya timu hiyo kunyakua kikombe hicho mara ya 19 na mara ya mwisho kushinda ilikuwa ni mwaka 2012.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search