Friday, 18 May 2018

Simba na Yanga kushindania nafasi ya kucheza dhidi ya Everton

Gor Mahia ndio waliopata fursa ya kucheza na Everton msimu uliopita. Wikendi, walicheza dhidi ya Hull City
Image captionGor Mahia ndio waliopata fursa ya kucheza na Everton msimu uliopita. Wikendi, walicheza dhidi ya Hull City
Bingwa mtetezi Gor Mahia ni miongoni mwa timu nane za Kenya na Tanzania zitakazoshiriki mashindano ya kombe la SportPesa Super Cup mwezi wa sita mjini Nairobi.
Jumla ya dola 57,500 zitashindaniwa katika mashindano hayo ya wiki moja yatakayofanyika katika uwanja wa Kasarani.
Gor Mahia ni miongoni mwa timu nne za Kenya zitakazoshiriki pamoja na watani wao wa jadi AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz, anasema mwandishi wa BBC John Nene.
Wawakilishi wa Tanzania ni bingwa wa ligi kuu Simba, Yanga, Singida FC na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar.
Afisa mkuu wa mauzo ya kampuni ya mchezo wa kubahatisha SportPesa, Kelvin Twissa, anasema mashindano haya yatazidi kuboresha uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Kenya.
"Tumechagua timu bora zilizonawiri katika ligi zao kuu za nyumbani mwaka jana, na pia hii ni njia moja ya kukuuza vipaji vya kandanda eneo letu,'' alisema Twissa.
Rooney dhidi ya Gor MahiaHaki miliki ya pichaWAYNE ROONEY/TWITTER
Image captionWayne Rooney aliiongoza Everton kuishinda klabu ya Kenya ya Gor kwa kufunga bao zuri nchini Tanzania mwaka jana
Mshindi wa mashindano hayo atasafiri hadi England kutoana jasho na Everton katika uwanja wao wa Goodison Park mwezi wa saba.
Bingwa mtetezi Gor Mahia ndiyo iliyocheza na Everton mwaka jana jijini Dar es Salaam ikapoteza kwa mabao 2-1, wafungaji wa Everton wakiwa ni mchezaji nyota wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney na Kieran Dowell, naye Jacques Tuyisenge akaipa Gor Mahia bao lao moja.

Klabu zitakazoshiriki

  • Gor Mahia FC - Kenya
  • AFC Leopards - Kenya
  • Kariobangi Sharks - Kenya
  • Kakamega Homeboyz - Kenya
  • Yanga FC - Tanzania
  • Simba SC - Tanzania
  • Singida FC - Tanzania
  • Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) - Zanzibar
Gor Mahia ilifuzu kucheza na Everton ilipoibuka mshindi wa mashindano ya SportPesa Super Cup kwa kuizaba AFC Leopards mabao 3-0 mechi ya fainali jijini Dar es Salaam.
Katika mechi za robo-fainali, AFC Leopards ilishinda Singida FC kwa mabao 5-4 ya penalti baada ya sare ya bao 1-1, Yanga ikashinda Tusker ya Kenya mabao 4-2 ya penalti kutokana na sare tasa, Gor Mahia ikainyoa Jang'ombe 2-0 na Simba ikakatwa mkia na Nakuru All Stars ya Kenya kwa kumeza mabao 5-4 ya penalti kutokana na sare tasa.
Matumaini ya Nakuru All Stars kusonga mbele yalifikia kikomo mechi za nusu fainali ilipolimwa mabao 2-0 na Gor Mahia, huku Leopards ikiing'oa Yanga kwa mabao 4-2 ya penalti baada ya sare ya kutofungana. Katika mechi ya fainali Gor Mahia ilizima kidomodomo cha Leopards kwa mabao 3-0.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search