Thursday, 10 May 2018

STENDI YA MABASI YAENDAYO KASI KUHAMISHWA JANGWANI

Halmashauri ya jiji la Dar es salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi yaendayo haraka Udart kilichopo jangwani na kuhamishia kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT).


Hatua hiyo ni kutokana na eneo hilo la jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo.


Kufuatia kikao cha kawaida kilichofanyika jana cha Madiwani, Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita amesema uamuzi huo umefikiwa kunusuru magari hayo yasiendelee kuharika.Menejimenti ya kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo waweze kufikia mwafaka.


”kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendeyo kasi UDART cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inapomyesha" alisema Mwita.


Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha maji hadi baharini.


Kufuatia mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha jijini Dar es salaam, Jangwani ni moja ya eneo ambalo mara kwa mara limekuwa likikumbwa na mafuriko na kupelekea safari za mabasi ya mwendokasi kuhairishwa


Aidha kufuatia mvua zilizonyesha siku tatu zilizopita zimepelekea mabasi 29 kati 140 kuharibika na na kufanya baadhi ya wafanyakazi kupewa likizo mpaka marekebisho yatakapokamilika.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search