Friday, 18 May 2018

Steve Nyerere amchana Mama Kanumba

Image may contain: 2 people
Muigizaji filamu bongo Steven Nyerere amefunguka juu ya kitendo cha Mama Kanumba kutoridhishwa na kubadilishiwa adhabu Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alifungwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwanaye Kanumba.
Akizunguma na www.eatv.tv Steve Nyerere amesema kwamba amefuta namba ya mama Kanumba kwani hana shughuli naye, na asitake kushindana na serikali kwa sababu hata yeye ilimsaidia alipohitaji msaada.
“Mimi namba ya yule mama nimeifuta nimekasirika nimeona hana shughuli tu, kwa sababu anaongea vitu ambavyo havipo yaani, na sikioni kama kina tija, unajua kuna vitu vingine sio vya kukurupuka kuongea, unatakiwa ukae na watu wakupe hata ushauri, halafu yeye sio mtu wa kugombana na serikali, serikali alipokufa Kanumba ilimsaidia sana, hata hapo alipokuwa anaishi ni serikali ilimpa, yeye hakutakiwa kujibu chochote, alitakiwa kunyamaza na maisha yakaendelea, hata ukimfunga Lulu miaka mia, mtoto atarudi!? Sasa usiilazimishe jamii ikuone umefeli na usiilazimishe jamii ikuone una roho mbaya”, amesema Steve Nyerere.
Steve Nyerere ameendelea kwa kusema kwamba mama huyo hapaswi kulalamika sana kwani hana uhakika kama kweli aliua, kwani pia wawili hao walikuwa kwenye mahusiano.
Hata hivyo East Africa ilifanya jitihada za kumtafuta Mama Kanumba juu ya tuhuma mbali mbali anazopewa, na kusema kwamba hawezi kuzungumza kwa wakati huo.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search