Tuesday, 22 May 2018

UKIMJAMBISHA MWENYE BUSHA SASA KUPELEKWA MAHAKAMANI

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limewahatarisha wananchi wa Tanzania kiujumla kuachana na vitendo vya udhalilishaji kwa wanaume wenye mabusha kwa 'kuwajambisha' ama kuwapigia miruzi kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmed Msangi wakati akifanya mahojiano na eatv.tv baada ya kushamiri kwa matukio mengi ya udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia licha baadhi ya watu kutofahamu kuwa wakifanya ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi.

"Vipo vifungu vya sheria vinavyoweza kumfikisha mtuhumiwa wa kitendo hicho Mahakamani pamoja kutozwa faini kulingana na mfungua mashtaka atakavyokuwa anataka kulipwa fidia kutokana na udhalilishaji aliyofanyiwa",amesema Kamanda Msangi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search