Wednesday, 23 May 2018

UNAI EMERY ATANGAZWA RASMI KUWA KOCHA MPYA WA ARSENAL

Unai Emery Atangazwa Rasmi Kuwa Kocha wa Arsenal
Unai Emery ametangazwa kuwa meneja mpya wa Arsenal na afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Ivan Gazidis.

Bw Gazidis amesema Emery amepewa fursa ya kipekee ya kuongoza "sura mpya" yaklabu hiyo ya England.

Emery, 46, amejiunga na Gunners baada ya kuondoka PSG ambapo aliwaongoza kushinda ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1.

Ujumbe wa Arsenal wazuka na kupotea katika mtandao wa Emery, kulikoni?
Mhispania huyo pia alishinda vikombe vya ligi mara nne akiwa na miamba hao wa Ufaransa.

Awali alikuwa meneja wa Sevilla ambapo aliwasaidia kushinda Europa League mara tatu mtawalia.

Atamrithi Arsene Wenger ambaye aliondoka klabu hiyo baada ya kuwaongoza kwa miaka 22. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search