Tuesday, 8 May 2018

WAZIRI APIGWA RISASI

Waziri wa Mambo ya Ndani Pakistan, Ahsan Iqbal (59) amejeruhiwa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akiwa katika mkutano wa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Punjab.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari mbalimbali vinasema kuwa Waziri huyo amejeruhiwa katika bega lake la kushoto kufuatia risasi moja kumpata ambazo zilikuwa zikifyatuliwa na kijana ambaye mpaka sasa hajafahamika. 

Hata hivyo msemaji wa huduma za uokoaji Jam Sajjad Hussain amedai kuwa Waziri huyo alifanikiwa kuingizwa kwenye gari yake na kutoka katika eneo hilo aliloshambuliwa na kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi.

Mbali na hilo mtoto wa Waziri huyo amesema kuwa baba yake hajapata majeraha makubwa ambayo yanatishia maisha yake hivyo ni majeraha ya kawaida ambayo anaendelea kutibiwa na madaktari.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search