Wednesday, 23 May 2018

WAZIRI MAHIGA ASHANGAZWA NA JEZI ZA LIPULI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga, ameshangazwa na ubora wa jezi za nyumbani za Lipuli FC msimu huu, huku akiwapongeza watengenezaji na viongozi wa timu kwa usimamizi mzuri.

Tukio hilo limefanyika kwenye ofisi za Lipuli FC mjini Iringa baada ya Waziri kuitembelea klabu hiyo na uongozi kumkabidhi jezi ya timu hiyo ndipo akashangaa namna ilivyotengenezwa kwa ubora.

''Jezi nzuri sana hii imetengenezwa wapi'' ? aliuliza Waziri ambapo viongozi walimjibu kuwa imetengeza hapa Tanzania. Mbali na kushangaa jezi hiyo Waziri alieleza kufurahishwa na kiwango cha timu hiyo ambayo imepanda ligi msimu huu.

Kwa upande mwingine viongozi wa timu hiyo wamemuomba Waziri Mahiga kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wako wa mwisho msimu huu Mei 28 dhidi ya Kagera Sugar. Mchezo huo utapigwa uwanja wa Samora mjini Iringa.

Zaidi msemaji wa Lipuli FC Clement Sanga ameelezea kwenye video hapo chini mambo mbalimbali ambayo Waziri aliongea na viongozi wa timu hiyo ikiwemo mipango ya msimu ujao.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search