Thursday, 10 May 2018

YULE MWANASAYANSI WA AUSTRALIA AJIUA KWA KUJICHOMA SINDANO


Basel, Uswis. Mwanasayansi David Goodall amehitimisha safari yake ya hapa duniani baada ya kujichoma sindano mwenyewe ya sumu iliyochukua dakika moja kuchukua uhai wake.

Mwanasayansi huyo mwenye miaka 104 aliyehitimisha maisha yake ya kuishi hapa duniani alizaliwa jijini London Aprili mwaka 1914 ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kuanza vita ya kwanza ya dunia.

Mwanasayansi huyo mkongwe alisafiri kutoka Australia mpaka Basel, Uswis kwa ajili ya kujitoa uhai kwa hiari, ingawa alisema anachukizwa na kitendo hicho.

Goodall alishika bomba la sindano yenye sumu na kusukuma kwenye mwili wake, na ilitumia dakika moja sumu ikaenea mwili na kupoteza uhai wake.

Sindano ambayo aliitumia kujichoma ilikuwa na sumu aina ya Sodium pentobarbital ambayo iliingia kwenye mishipa ya mwanasayansi huyo.

Wasamaria wema walimchangia Dola 20,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh45milioni ili kumsaidia kutimiza azma yake hiyo.

Kabla ya kifo chake alisema kwamba kinachomfanya aharakishe kufa ni kutokana na kupungua kwa uhuru unaosababishwa na umri.

Hata hivyo mwili wake utachomwa moto nchini Uswisi na kisha majivu yatapelekwa nchini Australia

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search