Friday, 1 June 2018

Katibu Mkuu mpya wa CCM, Dk Bashiru Ally abadili msimamo kuhusu Katiba Mpya


Dar es Salaam. Katibu Mkuu mpya wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema msimamo wake kuhusu mabadiliko ya Katiba utakuwa tofauti na ule aliokuwa nao awali kabla ya kuingia rasmi kwenye siasa za CCM kwa kuwa sasa ataendana na maelekezo ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 31 baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa katibu mkuu, Abdulrahman Kinana, Dk Bashiru aliyekuwa akitetea mabadiliko ya Katiba amesema msimamo huo aliutoa kwa kuwa alikuwa huru.

"Leo nazungumza kama katibu mkuu, yaani swali lako lina majibu humohumo, ukiwa mchambuzi unachambua kwelikweli. Ukiwa msemaji wa chama unawasilisha yaliyoamuliwa kwenye vikao,"amesema Dk Bashiru.

"Msimamo wa Halmashauri Kuu ndio chombo kikuu kilichoniliteua na inaweza kunifukuza. Kwenye uchambuzi kule nisingeweza kufukuzwa. Hapa kama wewe unanitakia mema, siwezi kuchambua yale ambayo hayajaamuliwa na vikao."


Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search