Friday, 1 June 2018

MBUNGE ATAKA WATU WANAOKAMATWA WAKITOROSHA MADINI WAPEWE ADHABU HII

Mbunge wa Mtwara Mjini Maftaha Nachuma ameitaka serikali kuweka adhabu kali ikiwemo kuua watu ambao watabainika kutorosha madini ya Tanzanite.

Akizunguma leo Bungeni Dodoma Mbunge huyo kupitia tiketi ya CUF, amesema kwamba madini ya Tanzanite ambayo yako kipekee duniani, yanastahili kulindwa kwa hali ya juu, sambamba na kuyafanya kuwa kama nyara za serikali, na yeyote atakayethubutu kuiba na kuyatorosha akikamatwa auawe.

“Tunaambiwa madini ya Tanzanai huko nje yamezagaa sana kwa sababu utoroshwaji ni mkubwa, tunashukuru serikali imejenga ukuta lakini bado, tunaiomba serikali kama kweli ina nia ya dhati ya kuifanya Tanzanite kuwanufaisha watanzania, udhibiti wa haya madini unahitajika, napendekeza yawe nyara ya Taifa na mtu akikamatwa anatorosha hovyo hovyo ikiwezekana auawe na iwe fundisho,” amesema Nachuma.

Maftaha ameendelea kwa kusisitiza kwamba kama Serikali ingekuwa na nia ya dhati, ingenunua mashine za kuchakata madini ili Tanzanite ichakatwe hapa hapa kudhibiti utoroshwaji na kuweza kutoa ajira zaidi.
Chanzo-EATV

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search