Friday, 1 June 2018

Serikali yakiri mashine za EFD kutofanya kazi

mashine+pic.jpg
Dodoma. Serikali imesema inalishughulikia tatizo la kutofanya kazi kwa mashine za Kieletroniki za kutoa risiti (EFD), kwa sasa wataalamu wamepiga kambi ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kushughulikia jambo hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Mei 30, 2018 na Naibu Waziri wa Fedha na Mpango, Dk Ashatu Kijaji wakati akijibu mwongozo uliotolewa na Mbunge wa Sumve (CCM) Richard Ndassa.

Ndassa amesema mitaani pamoja na maeneo mbalimbali nchini mteja akinunua mafuta hawezi kupata risiti za EFD kama kawaida.

“EFDs zote hazifanyi kazi hii ni wiki ya tatu. Tangu tarehe 11, 2018 hakuna huduma hii. Inawezekana ni hujuma kwa Taifa. Nina uhakikika mapato mengi yatapotea. Serikali inasemaje kuhusu janga la Taifa?”amehoji.

Akijibu mwongozo huo, Dk Kijaji amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kwamba kwa mara ya kwanza lilijitokeza Mei 11, 2018 wakalishughulikia hali ikawa imerejea kawaida.

“Hata hivyo tatizo hilo limerejea tena, wataalam wa E government na kitengo chetu cha ICT pale TRA wamepiga kambi kulishughulikia jambo hilo,”amesema.


Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search